NA BASHIR YAKUB -
Sura ya 29
Sheria ya ndoa imeeleza
mambo mengi . Baadhi yanajulikana
na baadhi hayajulikani.
Wakati mwingine hata
baadhi ya yanayojulikana haijulikani
kama yameruhusiwa na
sheria au yanafanyika
kimazoea. Na hapa
ndipo inapoibukia migogoro mingi ambayo
tunayoshuhudia mahakamani na hata
nje ya
mahakama. Aidha sheria hii
imebeba mambo mengi ya
talaka, matunzo ya watoto
na mwanamke, jinai za unyanyasaji wa
kijinsia, ndoa haramu na
halali na mengine mengi
kuhusu familia na
ndoa. Mengi kati ya haya
yameishaelezwa kwa anayetaka
kuyajua basi atembelee SHERIA YAKUB
BLOG atafute atapata humo.
Leo ni
muhimu kuzungumzia jambo
jingine muhimu ambalo
nalo limekuwa likitatiza na kuleta
shida kwa wanandoa. Ni
kuhusu ruhusa ya kuoa
na kuoa mke
zaidi ya mmoja. Ndoa
zipo aina nyingi
na upo uhuru
wa mtu kufunga ndoa kutokana na
maamuzi yake na mwenza wake
wanavyoamua. Yumkini unapoamua
kufunga ndoa ya
aina fulani yakupasa
pia uwe umejua
matokeo, athari za ndoa
hiyo. Kila aina ya ndoa utakayofunga ujue
wazi kuwa itaambatana
na haki fulani
, wajibu fulani na
mipaka fulani. Hakuna
ndoa utakayoifunga iwe moja kwa
moja bila mipaka . Na hili
hasa ndilo linalojadiliwa na
makala haya.
1.AINA ZA
NDOA .
Kwa kuangalia namna
ndoa zinavyofungwa ndoa
zinagawanywa katika mafungu matatu
kama ifuatavyo.
( a ) Ndoa za kidini.Hizi
ni ndoa ambazo
hufungwa kutokana na
taratibu za dini za wahusika. Ikiwa dini
husika inaruhusu ndoa
hata kwa watu wenye dini
tofauti basi haitakuwa
shaka kwao ndoa itafungwa hivyohivyo.
Na ikiwa hairuhusiwi
basi taratibu za kubadilisha
dini kabla ya
ndoa zitafanyika. Ndoa hizi
huhusisha waislam, wakristo,mabudha
n.k na
hufungwa misikitini,
kanisani , kwenye tempo,na
pengine popote ambapo dini husika
itaruhusu ndoa kufungiwa. Wahusika hutakiwa
kufuata taratibu za
ndoa katika dini
hiyo kipindi chote
cha maisha yao .
( b ) Ndoa
za kimila. Hizi ni
ndoa ambazo hufungwa kutokana
na taratibu za mila
za jamii fulani. Jamii
yaweza kuwa kabila
au koo. Hata
hivyo mara nyingi ndoa hizi
hufuata kabila zaidi
kuliko koo. Utakuta ndoa
zinazofungwa kwa taratibu
za kihaya, kichagga, kiyao, kikurya
n.k. Ndoa hizi zinaruhusiwa
mpaka sasa ikiwa
unaona masharti ya
ndoa hizi yatakuwa
nafuu na utayaweza.Nasema hivyo
kwakuwa wapo wanaodhani
kuwa ndoa hizi zilikuwa
za zamani na
sasa hazipo.
( c ) Ndoa
za kiserikali. Hizi ni
ndoa ambazo hufungwa
kwa mujibu wa taratibu maalum
za serikali. Ndoa hizi
hufungwa kwa mkuu wa wilaya
au vinginevyo itakavyoelekezwa.
2..KISHERIA ALIYFUNGA
NDOA YA MKE
MMOJA HAWEZI KUOA
MKE WA PILI.
Kifungu cha 15
cha Sheria ya
Ndoa ndicho kinchozungumzia jambo
hili. Kifungu hicho kifungu
kidogo cha ( 1 ) kinasema kuwa
hakuna mwanaume atakayekuwa amefunga ndoa
ya mke mmoja
atakayeruhusiwa kuoa mke
wa pili. Ndoa zote
za kikristo ni
ndoa za mke
mmoja na hivyo
ni vema kueleweka
kuwa ni kosa
iwapo mtu atafunga
ndoa ya pili
ikiwa ya kwanza
inaendelea. Wapo wengi
hasa siku hizi
wanafanya hivyo lakini
ni vema basi ieleweke
kuwa kufanya hivyo
ni kosa na
ndoa hiyo ya
pili haiwezi kuwa
ndoa. Si ndoa
kwakuwa inaharamishwa na sheria na
lazima ieleweke kuwa aliyeolewa ndoa
hii hastahili haki
zozote za kindoa
ikiwemo ile ya
kugawana mali ndoa inapovunjika.
Pia kifungu kidogo
cha ( 2 ) kinakataza mtu
aliyeoa ndoa ya mke
zaidi ya mmoja
kufunga ndoa ya mke
mmoja. Mfano wa hili
ni pale ambapo muislamu
aliyeoa kwa taratibu
za kiislamu zinazoruhusu mke
zaidi ya mmoja
halafu tena afunge
ndoa ya kikristo
ambayo inaruhusu mke
mmoja tu. Hii
itakuwa sio ndoa
na jambo hilo haliruhusiwi.
Nitoe angalizo kujiepusha
na ndoa hizo
kwakuwa mwisho wa
siku ni hakuna
ndoa na wahusika
watalazimika kukosa haki
zote za ndoa
wakati wa kuachana au
kifo. Pia athari huenda
mbali zaidi mpaka
kwa watoto wanaozaliwa
katika ndoa hizi
ambapo hukosa kutambuliwa na
hivyo kukosa haki
za msingi ikiwemo
urithi.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment