Tuesday 9 June 2015

ASIYE MTANZANIA ANAWEZA KUMILIKI ARDHI KWA NJIA HII.




Image result for mzungu

NA  BASHIR  YAKUB - 

Ni  kawaida  kuwa  katika  sheria  za  nchi hii  mtu  asiye raia  wa Tanzania  haruhusiwi  kumiliki  ardhi. Ardhi  yoyote  iwe  ya  makazi  au vinginevyo.  Hii  ndiyo  sababu  tukiwa  tunatafuta  hati  au  tunabadilisha  majina  ya  hati  baada  ya  mauziano  ni  lazima  katika nyaraka  unazowasilisha  ardhi  uambatanishe  cheti  cha  kuzaliwa. Hii  ni  kutaka  kuthibitisha  ikiwa  muombaji  ni  Mtanzania  au lah. Na  hata itokee  muombaji  hana  cheti  cha  kuzaliwa  basi  sheria  inasema  anapaswa kuwasilisha  kiapo.  Pamoja  na  hayo  haipo  moja  kwa  moja  kuwa  asiye Mtanzania  hana  mamlaka  kabisa kabisa  ya kumiliki   ardhi.

Utajiuliza  swali  kuwa  ikiwa asiye  Mtanzania  haruhusiwi  kabisa  kabisa  kumiliki  ardhi  inakuwaje  ukipita  baadhi ya maeneo  unaambiwa  mashamba  haya ni ya  Muingereza au  eneo  hili  la  mgodi ni  la  kaburu. Wanapataje  ardhi hawa  ndicho  tutakachokiangalia. Lakini  sio  kujua  hilo  tu  bali  wapo Watanzania ndani  na  nje ya  nchi na  wana  marafiki  wasio  Watanzania  na  wangependa kuwekeza  katika  ardhi ya Tanzania au kuingia  nao  ubia kuwekeza  kwa  pamoja lakini  hawajui nafasi/ hadhi(status)  ya  ardhi  kwa  mgeni  ikoje. Pia  tutajua.

1.HAKI  MILIKI  ZA   ARDHI.

Hapa  nchini  ardhi  ya  iliyosajiliwa  huwa  katika  namna  mbili,  kwanza  ni  ile inayopatikana  kifungu  cha  24 – 30  cha  Sheria  ya  ardhi  ambayo  huwa  ni  hati( right  of  occupancy). Pili  ni  ile  inayopatikana  kifungu  cha  23  cha  sheria  hiyohiyo ya  ardhi  ambayo  ni  leseni  ya  makazi(residential  license).  Pia  huwa kuna  sajili  isiyo  rasmi  ambayo  huitwa  ofa. Kimsingi  ardhi  iliyosajiliwa  hutakiwa  kuwa na  nyaraka  hizo . Na  nyaraka  hizi  ni haki  ya  wenyeji  tu. Na  huwezi kupata  nyaraka  hizi  bila  kuthibitisha  kwa  cheti  cha  kuzaliwa  au  kiapo  kuwa  wewe  ni Mtanzania.

2.  ASIYE  MTANZANIA  KUMILIKI  ARDHI.

Kifungu  cha  20 ( 1 )  cha  Sheria  ya  Ardhi  kinaweka  bayana  kuwa , “kwa  kuondoa  shaka  mtu  asiye  Mtanzania  hataruhusiwa  kupewa  au  kumiliki  ardhi   isipokuwa  ardhi  hiyo  iwe  ni  kwa ajili ya uwekezaji  chini  ya  Sheria  ya  Uwekezaji” . Maana  nyepesi  kabisa  ndani  ya  kifungu hiki  ni kuwa  mtu  aliye mgeni  ambaye  si  raia  wa  Tanzania  ataweza  kupewa  ardhi  iwapo  tu  lengo  la  kupewa  ardhi  hiyo  ni kwa ajili  ya  uwekezaji . Hii  ndio  sababu  ukipita  mahali  utaambiwa  hilo  shamba   la  Mcanada,  ule  mgodi wa  Kaburu  na  maneno  mengine  kama  hayo.  

Kwa  hiyo  wasio  wageni  wanamiliki  ardhi  isipokuwa  kwa  masharti  ya  uwekezaji  ambayo  husimamiwa  na  kituo  cha uwekezaji  Tanzania ( TIC) ambacho  huongozwa  na  Sheria  ya  Uwekezaji 23.  Hata  hivyo  ardhi wanayopata  wageni ni  ile ilyoandaliwa  kwa  ajili  ya  uwekezaji  tu. Swali  ni ardhi  iliyoandaliwa  kwa  ajili  ya  uwekezaji  ni  ipi  na baada  ya  kumaliza  uwekezaji  ardhi  hiyo  huenda  kwa nani. Tutaona  hapa  chini.

3. MWEKEZAJI  AKIMALIZA  MUDA  WAKE ARDHI  ALIYOPEWA HUENDA  KWA NANI.

Mwekezaji  aliyepewa  ardhi  anapomaliza  muda  wake au  akanyanganywa  ardhi  kwasababu  yoyote  ile,  au  akafukuzwa  nchini  basi   ardhi  ile  hurudishwa  katika  miliki  ya  kituo  cha  uwekezaji  Tanzania(TIC).  Hata  hivyo  sheria  inampa  mamlaka  Waziri  wa  ardhi  iliyepo  kwa  muda  huo  kuigawa  ardhi  ile  kwa  mamlaka nyingine  yoyote  kadri  anavyoona  inafaa. Hii  ndio  sababu  utasikia mwekezaji  ameondoka  na  ardhi imerudi  mikononi  mwa  kijiji.
Juu ya  hilo  nimeeleza  hapo awali  kuhusu  asiye  Mtanzania  kupata  ardhi  iliyoandaliwa  kwa ajili  ya  uwekezaji  tu.

 Kwa  mujibu  wa  sheria  ya  ardhi,  Ardhi  iliyoandaliwa  kwa  ajili  ya  uwekezaji   ni  ile  ardhi  maalum ambayo  hutengwa na  serikali  na  kuikabidhi  kwa  kituo  cha  uwekezaji(TIC). Kwa hiyo  si  kila  ardhi  ni  ya uwekezaji  kwa ajili  ya  wageni  isipokuwa  ardhi  ya uwekezaji  huwa  imetengwa  maalum  hata  kabla  wawekezaji  hawajaja.  Si  tu  hutengwa  bali  pia huwa  imetangazwa  katika  gazeti  la  serikali  kuwa   heka  kadhaa, eneo  fulani  kuanzia  sehemu  fulani  mpaka   sehemu  fulani  ni ardhi  ambayo  imetengwa  kwa  ajili  ya uwekezaji .  Hivi  ndivyo ilivyo. 

MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

                                           TANGAZO   MUHIMU                                                
VIWANJA     NA     NYUMBA          ZINAUZWA.
·        
WANASHERIA   WETU   WATAKUANDALIA   MIKATABA  YOTE  BURE  NA    KUKUSIMAMIA  MPAKA   MANUNUZI    YAKAMILIKE   BURE.
·        
UHALALI   WA  NYARAKA   NA   UMILIKI   UMETHIBITISHWA  NA                        WANASHERIA  WETU.
·        
UTAPEWA  MTU  WA  KUKUSAIDIA  KUFANYA  TRANSFER   KWA  HARAKA         BURE.
·        
IKIWA   UTATOKEA   MGOGORO  NDANI   YA  MWAKA  TANGU  TAREHE  YA       MANUNUZI    UTAPEWA   WAKILI   WA   KUSIMAMIA  MGOGORO    BURE
                                                        0784482959.

 KUONA   BOFYA  HAPO  JUU    MWANZO  WA   BLOG.




1 comments:

  • Sweet Africa says:
    9 June 2019 at 07:48

    Swali langu je ikiwa ninayo ardhi na rafiki yangu toka nchi ya nje anahitaji tufanye kilimo cha Ubiya, hapo Sheria inamruhusu mgeni huyo kwa njia ipi?

Post a Comment