NA BASHIR YAKUB -
Huwezi kufikiria umiliki wa kampuni kabla ya kufikiria kuhusu mtaji wa kampuni. Mtaji wa kampuni ni suala nyeti kwa wenye wazo la kumiliki kampuni au wanaomiliki kampuni tayari. Mtaji ndio kila kitu katika kampuni. Tangu unapokuwa katika harakati za kusajili kampuni utalisikia neno hili mtaji karibia katika kila hatua unayopita. Niseme mapema kuwa mtaji mdogo ndio kampuni ndogo na mtaji mkubwa ndio kampuni kubwa. Kwa hili mitaji imegawanyika mara mbili upo mtaji wa maandishi unaokuwa kwenye katiba na waraka wa kampuni( MEMAT) na upo mtaji wa mali halisi ( physical assets).
Mtaji wa unaokuwa
kwenye nyaraka nilizotaja mara nyingi hautambulishi
ukubwa au udogo wa
kampuni. Hii ni kwasababu
mtaji huu huwa
ni maandishi tu na
yawezekana kiwango cha fedha
kilichoandikwa humo kama mtaji
hakipo kabisa katika
kampuni. Hivyo mtaji
wa aina hii
hauna uhusiano wowote na
ukubwa au udogo
wa kampuni. Kwa
upande wa mtaji
wa mali halisi
huu ndio mtaji
ambao huweza kutambulisha
ukubwa au udogo
wa kampuni. Hii
ni kwasababu mtaji huu
huwa sio maneno
tu au maandishi bali
mali kwa maana ya
mali . Na kisheria mali
kama mali za
kampuni ndio mtaji
wa kampuni na
ndio nitakaozungumzia hapa. Nitazungumzia
mtaji lakini zaidi ni
kujua mtaji hujumuisha
nini.
1.CHIMBUKO LA
NENO MTAJI KATIKA
SHERIA.
Neno mtaji limeingia
katika sheria na
kuanza kutumika likianzia
kwenye sheria ya
udhamini (trust law), baadae likaingia
katika sheria za
mapato (revenue law) na
badae ndio sasa
likaingia katika sheria za
makampuni( company law). Kwahiyo neno
hili limeanza kutumika
katika sheria nyingine kabla
ya kutumika katika
sheria ya makampuni. Jaji maarufu wa Australia
Latham CJ amenukuliwa mara
kadhaa katika hukumu zake
mbalimbali akisema kuwa kisheria si rahisi kuwa
na maana moja ya neno mtaji . Hii
ni kwasababu ya
upana wa neno
lenyewe kimatumizi.
2. MTAJI
WA KAMPUNI NI NINI
NA NINI.
Unaposikia mtaji
wa kampuni mambo
manne hujumuishwa kama
ifuatavyo.
( a ) Pesa yote ambayo
imetolewa na wanachama na kuichangia
katika uanzishwaji wa
kampuni huitwa mtaji. Ni
kawaida kampuni inapokuwa inaanzishwa
wanachama kuunganisha nguvu
na kupata pesa
kwa ajili ya
uendeshaji. Pesa hii huitwa
mtaji na mara nyingi
mtaji huu ndio
unaojulikana kwa wengi.
( b ) Mkopo nao
ni mtaji. Pesa yote
ya kampuni ambayo imekopwa
kutoka taasisi za fedha, watu binafsi, mashirika, na
kila pahali pia nayo
ni mtaji . Si sawa kufikiri kuwa
kwakuwa pesa hiyo
ni deni basi
si mtaji wa
kampuni. Ni kawaida kwa kampuni
kukopa na pesa hii
huwa mtaji bila
kujali imekopwa ili
itekeleze shughuli ipi katika kampuni. Hii
ina maana hata ikikopwa leo
kwa ajili ya
kulipa mishahara ya wafanyakazi na
ikatumika yote ikaisha
bado inaendelea kuhesabika kama
pesa iliyoingia katika
mtaji wa kampuni.
( c ) Mali ( assets ) za kampuni ambazo si
fedha nazo huhesabika
kama mtaji wa
kampuni. Mali zaweza kuwa magari, baiskeli, nyumba, vifaa vya
kutendea kazi na kila
kitu ambacho ni
mali. Hii ina maana kuwa
ikihitajika taarifa yoyote
ya kutoa ufafanuzi
juu ya mtaji wa kampuni
basi mali hizi
nazo zote huhesabiwa
na kuingia katika
mtaji wa kampuni.
( d ) Pia
faida yoyote ambayo
haijagawiwa huingia katika mtaji wa
kampuni. Ni kawaida
kwa kampuni kutoa
mgao wa faida
kwa wanahisa wake
kila baada ya
muda fulani ambao
umepangwa. Faida ile inapokuwa
bado katika mikono
ya kampuni haijagawiwa
kwa wahusika inahesabika
kama mtaji wa kampuni. Ni
mpaka itakapotoka mikononi
wa kampuni ndipo
itakuwa si mtaji wa
kampuni tena.
Haya niliyoeleza wenye makampuni
makubwa wanayajua vyema. Tofauti
na wajasiriamali wenye makampuni madogo ambao wengi
wao huwa hawayajui haya .
Na
hawa ndio ninaowalenga
ili hata kama
anakuja mwekezaji wa
kutaka hisa katika
kampuni yako na anataka
kujua mtaji wa kampuni ni
kiasi gani basi mjasiriamali
huyu awe katika
uwezo wa kujua
mtaji hujumuisha nini na nini.
Au unapokuwa unaandika
taarifa ya kampuni na kuipost
sehemu mbambali ili
kuvutia wawekezaji basi
uoneshe mtaji wako
katika muktadha huo.
Huwezi kuingia ubia au
kumvutia mtu kuingiza
fedha katika kampuni au kumpata
mwekezaji mkubwa ndani ya
kampuni bila kujibu
swali la mtaji. Hii
ndio sababu na
umuhimu wa makala
haya.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment