NA BASHIR YAKUB-
Malalamiko ya
raia dhidi ya
jeshi la polisi
hayataishi kama polisi
wenyewe hawatajirekebisha. Na
ieleweke kuwa si kweli
kwamba wanaolalamika ni wajinga
au hawana sababu za msingi.
Mara zote ukiangalia
malalamiko ya raia huwa
ni ya msingi na
mzizi wake ni mmoja
tu. Ni utamaduni
wa askari wetu
kutopenda kutenda hatua
kwa hatua kama sheria
inavyoagiza. Sheria imetoa maelezo
mazuri tu ya namna
ya kuyaendea mambo. Tatizo
watekelezaji ndio hakuna.
Sheria husema
kingine na watekelezaji
hufanya kingine.
Namna hii
huwezi kuepuka chuki
na migongano kati
ya hawa watekelezaji
askari na raia. Na
migongano na kutokuelewana kunapokuwa
kukubwa na usalama
nao unayumba kwakuwa
ili askari afanye
kazi ya usalama
vizuri anategemea msaada
wa raia karibia
kwa asilimia zaidi
ya 80. Na
raia huyu hatatoa ushirikiano wakati
jana umempiga bila
sababu, umemtukana na kumtolea maneno
ya kebehi. Makala iliyopita
nilizumgumzia namna sheria
inavyomruhusu raia kukataa
kukamatwa na polisi
iwapo polisi huyo
atakiuka taratibu katika
ukamataji. Leo nazungumzia
namna sheria inavyokataza kumchukua mtu
mwingine baada ya
kumkosa mtuhumiwa halisi
wa kosa. Tutaona
hili likoje.
1.ASKARI KUONDOKA
NA MTU MWINGINE
BAADA YA KUMKOSA
MTUHUMIWA HALISI.
Hii ni tabia
ambayo imezoeleka sana
na ipo kwa
muda mrefu. Yumkini kuzoeleka
kwake na kuwepo
kwake kwa muda mrefu hakuifanyi hata kwa sekunde
moja tabia hii kuwa halali
kisheria. Mara nyingi
wanaokutwa sana na tabia hii
ni watu wa vijijini hasa
wa hali ya chini. Lakini
hata mijini pia
ipo sana. Nazungumzia
tabia ya kuondoka
na mtu mwingine
baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
Kwa mfano askari
wamekuja nyumbani kumtafuta
JOHN kwa kosa
analotuhumiwa nalo. Bahati
mbaya au nzuri
JOHN hayupo nyumbani. Kutokana na hilo askari
wanaamua kuondoka na
mke wa JOHN
au mtoto wake
ili kumfanya JOHN
aweze kutokea. Hiki ndicho
ninachozungumzia. Na wanaokuwa wakichukuliwa
mara kwa mara ni
mke wa mtuhumiwa
, mtoto au ndugu. Lengo
eti ni kumfanya mtuhumiwa
halisi aweze kujisalimisha.
2. SHERIA
INAKATAZA KABISA KUMCHUKUA
MTU MWINGINE BADALA
YA MTUHUMIWA HALISI.
Ni lazima ieleweke
na askari wetu
wafahamu kuwa sheria iko
wazi kuwa aliyetenda
kosa ndiye anayewajibika
na kosa. Haiwi na
haitokuwa kosa la
fulani akaliwajibikia fulani. Askari wajue
kuwa kamwe kisheria hakuna
anayesimama kujibu kosa
la mwingine . Ni kutokana na
msimamo huu mahakama kuu katika
kutafsiri sheria mbalimbali
zinazokataza jambo hili ikasema katika kesi ya
LULU TITU vs R ( 1968 ) HCD No. 330 kuwa
ni kosa kubwa
kwa askari kumkamata
au kuondoka na
na mtu mwingine
baada ya kumkosa
mtuhumiwa . Katika kesi hiyo
askari walikuwa wamemkamata
na kumchukua mke
wa mtuhumiwa baada
ya kumkosa mme
wake ambaye alikuwa
anatuhumiwa. Mahakama ilikemea
vikali jambo hilo
na kutia msisistizo
juu uharamu wake
kisheria. Maamuzi ya mahakama ( mahakama kuu
na ya rufaa)
ni sheria na hivyo
msimamo huo ni sheria.
3. NINI
UFANYE HILO LIKIKUTOKEA AU
KAMA LIMEKUTOKEA TAYARI.
Kwanza kesi hiyo
niliyotaja hapo juu
haikuishia kukemea jambo
hilo bali ilienda
mbele zaidi kwa kutoa
mwongozo wa nini mtu
afanye iwapo limemtokea
hilo . Mahakama ilisema kuwa
iwapo mtu amechukuliwa
bila kuhusika basi
anayo haki ya
kufungua shauri la
madai na kudai kulipwa
fidia. Katika shauri
la madai la namna
hii utamfungulia askari husika
lakini pia utaliunganisha jeshi
la polisi ambalo
ni mwajiri wa
askari huyo/hao. Lengo
la kuliunganisha jeshi
la polisi ni ili hukumu
itakapotoka ya kulipwa
fidia basi jeshi
hilo ndilo lilipe fidia
kwa niaba ya askari wake. Ndugu Mtanzania hakuna shaka fidia utalipwa
tu kama hili
limekutokea kweli.
Pili kitu kingine
ambacho unaweza kufanya
ni kugomea kukamatwa/kuchukuliwa. Katika
kesi ya JUMA NZIGE vs R (1964) EA 107
mahakama ilitoa mwongozo
kuwa raia ana
haki ya kugomea
ukamataji wowote ambao si
halali. Kwa maana
hii ikiwa we
si mtuhumiwa basi
unaweza kukataa kukamatwa na
hakuna lolote litakutokea
kwakuwa uko sahihi
mbele ya macho
ya sheria. KATAA UNYANYASAJI, CHUKUA HATUA.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment