NA BASHIR YAKUB -
Kifungu cha 112 ( 1 )
na ( 2 ) cha Sheria ya Mwenendo
wa Kesi za
Jinai
kinaeleza
kwa urefu kuhusu
hati ya kumkamata
raia ( warrant of arrest )
ambayo hutolewa na
mahakama. Kifungu hiki kimeeleza
namna hati hii
inavyopaswa kuwa na maudhui
yanayopaswa kuwa ndani ya hati
hiyo. Lengo ni
kumfanya raia ajue anakamatwa na
nani , kwanini na anapelekwa wapi. Ni
hati ambayo imebeba taarifa
zinazolenga kusimamia na kulinda
haki za mtuhumiwa . Yumkini mengi yaliyo
katika hati hii
huwa hayatekelezwi na
wahusika. Raia wajue
kuwa amri ya kukamatwa
kwa mtu inapotolewa na
mahakama ni lazima askari
anayekuja kukamata awe
na hati hii. Asije askari
kukukamata kwa maelezo kuwa
ametumwa na mahakama
wakati akiwa hana hati
hii. Nisisitize tena kuwa
amri ya kumkamata
raia inapotolewa na mahakama mkamataji askari
lazima aje na hati
hii kwa ajili ya kutekeleza kazi
hiyo. Na ili
hati iwe halali
lazima iwe na
taarifa zifuatazo kama
tutakavyoona hapa chini.
1. HATI LAZIMA
IWE NA TARIFA
HIZI.
( A ) LAZIMA HATI YA KUKAMATA IANDIKWE
NA JAJI AU
HAKIMU.
Upo utaratibu ambao
umezoeleka ambapo makarani
wa mahakama huandika hizi hati. Hili
ni kosa kubwa
kwani kifungu hichohicho
cha 112 cha Sheria ya
Mwenendo wa Kesi
za Jinai kimeweka
wazi kuwa hati
ya kukamata ni lazima
iandaliwe na hakimu
au jaji. Afisa
yeyote wa mahakama ambaye si
hakimu au jaji
hana kabisa mamlaka
ya kuandaa hati hiyo.
Basi kama ndio
hivyo ieleweke kuwa
hati yoyote ambayo haikuandaliwa
na hakimu au
jaji ndio hati batili na
ukamataji unaotokana na
hati hiyo ni
ukamataji haramu. Nimeeleza katika
makala zilizopita kuwa
sheria inamruhusu raia
kugomea ukamataji ambao
ni haramu kama
huo. Hivyo niseme tena
kuwa ikiwa hati
ya kukamata haikuandaliwa
na hakimu au jaji basi
raia anayo haki
ya kugomea kukamatwa.
( B ) LAZIMA HATI
YA KUKAMATA IWE
NA MUHURI WA
JAJI AU HAKIMU .
Kawaida kila mahakama
ina muhuri wake
ambao huwa na utambulisho wa Mahakama
husika.
Muhuri huo huwa
nao jaji au hakimu wa
mahakama husika. Muhuri
huo ndio unaotakiwa
kuwa katika hati
ya kukamata. Kama ni hati imetolewa
na mahakama kuu
muhuri uoneshe kuwa
ni wa mahakama kuu halikadhalika
mahakama nyinginezo kama za
wilaya na mwanzo.
( C ) HATI YA
KUKAMATA LAZIMA IONESHE
KOSA LA MTUHUMIWA
KWA UFUPI.
Mpaka hati inatolewa
kunakuwa na kosa
ambalo tayari raia
ametuhumiwa nalo. Hati
hii haiwezi kutolewa
iwapo hakuna kosa
ambalo limeanzishwa. Kutokana na
hilo ni lazima
kosa hilo lioneshwe ndani ya hati
hiyo ili mtuhumiwa
ajue anakamatwa kwa
ajili ya nini
ili naye ajue anaandaa
nini na nini kuhusu kosa
hilo. Kwa mfano kosa liandikwe hivi, KUUA KWA
KUKUSUDIA KINYUME NA KIFUNGU 196 CHA
KANUNI ZA ADHABU.
( D ) LAZIMA HATI
IONESHE JINA LA
MTUHUMIWA AU WASIFU
WAKE.
Isiwe hati imetolewa kwa
ajili ya JOHN
ikatumika kumkamata CLEMENT.
Aliyeandikwa kwenye hati
ndiye huyohuyo anayepaswa
kukamatwa. Hii ndio sababu
ya hati hiyo
kuwa na jina. Kama
haina jina basi
iwe inachambua wasifu
wa mlengwa kwa
namna hivyo hivyo alivyo. Kama
haina jina au wasifu wa
mlengwa basi hati hiyo
sio halali na
mtuhumiwa anaweza kuigomea.
( E ) LAZIMA ITAJE
JINA LA ASKARI/AFISA ALIYETUMWA
KUKAMATA .
Si kila askari
anamkamata anayemtaka. Hati ya
kukamatwa hueleza askari/afisa
maalum aliyepewa wajibu
wa kukamata mhusika. Itamtaja
kwa jina kuwa
huyu ndiye aliyepewa
mamlaka ya kumkamata
fulani.
Haya yote ni
kwa mujibu wa
kifungu cha 112 ( 1 ) ( 2 ) cha
Sheria ya Mwenendo
wa Kesi za Jinai. ACHA
KUNYANYASWA, CHUKUA HATUA.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment