NA BASHIR YAKUB -
Unapomiliki au
kuwa na
wazo la kumiliki
kampuni ni vema
pia kujitahidi kujua mambo
kadhaa yanayohusu kampuni.
Kampuni kama kampuni inayo
mambo mengi sana. Katika
hayo mengi si lazima
ujue yote isipokuwa yafaa ujue
japo machache ya
msingi ili upate ufanisi wa kuendesha
kampuni. Wengi waliofungua
makampuni hawajui hata
mambo madogo yanayohusu
kampuni na uendeshaji
wake . Unamkuta mtu anamiliki
kampuni kwa mwaka
wa tano lakini
hajui nini maana ya hata neno
Limited( LTD) ambalo
limeandikwa kwenye kampuni
yake.
Hii ni tofauti na
wenzetu wazungu ambao
hujishughulisha na kujua
mambo ya msingi
katika shughuli zao
mbalimbali wanazoziendesha. Kutokana
na hili nimekuwa nikieleza
mara kwa mara
baadhi ya mambo ya
msingi kuhusu kampuni.
Nakumbuka nimewahi kueleza namna
ya kuunda kampuni, maana ya neno limited,
namna ya kuandaa
mahesabu ya kampuni, jinsi ya
kununua na kuuza hisa, na
mengine mengi. Kwa anayetaka kuyaona haya
atembelee SHERIA YAKUB
BLOG. Leo tena naeleza
kitu kingine ambacho
ni, Maana ya hisa
na aina zake ( shares) .
1.NINI MAANA
YA HISA.
Hisa ni maslahi ya
kila mwanahisa aliyonayo katika kampuni
fulani. Yaani wewe kama ni
mwanahisa katika kampuni fulani basi
yale maslahi yako au
kiwango chako cha uwekezaji
ulichowekeza katika ile
kampuni ndio hisa zako. Kama mko
watu kumi katika
kampuni basi kila
mtu ana maslahi
au kiwango kadhaa cha uwekezaji ambapo
ukikusanya uwekezaji huo kwa
pamoja ndio utaitwa
hisa za kampuni. Uwekezaji
au maslahi katika
kampuni hutofautiana kutokana
na uwezo
wa kila mwanahisa.
Tofauti hutokana
na kiwango cha kila
mtu alichowekeza. Kuna mwenye hisa
kumi, kuna mwenye ishirini,
kuna mwenye hisa mia n.k. Hisa
siku zote hupimwa
kwa kiwango cha pesa.
Yawezekana uwekezaji wa mtu
kwenye kampuni ni magari
yaani amepata hisa kwa
kuchangia magari. Mwingine
amepata hisa kwa
kuchangia ofisi. Na mwingine
amepata hisa kwa kuchangia vifaa
vyote vya ofisi.
Katika kuhesabu hisa
michango hii yote
itawekwa katika viwango
vya pesa na
itasemwa kuwa fulani ana hisa za shilingi kadhaa
na sio ana hisa
za magari au vifaa kadhaa. Kwa
hiyo hisa huhesabiwa
kwa mtindo/viwango vya
fedha.
2. AINA ZA
HISA.
Hisa sio hisa
kama wengi tunavyojua
isipokuwa hisa zina
aina zake. Sio kila
mwenye hisa ana
hisa isipokuwa ana
hisa gani au za aina
gani. Aina za hisa za mtu katika
kampuni ndio humwezesha
kujua ana haki
gani katika kampuni, ana
wajibu gani na anawajibikaje likitokea
tatizo. Kwa hiyo haki,
wajibu(duty) na uwajibikaji(liability) katika
kampuni hutofautiana kutoka
mwanahisa mmoja hadi
mwingine kutokana na
aina za hisa anazomiliki. Wanahisa
wote hawana haki
sawa, hawana wajibu
sawa na hawawajibika
sawa pamoja na kuwa
katika kampuni moja. Hapa chini tutaona aina
za hisa.
( a ) HISA
ZA WAMILIKI ( EQUITY
SHARES).
Hizi ni aina
za hisa ambazo
huwa ndio nyingi
katika kampuni. Wale wanaomiliki
hisa nyingi katika
kampuni hisa zao huitwa hisa
za wamiliki. Huitwa
hisa za wamiliki
kwakuwa hawa huhesabika
kama ndio kampuni
yenyewe na hivyo
wenye hisa hizo
ndio wamiliki wa kampuni. Nimesema
hapo juu kuwa
wanahisa hawana haki sawa, wajibu
pamoja na uwajibikaji.
Wenye hisa hizi
wana haki kubwa
ya kimaamuzi katika
shughuli zote za uendeshaji
wa kampuni kwakuwa wao
kila hisa moja huwa ni
kura moja na
kwahiyo kila kitu
hupitishwa kwa kura
zao. Pia wana
haki ya kupata mgao
mkubwa kuliko wengine. Hata
hivyo wanawajibika zaidi
linapotokea tatizo kwa
mfano inapotokea hasara
wao ndio hupoteza
zaidi. Kwa jina jingine
hisa za hawa
huitwa HISA ZA
SIMBA( LIONS SHARE). Hii ni
kwasababu huko mwituni
simba hupata mgao
mkubwa wa nyama kati ya
wanyama wote.
( b ) HISA ZA
KAWAIDA.
Hizi ni zile
hisa ambazo humilikiwa
na watu wengine
wa kawaida katika
kampuni. Mara nyingi hawa
ndio huwa wengi
japo kila mtu
huwa na hisa kidogo kidogo. Mgao wao
wa faida hutokana
na asilimia ya kile
mtu anachomiliki. Maamuzi yao
katika kampuni huwa
ni madogo ukilinganisha na
wenye zile hisa za
umiliki( equity shares). Hata
hivyo uwajibikaji wao
nao ni mdogo pia kwani
hupata hasara kidogo
pale kampuni inapopata
hasara. Pamoja na
hayo sheria imewapa
kipaumbele cha kupewa
mgao wa faida kabla ya
kundi jingine lolote.
( c ) HISA ZA
WAANZILISHI ( DEFERRED SHARES).
Hizi ni hisa ambazo
hutolewa kama zawadi kwa
waanzilishi wa kampuni. Mgao wa
faida wa hisa hizi huwa
sio wa moja kwa moja
isipokuwa hutegemea na
faida inayozidi. Kawaida mgao wa
faida kwa wanahisa
wengine hutoka katika
faida ya kawaida lakini hawa
hawapewi mgao kutoka
faida ya kawaida
isipokuwa hupata pale faida inapozidi
au kuvuka kiwango ilichotegemewa.
( d ) HISA
ZA KAMPUNI( CORPORATE SHARES).
Zote nilizotaja juu ni
hisa za kampuni
lakini bado jina
hili hupewa hisa hizi
kutokana na kuwa
ni hisa maalum
ambazo hutolewa kwa
waajiriwa/wafanyakazi katika kampuni husika. Waajiriwa hutengewa hisa zao
na mwenye uwezo
huweza kuchukua hisa
hizo kwa kiwango
cha uwezo wake.
Mwajiriwa huendelea kuwa na
hisa hizo hata baada
ya utumishi wake
kukoma . Kwa ufupi
sana niseme tu
kuwa hisa sio
hisa ila hisa
ni una hisa
za aina gani.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
Asante kwa kunielimisha kuhusu hisa Mara kadhaa nimejaribu Ku Google lakini ckupata kwa undani kama ulivyo eleza
Asante kwa ufafanuzi mzuri
Asante kwa ufafanuzi mzuri
Ahsantee sana
Thanks very much
Sikua nafaham leo ndo nimefaham
Kwamfano tumeanzisha ushirika unajumla ya watu 10, tukatoa ada ya 150,000/- kila mwanaushirika kwa ajili ya kupata mtaji wa kunzisha biashara, hapo hisa ya kila mwanaushirika inakua vip?