NA BASHIR YAKUB -
Mara nyingi unapounda
kampuni huwa ni
lazima kueleza katika
zile Memorandum kuhusu
ukurugenzi na wakurugenzi.
Huwezi kusajili kampuni ikiwa memorandum
zako
hazioneshi lolote kuhusu
hilo. Kimsingi nitaeleza machache
japo yapo mengi kuhusu
ukurugenzi na wakurugenzi katika
kampuni. Kwa kampuni
zetu ndogo ndogo za
kijasiriamali mara zote
wakurugenzi ndio hao hao
wamiliki na ndio hao
hao wana hisa. Niseme
mapema tu kuwa si kosa kuwa
hivyo isipokuwa yatupasa
kufahamu kuwa kuna
tofauti kati ya
wakurugenzi, wanahisa, na wamiliki.
Wakurugenzi
wanaweza kuwa watu
wa kuajiriwa na
wasiwe na uhusiano wowote katika
umiliki. Unakuta mtu ameajiriwa tu kama mkurugenzi kwa ajili
ya kuendesha kampuni
pengine kutokana na
elimu yake, uwezo
wake, uzoefu n.k. Mwanahisa naye anaweza
kuwa mwanahisa tu na
asiwe mkurugenzi na mmiliki
anaweza kuwa mmiliki tu
na asiwe mkurugenzi. Isipokuwa
tu mmiliki lazima awe mwanahisa kwasababu
hakuna namna ya
kufikia kuwa mmiliki
wa kampuni bila kuwa
mwanahisa.
Hivi ni vitu ambavyo
huwezi kuvitenganisha. Mara nyingi wanaotenganisha umiliki,
ukurugenzi na uanahisa
ni wenye makampuni
makubwa. Makampuni yetu madogo
ya kufuga kuku
mkurugenzi ndiye mmiliki
na ndiye mwanahisa. Tutaona
baadhi ya mambo hapa
chini kuhusu ukurugenzi
wa kampuni.
1.NINI MAANA
YA MKURUGENZI.
Sheria ya Makampuni
tunayotumia hapa nchini
imetoa tafsiri nyepesi
ya maana ya mkurugenzi
kwa kusema kuwa mkurugenzi ni
mtu yeyote ambaye
amepewa nafasi ya
ukurugenzi. Sheria hiyo
inasema hivyo kwa
kumaanisha kuwa ili umwite
mtu mkurugenzi au
hapana itategemea na
na majukumu anayotekeleza katika kampuni. Ni
majukumu tu ndio
yatamtambulisha mtu kama
mkurugenzi. Hii ina
maana yawezekana mtu
akawa anaitwa mkurugenzi lakini
hana majukumu ya
kiukurugenzi. Kwa tafsiri
hii huyu kisheria sio
mkurugenzi. Mwingine yaweza
kuwa anaitwa mwenyekiti
lakini akitekeleza majukumu
ya kiukurugenzi. Huyu
kisheria atatambulika kama
mkurugenzi. Kwa hiyo kwa
kujibu wa tafsiri
hii kumbe tunaona kuwa ukurugenzi
ni majukumu wala sio jina.
Pamoja na hayo
baadhi ya Mahakama huko Wingereza zimekuwa
zikitoa tafsiri mbalimbali
kuhusu maana ya ukurugenzi
ambapo tafsiri iliyokubalika
sana ni ile inayosema kuwa mkurugenzi ni mtu
ambaye ana mamlaka
ya kimwongozo, kimaadili
na kiutawala katika
shughuli zote na
za kila siku
za kampuni.
2. WANATAKIWA
WAKURUGENZI WANGAPI KATIKA
KAMPUNI ?.
Linapofika suala la
idadi ya wakurugenzi
kampuni hugawanyika mara
mbili , yaani kampuni binafsi( private company)
na kampuni za umma ( public
company). Kwa kampuni
binafsi hata mkurugenzi
mmoja inaruhusiwa, kwa maana
kuwa anaweza kuwa
mmoja au zaidi .
Kwa kampuni za umma
inaruhusiwa kuanzia
wakurugenzi wawili na kuendelea. Mkurugenzi mmoja
haruhusiwi.
3. MAJUKUMU
YA WAKURUGENZI.
Majukumu ya mkurugenzi
yeyote wa kampuni
ni mawili, kwanza
ni mdhamini na pili
ni wakala. Akiwa
kama mdhamini mkurugenzi
anao wajibu mkubwa
wa kuhakikisha mali
na fedha za
kampuni ziko salama. Kwa hiyo
kwa namna fulani anakuwa
kama mtu aliyewekeshwa
au anayelinda amana ya kampuni.
Akiwa
kama wakala mkurugenzi
anatakiwa kuwa kila analofanya analifanya
kwa niaba ya maslahi mapana
na mazuri ya kampuni. Kawaida kazi
ya wakala ni
kusimama badala ya fulani na
kuhakikisha anafanya vyema
kwa ajili ya fulani
anayemwakilisha. Wakala ni
mwakilishi na mkurugenzi
hiyo ndiyo nafasi
yake kwa kampuni.
Aidha mkurugenzi katika
kutekekeza majukumu yake
hayo mawili anapaswa kutekekeza
kila tendo lake
kwa uangalifu, umakini, weledi, na kutumia kila
mbinu kwa manufaa
ya kampuni.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment