NA BASHIR YAKUB -
Watu wengi wana
maeneo lakini wameyatelekeza. Kwa mujibu
wa Sheria ya
Ardhi sura ya 113
kutelekeza eneo ni
kosa ambalo mtendaji
wake ambaye ni
mwenye eneo anatakiwa kuadhibiwa. Nitoe tahadhari
kuwa sio vema
watu kujisahau baada
ya kuwa wamemiliki
maeneo. Wakati mwingine si rahisi
kujua kama suala la
kufutiwa umiliki lipo ikiwa halijakufika. Lakini amini lipo
na wapo watu wamefutiwa umiliki
na maeneo yao
kuingia mikononi mwa
serikali au kugawiwa kwa watu
wengine.
Wakati mwingine huko
ardhi wako watu wanalitaka eneo lako
na wanakusubiri kwa
hamu ukiuke masharti ili
eneo lako wachukue
wao au wampatie mshirika wao ambaye
yuko nyuma ya
mchezo huo. Haya yapo sisi
tunaoshughulika na masuala
ya ardhi tumeyashuhudia sana. Binafsi ninazo
kesi ambazo watu
wamefutiwa umiliki na
maeneo yao wamepewa
watu wengine. Hivyo
hili si jambo
la mzaha hasa kipindi
hiki ambapo Wizara
ya ardhi imeamua
kufanya kazi kwa
kufuata taratibu na
kufuatilia kila jambo. Nimezungumzia
kutoendeleza maeneo lakini sababu
si hiyo tu bali zipo
nyingi kama tutakavyoona.
1.UTARATIBU WA
KUFUTIWA UMILIKI.
Sheria ya Ardhi
kifungu cha 48(1)(g)(I – iii)
imetoa maelezo ya taratibu (procedures) za
kufuata kabla mtu
kufutiwa umiliki wa ardhi
. Kifungu hicho kinaelekeza
kuwa kwanza mmiliki
aliyevunja masharti ya
umiliki ambayo tutayaona
baadae atatakiwa kupewa
taarifa rasmi ya
maandishi iliyo katika
mfumo rasmi ikieleza
masharti aliyokiuka mmiliki
na nini mamlaka
za ardhi zinatarajia
kufanya kutokana na
ukiukaji huo. Taarifa
atapewa mhusika na
hatafutiwa umiliki mpaka
zitakapoisha siku tisini
tangu kupewa ile
taarifa. Zitakapoisha siku tisini
na mmiliki hajafanya
kile kinachotakiwa basi
taratibu za kumfutia
umiliki zitaanza mara
moja.
Pili sheria inasema
taarifa ya kufutiwa umiliki itatakiwa kusambazwa
kwa wahusika wote
ambao wana maslahi
katika ardhi ile. Wenye maslahi
katika ardhi ni
kwa mfano kuna
taasisi ya fedha iliyomkopa mmiliki na ardhi
hiyo ndio ilitumika
kama dhamana, au ardhi ile
ni ya familia
na hivyo taarifa
hatapewa baba tu au mama
tu isipokuwa watapewa
wote wawili, au
ardhi kama ni ya urithi
basi taarifa atapewa
msimamizi wa mirathi
pamoja na warithi
wote.
2. NANI
MWENYE MAMLAKA YA
KUFUTA UMILIKI WA ARDHI.
Kifungu cha 48(3)
cha Sheria ya
Ardhi kinasema kuwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano
ndiye mwenye mamlaka ya
kufuta umiliki wa
ardhi. Aidha taratibu zote
za awali zitafanywa na kamishna
wa ardhi ikiwemo
ile ya kumpatia
mmiliki taarifa na baada ya
hapo atatoa taarifa
kwa rais pamoja
na mapendekezo yake
ya kutaka mmiliki kufutiwa
umiliki. Kwahiyo rais
husikiliza mapendekezo ya kamishna
wa ardhi kwakuwa ndiye
mwenye dhamana ya
sekta hiyo.
3. SABABU ZINAZOWEZA
KUSABABISHA UMILIKI WA
ARDHI KUFUTWA .
Kifungu cha 45 (2)(I – vi) cha Sheria
ya Ardhi kinaeleza
sababu za msingi
ambazo zinaweza kupelekea
mhusika kufutiwa umiliki
ardhi.
( a ) Kwanza ni iwapo
eneo limetelekezwa kwa
muda usiopungua miaka
miwili. Muda usiopungua miaka
miwili maana yake
ni kuanzia miaka
miwili na kwenda mbele. Kutelekeza eneo
kwa mujibu wa maana
hii hapa ni
pamoja na kutoonekana
ukishughulika na eneo
lako kwa namna
yoyote tangu upatiwe
umiliki.
( b ) Jaribio lolote
la kutaka kuuza
au kugawa ardhi
kwa mtu asiyekuwa
Mtanzania. Ni kosa mtu asiyekuwa raia wa
Tanzania kumiliki ardhi
hivyo jaribio lolote la
kumpatia ardhi linatosha
kuwa kosa la kufutiwa
umiliki.
( c ) Kama
eneo unalomiliki si
chini ya ekari
mia tano na
umekuwa hutumii eneo
hilo kwa namna ulivyoainishiwa matumizi yake kwa kipindi
kisichopungua miaka mitano.
( d ) Jaribio lolote
la kutoa ardhi kwa
mamlaka nyingine kinyume na
namna ulivyoagizwa na
mamlaka wakati unapewa
eneo husika.
( e ) Kutumia eneo
kinyume na masharti
yaliyo kwenye hati ikiwa ni
pamoja na matumizi yoyote
yaliyo kinyume na sheria
ya ardhi,sera,miongozo na
kanuni zake.
( f ) Pia
Rais kwa mamlaka aliyonayo anaweza
kufuta umiliki wa ardhi ya mtu yeyote kwasababu zozote
zinazohusu maslahi ya
umma.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment