NA BASHIR YAKUB -
Makala zilizopita nilieleza
mazingira ya kisheria ambapo
mtu anaweza kunyanganywa
ardhi yake na
kufutiwa hati miliki
na hatimye ardhi
kupewa mtu mwingine
au kukabidhiwa mikononi
mwa serikali. Nilieleza mambo
mengi ikiwemo sababu
ambazo zinaweza kupelekea mamlaka za
ardhi kufuta hati
miliki ya mtu. Pia
nilionya kuwa unapomiliki ardhi
sio kwamba umemaliza,
hapana, isipokuwa kuna umuhimu
mkubwa wa kuzingatia na
kufuata masharti yaliyo katika
hati miliki. Hii ni
kwasababu Sheria ya Ardhi
imeweka bayana na kutoa mamlaka
kwa ofisi kuu za
ardhi kufuta umiliki
wa mtu iwapo unakiuka
masharti ya hati.
Pia nikaeleza kuwa
yawezekana maafisa ardhi
kutumia mwanya huo kuchukua
ardhi yako kwa
manufaa fulani au kwakuwa
yupo mtu nyuma ya
mchezo huo ambaye
anaitaka ardhi yako. Utatumika mwanya
wa kutotekeleza masharti
kukunyanganya ardhi ili apewe
huyo aliyesimamia mchezo
huo. Na mwisho nikasema
kuwa huwezi kujua
kama haya yapo
mpaka yakutokee vinginevyo
unaweza kudhani tunaongea
vitu ambavyo havijawahi
kutokea. Waliofikwa na haya
wanajua nazungumza nini.
Ambao hawakusoma makala
hayo hawajachelewa andika
neno SHERIA YAKUB BLOG kwenye
mtandao na fungua blog
hiyo utaona makala
hayo na nyingine
nyingi za sheria. Makala ya
leo yatazungumzia matokeo
ya kufutiwa umiliki,
kwa mfano ikiwa
ardhi ulikuwa umeikopea
nani atalipa deni hilo, pengine ardhi
ilikuwa na mgogoro
mahakamani nani ataendeleza
mgogoro huo, pengine kuna
mtu alikuwa ameshalipia
ardhi hiyo nusu
kwa ajili ya kuinunua , haki zake zinalipwa na
nani, na vitu
vingine kama hivyo.
1.MATOKEO YA KUFUTIWA
HATI YA
ARDHI.
Kifungu cha 49( 2 – 5) cha Sheria
ya Ardhi ndicho
kinachozungumzia matokeo ya
kufutiwa hati ya
ardhi. Hapa chini
matokeo yataelezwa.
( a ) Matokeo ya kwanza kabisa
ni kuwa haki zote
za kuwa kama
mmiliki ikiwemo ile
haki ya kutumia
eneo zinakwisha palepale
na mtu anakuwa
anahesabika sio mmiliki
tena. Hii ina maana
hata ukikutwa ndani
ya eneo hilo
basi utahesabika kama mvamizi na ipo
haki ya kukufungulia
mashtaka ya madai ya uvamizi
kama mvamizi au ya jinai
pia kama mvamizi (criminal trespass). Hati miliki
inapofutwa si tu
mtu hatakiwa kulitumia
lile eneo isipokuwa
hata kuonekana eneo
hilo huwa ni kosa.
Haki zote za
umiliki alizokuwa nazo
mtu hurudi mikononi
mwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano
ambaye ndiye mdhamini
mkuu wa ardhi yote ya Tanzania.
( b ) Ikiwa kuna
kesi yoyote iko
mahakamani kuhusu ardhi hiyo
basi kama mtu
aliyefutiwa umiliki ndiye
aliyekuwa ameifungua kudai
baadhi ya haki kesi
hiyo itachukuliwa na
serikali na haki
hizo sasa zitadaiwa na serikali
na kama zitalipwa
malipo yataingia mikononi
mwa serikali. Lakini ikiwa
kesi hiyo aliyefutiwa
umiliki ndiye aliyekuwa
ameshitakiwa na anadaiwa
madai fulani kuhusu
hiyo ardhi basi
serikali pia itaichukua kesi hiyo na kuwa kama
mshitakiwa wa kwanza lakini
itamuunganisha mtu aliyefutiwa
umiliki kama mshitakiwa
wa pili na iwapo
hukumu itatoka ikitaka washitakiwa
walipe malipo yoyote
basi mtu aliyefutiwa
umiliki ndiye atakayetakiwa
kulipa na si
serikali.
( c ) Kama
kuna maendelezo yoyote ambayo
yalikuwa yamefanywa na mtu
aliyefutiwa umiliki katika ardhi
aliyonyanganywa basi
serikali itatakiwa kumlipa
fidia sawa na
gharama alizotumia.
Isipokuwa malipo hayo
yatatolewa tu iwapo
maendelezo hayo yalikuwa
ni maendelezo yaliyoainishwa
kwenye hati miliki. Kama
hayakuainishwa kwenye hati
miliki hakuna fidia.
( d ) Ikiwa kuna
kodi za ardhi au
tozo zozote ambazo
aliyefutiwa hati alikuwa
hajalipa basi atatakiwa
kuzilipa kwa kupewa
notisi ya siku
14 na kisingizio
kuwa amefutiwa umiliki
hakiwezi kutumika kutolipa
malimbikizo hayo.
( e ) Pia
serikali haiwajibiki kwa
namna yoyote kulipa Madeni yoyote
ambayo yalichukuliwa na
mtu aliyefutiwa umiliki
kwa kutumia ardhi
hiyo kama dhamana na pia haiwajibiki
kwa wapangaji, wanafamilia
au kundi lolote lenye
maslahi ya kuishi au biashara katika
ardhi iliyochukuliwa. Mizigo hii yote
ni ya mhusika
aliyefutiwa umiliki.
Kwa leo ni
hayo tu.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment