NA BASHIR YAKUB-
Kutokana na maendeleo
ya biashara duniani
kote imekuwa ni vigumu
sasa kufanya biashara
nje ya kampuni. Hii
ni kwasababu kila
kampuni au taasisi
utakayotaka kufanya nayo
biashara iwe kununua
kwao au kuuza
kwao basi kitu
cha kwanza watakachokwambia ni
kuwa hatufanyi biashara
na watu binafsi. Zipo
biashara ambazo watu
wengi bado wanazifanya
nje ya kampuni
lakini ukweli ni
kuwa biashara hizo
kwa ulimwengu wa biashara
wa sasa ni za
kienyeji na tija
yake bila shaka
ni ya kusuasua. Kwa hali
ilivyo sasa hadi migahawani unaposupply
mayai au kuku wa
nyama n.k sio muda mrefu watakwambia
sasa tunahitaji kampuni ndio isupply na sio mtu
binafsi . Kama hali
ni hiyo nini basi
mjasiriamali wa leo afanye.
1.NINI MJASIRIAMALI
AFANYE KWA SASA.
Kilio cha mjasiriamali
makini siku zote
huwa hali na wala halali
isipokuwa anawaza nini
kesho afanye ili
biashara zake zitoke
hapo zilipo na kwenda
hatua nyingine mbele.
Mjasiriamali mwenye mawazo
hayo ndiye huanza
na mtaji wa
elfu kumi baada
ya mwaka zikazaa
milioni tano na baada
ya miaka akamiliki
milioni mia. Huyu huitwa
mjasiriamali mwenye fikra
chanya( positive thinking enterprenuer) . Nimesema hapo
juu kuwa hali
ya biashara imebadilika
kwa namna ambayo
wadau wa biashara
wamejielekeza katika kufanya
kazi na makampuni
badala ya watu
binafsi kama tulivyozoea.
Swali
la nini mjasiriamali
afanye katika hali
hiyo jibu lake
ni kuwa mjasiriamali
naye abadilike. Kama mwaka
jana ulifuga kuku wewe kama
wewe binafsi basi leo
fuga kuku chini ya
kampuni, kama mwaka
jana ulilima mihogo
Chanika na kuuza sokoni
wewe kama wewe basi
leo lima mihogo
na uza lakini
si kama wewe binafsi isipokuwa
chini ya kampuni. Una tigo pesa
yako, duka, liwe la
mavazi au bidhaa
nyingine, fundi fenicha,
unamiliki taxi, fundi cherehani, na
kila kitu unachofanya
kwa ajili ya kipato
basi sasa ni
wakati kumiliki kitu hicho kupitia
kampuni.
Hii ni
moja ya njia
kati ya njia
za mafanikio zilizo baki.
Biashara hufananishwa na
hali ya hewa. Leo
jua kesho mvua. Keshokutwa joto , mtondogoo baridi.
Biashara nayo hivyohivyo.
Kama mjasiriamli lazima
ukubali kubadilika haraka
na mara moja mara
tu yanapoingia mabadiliko . Lazima mjasiriamali
ajitambue na ajue
kuwa alivyofanya biashara
mwaka jana sivyo
atakavyofanya mwaka huu.
2. KWA
LAKI NA NUSU
WAWEZA KUMILIKI KAMPUNI.
Mara nyingi tunapozungumzia suala
la kampuni watu wengi huogopa
na kudhani kampuni ni kitu kikuuuubwa
kuliko hata vikubwa
vyote. Jamani, jambo hili
si kweli. Kampuni
ni kitu cha kawaida
kabisa ni mfumo
tu wa kufanya
biashara kutoka mtu
binafsi kwenda ushirika. Nimekuwa
nikisisitiza hili mara
kwa mara ili kuondoa
hofu na dhana hiyo ambayo
imeshajengeka kwa kuamini
kuwa kampuni ni
kitu kikubwa sana na cha
matajiri hivyo mtu
wa kawaida mjasiriamali
muuza mayai, muuza mihogo,
fundi fenicha, mmiliki duka
la vipodozi na vyakula
mtaani, mtoa huduma ya pesa kwa njia ya
simu, mkulima wa
kawaida kabisa kijijini
kuwa hawezi kumiliki. Nimekuwa
nikilisisitiza hili kwakuwa linawatia
wajasiriamali uoga na
matokeo yake linadumaza
kuendelea kwao.
Wengi hudhani ili
mtu amiliki kampuni
ni lazima awe na biashara
kubwa kama tunavyomuona
Bakhresa, Muhammed enterprises, IPP , migodi
ya madini , biashara ya
kuuza magari na
biashara nyingine kubwa
kubwa kama hizo. Mawazo
hayo si ya
kweli na leo
nakueleza mjasiriamali mwenye
kiu ya maendeleo
kuwa kwa shilingi laki
na nusu za
kitanzania unaweza kumiliki
kampuni na ukafanya
biashara kisheria kabisa.
Ni hivi, pale
wakala wa usajili wa
makampuni( BRELA) aina za
makampuni zimegawanyika kimitaji
katika namna tatu. Kuna
kampuni za mtaji
wa milioni 5- 10, mtaji wa m 10-30
na mtaji wa m 30- bila
ukomo. Kampuni
ninayoongelea hapa ni
hii ya mtaji
wa milioni 5-10. Usajili
mpaka unamiliki kampuni
ya namna hii hauhitaji
kuwa na zaidi
ya shilingi laki na
hamsini mpaka na sitini tu. Ada
kamili ya usajili “ registration fee” ni Tshs
100,000/= ( laki moja tu) , unaongeza Tshs
56,000/=( elfu hamsini na
sita tu ) kwa ajili ya ada
ya kufungulia jalada “filling
fee”, tena unaongeza
Tshs 10,000/=( Elfu kumi
tu) kwa ajili ya “stamp duty”. Ukipiga hesabu
jumla utaona ni
pesa isiyozidi laki
moja na elfu sitini
na sita tu. Kwa pesa
hii kampuni inasajiliwa
na unapata cheti
cha kuzaliwa kwa kampuni
na
unaweka biashara chini
ya kampuni.
Aidha suala la
mtaji wa m 5-10 huwa katika
maandishi tu si
lazima kuwa na
pesa hiyo mkononi
hivyo usiogope.Ili upate
kampuni pesa unayotakiwa
kuwa nayo mkononi
ni hiyo laki na
sitini na sita
niliyoitaja na wala
si hiyo milioni 5 au
10. Zaidi tujue kuwa kufanya biashara
chini ya kampuni kuna
faida nyingi sana mojawapo
ni
wepesi wa kupata
tenda na kupata ushiriki
katika makampuni mengine
makubwa . Faida nyingine
nyingi za kitaalam niliwahi kuzieleza
katika makala zilizopita. Mjasiriamali badilika
sasa miliki kampuni.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
VITU MUHIMU WAKATI WA KUSAJILI GAZETI NININI MSAADA
Sawa kabisa
Na ikiwa umekadiriwa na TRA 300,000 na ww mtaji wako una milioni moja je! Ukishindwa kulipa unachukuliwa Hatua?? Naomba msaada