NA BASHIR YAKUB -
1.USHAHIDI WA
KUAMBIWA NININI.
Ushahidi wa kuambiwa
ni ushahidi unaotolewa
na mtu ambaye
hakuona tukio likitendeka,
hakusikia tukio likitendeka,
hakuhisi wala kuonja, wala
kunusa jambo lililo mbele
ya mahakama kama
kosa isipokuwa aliambiwa
na mtu mwingine aliyeona, kusikia, kuhisi, kunusa au
kuonja. Hapa kuna
watu wawili, kwanza
aliyeona au kusikia , na pili yule aliyeambiwa na
huyu aliyeona au
kusikia . Kwahiyo
katika maana yetu huyu
wa pili
aliyeambiwa na wa
kwanza aliyeona au
kusikia ndiye mwenye
ushahidi wa kuambiwa.
Ni
kwa maana hii tunasema
huyu wa pili
aliyeambiwa akienda kutoa
ushahidi wake mahakamani
utaitwa ushahidi wa
kuambiwa.
Kwa mfano “A” amemuona “ B”
akimuua “C”. “ A”
baada ya kuona
tukio lile akamwambia
rafiki yake “D”. Ina maana “D” hakuona
lolote isipokuwa ameambiwa
na rafiki yake “A” aliyeona. Kwa
maana hii ushahidi
wa “D” ni ushahidi
wa kuambiwa. Ameambiwa
na nani, ameambiwa
na “A” aliyeona
tukio. Hii ndio
maana ya ushahidi
wa kuambiwa. Kwa
jina la kitaalam
ushahidi huu huitwa “hearsay evidence” .
Na kwa jina
jingine la mtaani
huitwa “ ushahidi wa nilimsikia
akisema”.
2. SABABU NNE
KWANINI USHAHIDI HUU
HAUKUBALIKI.
( A ) Sheria
ya ushahidi kifungu
cha 61 na 62
kinauweka ushahidi wa
kuambiwa katika ushahidi
wa maneno( oral evidence) . Na kanuni
za ushahidi wa
maneno ni kuwa ili uweze
kukubalika kama ushahidi
sahihi ni lazima
kama swali ni
nani aliyeona tukio
likitendeka, basi jibu
awe nalo mtu
aliyeona tukio likitendeka,
na kama swali ni
nani aliyesikia tukio
likitendeka, basi jibu
awe nalo aliyesikia
tukio likitendeka, na
kama swali ni
nani aliyehisi au
kuonja kitu fulani ,
basi jibu awe
nalo mwenyewe kabisa
aliyehisi au kuonja kitu
hicho, na kama
swali ni mtaalam yupi
alipima na kugundua
kuwa jambo fulani lilisababishwa
na kadha wa kadha, basi
jibu awe nalo
mtaalam huyohuyo na
si vinginevyo.
Hii
ndio kanuni inayoongoza ushahidi
wote wa maneno (oral evidence). Kwahiyo kwakuwa ushahidi
wa kuambiwa nao
ni ushahidi wa
maneno lakini uliokosa
sifa hii basi mtu
aliyesikia kutoka kwa mtu aliyeona ushahidi
wake hauwezi kukubalika kwakuwa atapingana
na kanuni hii
inayotaka mwenyewe kabisa
aliyeona, kusikia au kusikia
kuwa ndiye awe shahidi.
Hii ni sababu
ya kwanza ya
kutokubalika ushahidi wa kuambiwa
au ushahidi wa nilimsikia akisema.
( B ) Pili
ushahidi wa kuambiwa
hautolewi kwa kiapo. Kawaida shahidi hutakiwa kuapa
mahakamani kabla ya kutoa
ushahidi na kiapo ndio kitu pekee
ambacho huthibitisha kuwa
mtu anachosema ni
kweli na kweli
tupu. Ikiwa mtu atatoa
ushahidi bila kuapa
basi ushahidi huo hauwezi
kuitwa kweli na kweli
tupu. Kwa mujibu wa sheria
ya ushahidi mtu
anayetakiwa kuapa ni yule
aliyeona tukio, kusikia, kuhisi,
kuonja au kuthibitisha
kitaaluma. Huyu ndiye anayetakiwa
kuapa. Kwa maana hii
aliyeambiwa anaweza kutoa
ushahidi lakini bila kuapa kwasababu
hairuhusiwi kwake kuapa . Na
kama haapi basi
ushahidi wake kuanzia
hapo huwa sawa na
bure, usio na maana
yoyote halikadhalika usiokubalika.
( C ) Pia
haukubaliki kwakuwa ni ushahidi ambao
ni mwepesi kuharibiwa. Hii ni
kwasababu aliyeona au
kusikia ni tofauti
na aliyeambiwa. Aliyeona
au kusikia si rahisi kusahau
alichokiona au kukisika lakini
aliyeambiwa ni rahisi
kusahau alichoambiwa chote au
sehemu yake au nukta
kadhaa za alichoambiwa.
Hali hii ya
kuwepo kwa uwezekano wa
kusahau huwa inamtoa
nje mtu huyu
aliyeambiwa kwakuwa muda
wowote anaweza kuharibu
ushahidi kwa kusahau
nukta kadhaa kwa
kuongeza au kupunguza
na hivyo kuathiri
uhalisi. Hii ni kawaida
hata wewe ukitumwa ukampe
maagizo mtu fulani
hautatoa maagizo vilevile
na kwa maneno yaleyale kama
aliyekuagiza alivyosema.Utaongeza au
utapunguza.
( D ) Mwisho, ushahidi
wa kuambiwa haukubaliki
kwa kuwa ni
ushahidi unaoacha kiu. Ushahidi
mzuri ni ule
unaomaliza kiu ya mahakama na
ya kila mtu. Hii ni kwasabbu
ushahidi wa kuambiwa
mpaka mtu aliyeambiwa
anapomaliza kutoa ushahidi
wake bado kila
mtu katika mahakama
hubaki akiwa na hamu
ya kumuona au
kumsikia aliyeona tukio kwa
macho yake na
akamsimulia huyu aliyetoa ushahidi. Kila mtu
hubaki na swali
la sijui huyu
jamaa aliyeshuhudia yuko
wapi. Hii ndio kiu
inayobaki na kuufanya
ushahidi huu kutojitosheleza. Ni sawa
na wewe uambiwe
na mtu aitwaye PATRICK
kuwa alimsikia ALOYS
akisema alimuona SAMUEL
akichoma moto nyumba yako.
Bila shaka utapenda
zaidi kumuona ALOYS ili akwambie
kilichotokea kuliko PATRICK
anayekusimulia ambaye hakuwepo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment