NA BASHIR YAKUB-
Siku zote wananchi
wamekuwa wakililalamikia jeshi la polisi
kwa namna linavyoendesha shughuli
zake hasa wakati wa ukamataji (arrest). Matumizi ya
nguvu, ubabe na kutofuata
sheria na taratibu
maalum limekuwa ndio
tatizo kubwa kwa
wananchi dhidi ya askari.
Sio
siri askari wamekuwa wakitumia
nguvu na ubabe
mno katika kuwakamata raia. Hata
pale pasipo na haja
yoyote ya kutumia
nguvu bado wao
wamekuwa wakilazimisha nguvu
nyingi hali ambayo
hupelekea vurugu , kuumizana na
hata mauaji. Mara nyingi
unapochunguza matukio mbalimbali
ya vurugu ambayo huwahusisha raia na polisi
utagundua kwa haraka kuwa ubabe
wa askari ndio uliopelekea
vurugu. Basi leo nitaeleza
nini ufanye askari
anapokiuka taratibu hasa wakati wa
kukamata/kuweka chini ya ulinzi.
1.NINI MAANA
YA KUKAMATA ( ARREST ).
Sura ya 20
Sheria ya Mwenendo wa
Makosa ya Jinai
kama ilivyofanyiwa marekebisho
2002 ndiyo sheria
inayotoa mwongozo wa
namna na jinsi
ya kumkamata mtu. Pamoja
na hayo sheria hii
haikueleza moja
kwa moja nini
maana ya kukamata. Hata hivyo
kutokana na miongozo mbalimbali ya
kimahakama ambayo hutumika
kutafsiri sheria hii tunaweza kupata
tafsiri ya neno
kukamatwa kwa kusema
kuwa ni tendo
la kumzuia kwa
muda raia ambaye
inatuhumiwa kwa kosa fulani,
ambalo
hufanywa na mamlaka
husika. Kwa tafsiri hiyo tendo la kuzuia lazima
liwe la muda,
raia anayekamatwa lazima awe
ametuhumiwa, na pia ukamataji lazima
ufanywe na mamlaka.
Huo ndio utakuwa
ukamataji ( arrest).
2. NANI
NA NANI WANARUHUSIWA
KUMKAMATA RAIA ( ARREST ).
Kwanza kifungu cha
14 cha Sheria
ya Mwenendo wa Makosa
ya Jinai kinampa mamlaka
askari polisi kumkamata au
kumweka chini ya
ulinzi raia mtuhumiwa . Hii ni
kusema kuwa mamlaka ya
kukamata aliyonayo askari yeyote
ameyapata kutoka kifungu
hiki.
Pili kifungu cha 18
cha sheria hiyohiyo
kinampa hakimu yeyote
mamlaka ya kumkamata
raia mtuhumiwa. Mahakimu wamegawanyika, wapo
mahakimu mahakama za
mwanzo, mahakimu mahakama za
wilaya na mahakimu mahakama za
hakimu mkazi. Hawa wote ni
mahakimu na wanayo mamlaka
ya kumkamata mtuhumiwa
kwa mujibu wa
kifungu hiki.
Tatu kifungu cha 16
cha sheria hiyohiyo kinatoa
mamlaka kwa raia yeyote kumkamata mtu anayetenda kosa.
Hapa tofauti ni kuwa
mamlaka ya raia
kumkamata raia mwenzake ni
madogo na huwezekana pale tu ambapo
mtuhumiwa ametenda kosa
kubwa na pengine
kuna wasiwasi kuwa
anaweza kutoroka asipozuiliwa
haraka na kwa
muda huo. Lakini kama
mazingira si haya basi
raia anatakiwa kutoa
taarifa polisi ili
wao wenyewe ndio wafanye
kazi hiyo.
3. MATUMIZI
YA NGUVU
HAYARUHUSIWI WAKATI WA
KUMKAMATA RAIA.
Kifungu cha 21
cha sheria hiyohiyo
kinakataza kabisa matumizi
ya nguvu wakati wa kumkamata
raia. Matumizi ya nguvu
ni pamoja na
kumpiga raia, kumfunga pingu, kumshika suruali
kwa kumningiza, kumtukana au matumizi
yoyote ya lugha
chafu na kila
kitu kinachofanana na
hayo.
4. SHERIA INAKURUHUSU
RAIA KUKATAA KUKAMATWA ASKARI ANAPOKIUKA
TARATIBU.
Katika kesi ya
Nzige Juma vs R (1964) EA 107 uk 147 mahakama
ilisema kuwa ikiwa
mtu atakamatwa bila
kufuata utaratibu basi mtu huyo anaruhusiwa kugomea
ukamataji huo. Huu ndio
uamuzi wa mahakama
na kwa mujibu
wa sheria uamuzi
wa mahakama ni sheria
na hivyo maamuzi
hayo ni sheria. Kwa sheria hii
nitoe mwito kwa
raia kutowaonea aibu
askari polisi wanaokiuka
taratibu ikiwa ni
pamoja na matumizi
ya nguvu katika
ukamataji kwa kuwagomea. Ieleweke kuwa
kugoma katika hili
si kuvunja sheria
bali ni kutekeleza sheria. Ni haki
yako kama zilivyo
haki zako nyingine. Na
kugoma katika hili
hakuwezi kukuletea shida
yoyote na hivyo
huna haja ya
kuwa muoga. Kumbuka
kama wewe mwenyewe hautaweza
kulinda haki zako
hakuna atakayelinda haki
hizo kwa niaba
yako. Wewe ndio unatakiwa
kuwa wa kwanza
kulinda na kusimamia haki
zako kwa msimamo
usioyumba na bila woga
huku ukiamini kuwa
uko salama mbele ya
sheria. Chukua hatua sasa kwa
kukataa na kugomea
ukamataji uliokiuka taratibu.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment