Tuesday, 23 June 2015

JE WAWEZA KUUZA NYUMBA/KIWANJA ULICHOKOPEA BILA KUMPA TAARIFA ALIYEKUKOPA?.


Image result for NYUMBA YA MKOPO

NA  BASHIR  YAKUB - 

Wakati  mwingine  waliokopa  kwa  kutumia  viwanja /nyumba   huwa  na  mahitaji ya  kuviuza.  Wasiwasi  wao mkubwa  huwa  ni kwa  mtoa  mkopo  iwapo akijua  eneo  lililowekwa  dhamana  limeuzwa  . Pia  wanunuzi  wa  maeneo  ambayo  yamewekwa  dhamana  nao  wakati  mwingine  huwa  na wasiwasi  juu kununua  maeneo  kama   hayo.  Nilwahi  kueleza  namna  ya  kununua  ardhi  iliyowekwa  mkopo japo  sicho  ninachozungumza  leo. Leo naeleza  hadhi  ya  kisheria ( legal  status)   kwa watu  wa  aina  tatu. Kwanza sheria  inasemaje   kwa  aliyechukua  mkopo  na kuweka  dhamana  nyumba/kiwanja  na  sasa  anataka  kuuza  eneo  hilo  japo hajamaliza  mkopo. Pili  sheria  inasemaje  kwa  mtoa mkopo  ambaye  anagundua  kuwa  eneo  alilopewa  kama  dhamana  na  akatoa  hela  limeuzwa  bila  kupewa  taarifa. Tatu  Sheria  inasemaje  kwa  huyu  aliyeuziwa  eneo  lenye  mkopo.

1.KUUZA  NYUMBA/KIWANJA  CHA  DHAMANA.

Kwanza  ieleweke  vyema  kuwa  si  dhambi  hata  kidogo  kuuza   eneo  uliloweka  dhamana   ikiwa  hilo  litafanyika kwa  kuzingatia  misingi  maalum  ya  kisheria.  Kifungu  cha 68  cha  Sheria ya  Ardhi  kimezungumzia  habari  hii  kwa  namna   fulani.  Kubwa  zaidi  unapokuwa unaamua kuuza  eneo uliloweka  dhamana  wakati  ukijua  hujamaliza  deni    ni  kuhakikisha   haufanyi  hivyo  kwa  hila.  Uza   lakini  isiwe  kwa  hila. Kuuza  kwa  hila  kwa  maana  hii  hapa  ni  kuuza  ambako  kunalenga   kukwepa  kutolipa deni.Haya  yanatokea   sana,  mtu  anajua  ana  deni  na   eneo  lake  litauzwa  muda wowote  basi  anaamua  kuuza    akiamini  kuwa  yule  anayenunua  atajuana  na  watu  wa  mkopo  kwakuwa  yeye atakuwa  amekimbia  au  vinginevyo. Huku  ndiko  kuuza  kwa  hila.  Aidha  sheria   imeeleza  kuuza kutokuwa  kwa  hila  ambako ni kuuza  kwa kumshirikisha   mtoa  mkopo. Inatakiwa mtoa  mkopo  awe  amearifiwa  na  akijua  kila  hatua ya kinachoendelea.   Hii  ni kwasababu  pia  mwisho  wa  siku  mtoa  mkopo  atatakiwa  kukabidhi  kwa  mnunuzi  nyaraka  ya kununulia ardhi  kwakuwa  anakuwa  nayo  yeye  ikilinda  deni.

2.  JINAI  KWA  KUUZA  ENEO  LA  DHAMANA.

Wengi  wanaouza  maeneo  waliyoyaweka  dhamana  bila  kutoa  taarifa  kwa  watoa  mikopo   huwa  wanatenda  jinai  ya  kughushi.  Hii  ni  kwasababu   unapomuuzia  mtu  ardhi  ni  lazima  umpatie  nyaraka iwe  hati, leseni  ya  makazi, ofa  au  hata  mkataba  wa  kununulia ( sale  agreement).  Na  ikiwa  mtu  amechukua  mkopo  na  hajamaliza  kulipa  basi  nyaraka  hii  huendelea  kuwa  mikononi  mwa  mtoa  mkopo. Kutokana  na  hilo  ina  maana  mtu  huyu akiuza  atakuwa  hana  nyaraka  yoyote  na  akiwa  nayo  basi  ni  ya  kughushi . Mara  nyingi  haya  hujitokeza  maeneo  ambayo  hayana  hati  wala  leseni  za  makazi  ambapo   huwa  rahisi  kwa  mtu  kuandaa  mkataba  wa  kununulia  na  kumkabidhi  mnunuzi  kwa hadaa  kuwa  ndio  alionunulia.  Hii  ni  jinai  kubwa  sana  ambayo  huadhibiwa  vikali.

3. SHERIA  INASEMAJE  KWA  ALIYENUNUA  NYUMBA/KIWANJA  CHA  MKOPO  BILA  KUJUA.

Upo  msemo  wa  kisheria  usemao “buyer  be  aware”( Mnunuzi  kuwa  makini). Mara  kwa  mara  huwa  naeleza  namna ya kuwa  makini  unapotaka  kununua  ardhi. Mara nyingi  nimeeleza  mbinu  za  kufuata  ili  kununua  kitu  kilicho  halali.  Kwa  mazingira kama  haya mnunuzi  anakuwa  amepoteza  isipokuwa  anachoweza  kufanya  ni  kumfungulia  kesi  ya  madai  aliyemuuzia  akimdai  fedha  alizonunulia,  fidia, usumbufu na  gharama  alizoingia  na  hapohapo  anaweza  kumfungulia  kesi  ya  jinai kwa  udanganyifu  na  kughushi.  Lakini  haya  yote  yanawezekana  iwapo umebahatika  kumpata aliyekuuzia. Ikiwa  ameuza  na  kukimbia   basi  ni  rahisi  tu  kuhesabu  kupoteza.

4. SHERIA  INASEMAJE  KWA   MTOA MKOPO  ALIYEJUA  KUUZWA  KWA  DHAMANA  BILA  KUTAARIFIWA.

Kifungu  cha  70  cha  Sheria  ya  Ardhi  kinasema  kuwa  iwapo   mtoa  mkopo   atagundua  uuzwaji  wa  eneo  la  dhamana   bila  taarifa  yoyote  kwake  basi  atakuwa  na  haki  ya  kwenda  mahakamani  kuomba  kusitishwa  kwa  uuzaji  huo.  Kusitishwa  kwa uuzaji  kwa maana  hii  ni  pamoja na kubatilishwa  kwa  mkataba  wa  mauzo iwapo  tayari  mauzo  yamekamilika  au  kuzuia  kuendelea  na  uuzaji  iwapo  uuzaji   bado  unaendelea. Mtoa  mkopo   ataieleza  mahakama  kuwa  uuzaji  unalenga   kuingilia  deni  lake.

Angalizo  langu  ni  kwa wanunuzi  kuwa  makini  sana  katika  kununua  ardhi. Ardhi  zina  matatizo  sana   kuliko  inavyosemwa. Hakikisha  unafuata  taratibu  zote  za  kisheria za  manunuzi kama  ambavyo  nimekuwa  nikieleza  ikiwemo  kuandaliwa  mkataba  wa  kisheria  unaokidhi  haja  ya  mazingira  husika.

MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

                                           TANGAZO   MUHIMU                                                
VIWANJA     NA     NYUMBA          ZINAUZWA.
·        
WANASHERIA   WETU   WATAKUANDALIA   MIKATABA  YOTE  BURE  NA    KUKUSIMAMIA  MPAKA   MANUNUZI    YAKAMILIKE   BURE.
·        
UHALALI   WA  NYARAKA   NA   UMILIKI   UMETHIBITISHWA  NA                        WANASHERIA  WETU.
·        
UTAPEWA  MTU  WA  KUKUSAIDIA  KUFANYA  TRANSFER   KWA  HARAKA         BURE.
·        
IKIWA   UTATOKEA   MGOGORO  NDANI   YA  MWAKA  TANGU  TAREHE  YA       MANUNUZI    UTAPEWA   WAKILI   WA   KUSIMAMIA  MGOGORO    BURE
                                                        0784482959.

 KUONA   BOFYA  HAPO  JUU    MWANZO  WA   BLOG.
1 comments:

 • Ryan Kenneth R says:
  28 May 2017 at 15:54

  Hello!

  Unahitaji halali na ya haraka huduma ya mkopo?
  Kwa sasa sadaka 3% Mikopo ya yote Aina mikopo ya biashara, Mikopo kibinafsi, Gari Mikopo, kilimo Mikopo, au fedha Project? Sisi kutoa mikopo kwa makampuni na watu binafsi duniani kote, konsolideringen madeni, hata kama una
  alama ya chini ya mikopo na kutafuta ni vigumu kupata mikopo kutoka benki ya eneo lako au taasisi yoyote ya kifedha? , Na sasa kuwa na wakati mgumu kukabiliana na benki yako, au nyingine taasisi za fedha? Je, unahitaji haraka mkopo kama ndiyo Email yetu nyuma kupitia (ryanloaninvestment@outlook.com) sisi Kutoa kila aina ya Mikopo.

  Omba Sasa na kupata fedha yako haraka!

  * Kukopa kati 5000 na Euro 50,000,000
  * Chagua kati ya miaka 1 hadi 30 kulipa.
  * Flexible suala mkopo na masharti.

  mipango hii yote na zaidi, wasiliana nasi sasa.

  wasiliana nasi kupitia barua pepe: kwa ajili ya kampuni ya mkopo yeyote aliyenisaidia hapa ni maelezo yao mawasiliano (ryanloaninvestment@outlook.com)


  kuhusu
  Management.
  Wito simu: +27 (0603170517)
  Wasiliana Speedy yako Loan Sasa!

Post a Comment