NA BASHIR YAKUB-
Makampuni ya simu
kama Vaodacon, Airtel, Tigo,
Zantel, Sasatel, na mengineyo yamekuwa
yakitenda makosa mbalimbali
kwa wateja wao. Mara
kwa mara wateja
wa simu wamekuwa
wakilalamikia matendo ya
makampuni haya lakini
wengi wao wamekuwa
hawachukui hatua zaidi
ya kulalamika. Ni watu
wachache mno ambao
wamekwishachukua hatua za
kisheria dhidi ya
makampuni haya licha ya
uonevu mkubwa wa kihuduma
wanaousababisha.
Ukiangalia kwa
haraka utaona kuwa walio
wengi hushindwa kuchukua
hatua kwanza kwa
kutojua kama kuna
uwezekano wa kuchukua
hatua , pili kutokujua kama
kilichotendeka ni kosa na kinahitaji
adhabu au wakati
mwingine kwa kuamua
kuacha tu.
1.MNIGERIA ALIPWA
USD 90,000 KWA KOSA LA KAMPUNI
YA SIMU.
Nchi kama marekani,
uingereza na karibia
nchi nyingine za
ulaya zote, na
Afrika zaidi Nigeria
na Afrika kusini
makampuni ya simu yamekuwa
yakilazimika kulipa fidia nyingi
mara kwa
mara kwa wateja
wao kutokana na
makosa mbalimbali ambayo makampuni
yamesababisha kwa wateja.
Hivi karibuni nchini
Nigeria kampuni moja
ya simu imelazimika
kumlipa fidia ya USD
90,000 mtu mmoja
ajulikanaye kwa jina
la Edo Emeka baada
kuishtaki kampuni hiyo
kwa kumfungia kadi/namba(line) yake
pasi na sababu
za msingi.
Katika kesi
hiyo mlalamikaji Emeka
aliieleza mahakama kuu mjini
Lagos usumbufu alioupata
kwa kitendo hicho
cha kufungiwa namba
yake kitendo kilichopelekea mahakama
iamuru alipwe tuzo(decree) hiyo.
Aidha zipo kesi
nyingi katika nchi
mbalimbali ambapo watu
wamelipwa mamilioni ya
pesa kutokana na
makosa yanayosababishwa na
makampuni haya. Hapa kwetu
makampuni haya hutengeneza faida
tu na sisi hatuyawajibishi kwa namna
yoyote kwa makosa
na usumbufu tunayosababishiwa
kila siku.
2. KWA
MAKOSA HAYA WAWEZA KUISHTAKI KAMPUNI
YA SIMU .
Hapa kwetu sawa
na nchi nyingine
duniani makosa
ya makampuni ya simu
kwa wateja wao hufanana.
Kuna kufunga namba ya mtu
bila sababu za
msingi, kukata salio
la mtu bila
sababu za msingi, kumwekea mtu
mwito wa simu ambao
yeye mwenyewe hajachagua , kutumia mziki
wa msanii katika
program yoyote bila
ridhaa yake , kutokuwa hewani
au kukata mawasiliano
bila taarifa kwa
wateja, majenereta ya
minara kusabababisha usumbufu
na kelele kwenye
makazi ya watu, kwa kutaja
ni machache.
3. NAMNA
YA KUYASHITAKI MAKAMPUNI
YA SIMU.
Watu wengi hata nchi
za nje walioyashitaki makampuni
ya simu wameshitaki katika
kesi za madai.
Kesi za madai
ni kesi ambazo
hukumu yake kama
mlalamikaji atashinda basi
hutakiwa kulipwa kiasi fulani cha
hela. Malipo hayo yaweza
kuwa ya fidia,
usumbufu, gharama, kutegemea
na mtu mwenyewe
alichoomba kulipwa. Kosa
kwa mfano kosa
la kufungiwa namba . Imekuwepo tabia
ya makampuni haya
kufunga namba ya
mtu kwa kisingizio
cha kuwa eti
amekuwa hatumii kadi/laini
hiyo kwa muda.
Wapo watu
ambao huacha kutumia
laini zao kwasababu
za kuwa nje
ya nchi na
wengine huacha kutumia
kwa ugonjwa wa
muda mrefu na wengine huwa
na kadi nyingi na
hivyo hutumia kila
moja kwa awamu. Hili
linapaswa kuwa kosa
iwapo sharti hilo
lipo katika ile karatasi unayopewa
wakati wa usajili wa kadi.
Ni vema kujua
kuwa karatasi unayopewa
wakati wa usajili
ndio mkataba wa
makubaliano kati yako
na kampuni ya
simu. Ukiangalia karatasi
za makampuni yote
yaliyoko nchini hakuna
karatasi hata moja
yenye maelezo ya
kufungiwa kadi iwapo
itakuwa haitumiki kwa
muda fulani. Hivyo ni kusema
kuwa kitendo chochote
cha kufunga kadi
ni kufanya kosa
na kusababisha usumbufu
ambao unahitaji kufidiwa.
Pia kumwekea
mteja mlio ambao
mpigaji akimpigia anausikia
wakati mteja hakuuomba
ni kosa ambalo wakati mwingine humvunjia heshima
mteja. Kwa kampuni za
simu za hapa
kwetu ni rahisi
kumpigia simu Sheikh
mkuu ukasikia mwito wa
nyimbo ya kwaya
au ukampigia Kardinali
Pengo ukasikia kaswida au aya za Qurani
kama mwito wake.
Pia nyimbo za
wasanii kutumika kibishara
bila wao kutoa
ridhaa ni kosa
linalohitaji fidia. Kutokana
na haya fungua
kesi mahakama kuu kwa
mfano itaandikwa BASHIRI
vs
AIRTEL TANZANIA LTD huku
ukiainisha kosa ulilotendewa,
madhara uliyopata na
kiasi cha fidia
unayotaka. Kesi hizi hufunguliwa
mahakama za wilaya
na mahakama kuu
kulingana na kiwango
cha hela unachodai.
Wakili mmoja ajulikanaye
kama ISHENGOMA tayari
ameishtaki AIRTEL akidai
kulipwa milioni 400 kwa kumfungia
kadi alipokuwa nje
ya nchi kimasomo. Na
wewe pia waweza
kufanya hivyo ili
kukomesha usumbufu unaosababishwa na makampuni haya.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment