Tuesday 5 May 2015

MJASIRIAMALI UNAHITAJI KAMPUNI, FAHAMU KITU KIITWACHO “ MIKATABA KABLA YA KAMPUNI”.



Image result for WAJASIRIAMALI

NA  BASHIR  YAKUB-

Ni  jambo  la  kutia faraja  kuwa   vijana wengi  wamekuwa  wajasiriamali   na wanafanya  biashara  mbambali   katika    maeneo mbalimbali  ya  nchi. Wengine  biashara  ni  nzuri  na  wengine  wanalalamika  biashara  sio  nzuri. Kila  mtu  ana  muono wake   kuhusu  mwenendo  wa  biashara  zake.  Pamoja  na  hayo  ushahidi  wa  sayansi  ya  biashara  unathibitisha  kuwa  kwa  asilimia  zaidi  ya  70  suala  la biashara  kuwa  mbaya   au  nzuri  hutokana  na  mtu  mwenyewe alivyojipanga. Mbinu, umakini, mtaji, uendeshaji, mipango,  na  weledi.  

Nilipoandika  kuhusu  njia au namna  ya kuunda  kampuni  nilieleza  kuwa  masuala  ya  uendeshaji  wa  kampuni   huwa  ni  masuala  ya  kisheria. Kila  kitu  katika  kampuni  ni sheria  kuanzia  usajili, uendeshaji    mpaka  kufa  kwa  kampuni .
 Ni  kwa  maana  hii  nasema  kuwa  mjasiriamali   anapopata ushauri   mzuri  wa  masuala  mbalimbali  ya  sheria  katika  uendeshaji  wa  kampuni  basi  yaweza kuwa  nafasi  ya  ustawi wa  kampuni.  Leo  nazungumzia kitu  kingine  cha  kisheria  katika  uendeshaji  kampuni kiitwacho  mikataba  kabla  ya  kampuni ( pre  incorporation contracts). Tutaona  hapa chini  maana  na  umuhimu  wa  kujua  kitu  hiki.

1.NINI  MAANA  YA  MIKATABA  KABLA  YA  KAMPUNI ( PRE  INCORPORATION  CONTRACTS ).

Mikataba  kabla  ya  kampuni   ni  kama  jina  lenyewe  linavyojieleza.  Hii  hujumuisha  biashara  alizokuwa  anafanya  mtu  kabla  ya  kuwa  na   kampuni lakini baadae  akawa  na  kampuni   na  akaendeleza  biashara  zilezile. Watu  wengi  ambao  tayari  wameanzisha  makampuni   hujikuta  walikuwa  na  biashara  zao   hata  kabla  ya  kuunda  makampuni hayo.  Pengine  kutokana  na  biashara  kupanuka  mtu  anaamua  kuunda  kampuni   ili  kuendeleza biashara  ileile.  Kwa ufupi  maana  ya  hili  ni   kuwa,  ni  ile   biashara   aliyokuwa  nayo  mtu    na  kuamua  kuiundia  kampuni .

Mtego ( technique)   wa  kisheria  uliopo  hapa ni  kuwa  umekuwa  na  biashara  ambayo  haikuwa  kampuni ,  ina  maana  katika  biashara  hiyo  umefanya  mikataba  mbalimbali  kwa  mfano  umefanya  mkataba  wa  pango au   mkataba  wa  manunuzi ya  eneo  la  biashara, umekuwa  ukinunua  bidhaa  mbalimbali   kwa  kuandikishana  au  kupewa  risiti( risiti nayo ni  mkataba),mikopo  mbalimbali,  ulinunua mali  mbalimbali  kwa  ajili  ya biashara  zako  kwa  mfano  gari, pikipiki, baiskeli  au  maguta  kwa  ajili  ya  kubebea  mizigo n.k  Hii  yote  ni  mikataba  uliyoifanya  kabla  ya  kuunda kampuni  na  ndio  huitwa “pre incorporation  contract”. Swali  ni  je  utakapounda  kampuni  na  biashara  hiyo  yote  na  mali  zake kuziweka  chini  ya  kampuni , mikataba  hiyo  itakuwa  inaibana  kampuni  na  je kampuni  inawajibika  kwa  lolote  litakalotokana  na  mikataba  ambayo  imeingiwa  kabla  ya  kuundwa/kuzaliwa kwake ?.           

2. JE , KAMPUNI  INAWAJIBIKA   KATIKA  MIKATABA  AMBAYO  IMEFANYWA  KABLA  HAIJAUNDWA.

Mikataba  inayofanywa  na  mtu  kabla  ya  kuunda  kampuni  kwa  mfano  mikopo, na  miamala  mbalimbali  ya  manunuzi  hasa  zile  ambazo  zinahusisha  madeni ambazo  zimeingiwa  kabla  ya  kuundwa  kwake na kuwekwa  chini  yake   baada  ya kuundwa   kisheria  kampuni hiyo  haiwajibiki  na  mikataba   hiyo.  Mtu  binafsi  aliyefanya  miamala  hiyo  ndiye anayewajibika   nayo  na  si  kampuni.  Kwa  hiyo  ni  vema  wajasiriamali  wanaonzisha  biashara  nje  ya  kampuni  na baadae  biashara  ile  kuiingiza ndani  ya   kampuni  kujihadhari  sana  na  hili.

3.  KUUZWA  MALI  ZAKO  BINAFSI  BADALA  YA   ZILE   ZA  KAMPUNI.

Kisheria  kampuni  inaposhindwa  kulipa  madeni  mali  zake  ndizo  hukamatwa  na  kuuzwa  ili  kufidia  madeni.  Kamwe  mali  za   mtu  binafsi/mmiliki  wa  kampuni   haziwezi  kukamatwa  kufidia deni  la  kampuni.  Lakini  ikiwa   madeni  ya  kampuni  yaliingiwa  na  mtu  kabla  ya  kampuni  kuundwa  na  baadae  mtu  huyo  akaunda  kampuni  na  kuiweka  biashara  yake  yote  na  madeni chini  ya  kampuni  basi   madeni  hayo  hayahesabiki  kama  ni ya  kampuni   na   hivyo katika  kuuza  kulipa  madeni ni  mali  za  mtu  binafsi  zitakazomatwa  na  kuuzwa.  

Haya  ni  mambo  ya  kiufundi  kidogo  lakini   ni  muhimu sana  kwa wajasiriamali  kuyajua  kwakuwa  nimeyaandika  baada  ya  kuyakuta  mahakamani   kwa  wingi  ambapo  makampuni  madogo madogo  ya  wajasiriamali  mbalimbali   yameshitakiwa  mengine  kushitaki,  wengine  mali  zao  imeshatolewa amri  ya  kuuzwa,  mengine  kufilisiwa,  ni  vilio  vitupu.  Nisisitize  kuwa  ushauri  wa  kisheria  katika  kila hatua  ya  kampuni  ni  muhimu  kwa   ustawi  wa  kampuni  ili  kuepuka  kutumia  muda  mwingi  kushughulikia  migogoro  badala  ya  kushughulika  na  mambo  ya  msingi  ya kuendeleza  kampuni  kwa  maendeleo  yako. Jihadhari
MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

                                           TANGAZO   MUHIMU                                                
VIWANJA     NA     NYUMBA          ZINAUZWA.
·        
WANASHERIA   WETU   WATAKUANDALIA   MIKATABA  YOTE  BURE  NA    KUKUSIMAMIA  MPAKA   MANUNUZI    YAKAMILIKE   BURE.
·        
UHALALI   WA  NYARAKA   NA   UMILIKI   UMETHIBITISHWA  NA                        WANASHERIA  WETU.
·        
UTAPEWA  MTU  WA  KUKUSAIDIA  KUFANYA  TRANSFER   KWA  HARAKA         BURE.
·        
IKIWA   UTATOKEA   MGOGORO  NDANI   YA  MWAKA  TANGU  TAREHE  YA       MANUNUZI    UTAPEWA   WAKILI   WA   KUSIMAMIA  MGOGORO    BURE
                                                        0784482959.

 KUONA   BOFYA  HAPO  JUU    MWANZO  WA   BLOG.





0 comments:

Post a Comment