NA BASHIR YAKUB-
Kifungu cha 18 cha
Sheria ya Kanuni
za adhabu sura
ya 16 kimeeleza
hatua ya mtu
kujikinga mwenyewe, kumkinga
mwenzake , mali
yake mwenyewe na mali ya
mwenzake. Kujikinga( defence)
maana yake ni
kujilinda au kujitetea
inapokwa imekutokea dharula
ya kuvamiwa na
mtu au watu
waovu. Uovu ni uovu
si lazima awe
mwizi . Hata mtu
asiyekuwa mwizi lakini
amekuvamia kwa nia
ovu iwe nyumbani, kazini au
sehemu nyingine yoyote
basi ni adui
unayepaswa kujikinga naye.
1.KUJIKINGA NI
HAKI YA KILA
MTU.
Haki ya kujikinga
na adui si
tu imeelezwa katika
kifungu nilichotaja bali
pia ni haki
ya msingi ya
kikatiba. Haki hii pia
huingia katika zile
haki ambazo huitwa
haki za kuzaliwa ( in born right). Haki
za kuzaliwa ni zile haki
ambazo sio lazima
ziwe zimeandikwa katika sheria
fulani halafu ndipo mtu azitekeleze .
Ni haki ambazo
hata kama hazikuandikwa
popote mtu ni
lazima azipate tu. Kwa
mfano haki ya
kula au ya
kuishi.
Haihitaji iwe imeandikwa
popote katika katiba
au penginepo ili
uweze kula au kuishi.
Ni kitu ambacho
hutokea moja kwa moja(
automatic). Ni kitu ambacho
huandikwa kama haki
katika sheria lakini
hata kisingeandikwa ilikuwa
ni lazima kiwepo. Halikadhalika ndivyo
ilivyo katika haki ya kujikinga ( defence) kwani haihitaji kuwa imeandikwa popote kuwa
mtu akikuvamia kukudhuru
ujikinge naye. Inakuja
tu moja kwa
moja mtu akitaka
kukudhuru ni lazima
ujilinde kwa kutafuta
namna ya kujiepusha
naye.
2. INARUHUSIWA KUJIKINGA
HADI KUUA.
Kifungu cha 18c cha
sheria hiyohiyo ya
kanuni za adhabu kinasema
kuwa mtu anaweza
kujikinga mwenyewe, mali yake ,
kumkinga mtu mwingine, mali ya mtu
mwingine dhidi ya
hatari au shambulio
mpaka kufikia hatua
ya kuua au
kusababaisha madhara makubwa
ya kimwili. Madhara makubwa
ya kimwili ni
pamoja na kukata
kiungo cha mtu
mfano mguu, mkono,
au kusababnisha madhara
mengine kama kusababisha
kidonda kikubwa na
hali nyingine zote
zinazofanana na
hizo.
3. ANAYEUA AU
KUSABABISHA MADHARA MAKUBWA
KWA MTU MWINGINE
KATIKA KUJIKINGA HANA
KOSA KISHERIA.
Mtu yeyote anapokuwa
katika harakati za
kujikinga au kumkinga mtu
mwingine na adui halafu akaua
au akasababisha kifo kisheria
anakuwa hana kosa na
hapaswi kushitakiwa na
hata akishitakiwa basi
utetezi wake
( defence)
itakuwa ni kusema kuwa
alikuwa katika harakati
za kujikinga, kumkinga mtu
au mali.
4. BAADHI YA
MAKOSA AMBAYO UKITENDEWA
WAWEZA KUUA KATIKA
KUJIKINGA.
Kifungu hicho cha
18C ( a – e) kimetaja baadhi ya
makosa ambayo ukitaka
kutendewa, au mtu mwingine kutendewa
basi yafaa kujilinga
hadi kuua au kusababisha kifo. Baadhi
ya makosa hayo
ni kubaka, kulawiti,
Kunajisi, jaribio la
kuua, shambulio lolote linalolenga
kusababisha madhara makubwa
ya kimwili, utekaji
nyara, wizi wa silaha, kuchoma moto, na
makosa mengine yote
ambayo yanalenga kusababisha
uharibifu mkubwa katika
mali.
5. MAANA HALISI
YA KUJIKINGA HADI
KUUA.
Kujikinga hadi kuua
mfano wake ni
huu, mtu amekuvamia nyumbani
mchana au usiku
na lengo lake
ni kukuua kwakuwa
tayari ameshikilia upanga.
Katika mazingira kama hayo basi na wewe
waweza kuchukua upanga
au namna nyingine
yoyote kumuwahi kabla
hajakukata wewe. Au
mkabaji amekukaba usiku
au mchana lengo
ikiwa akuibie na
amekukaba kiasi usipofanya
jitihada anaweza kukusababishia kifo. Katika
mazingira kama hayo
kama utapata nafasi
ni ruhusa kupiga
popote au kutumia
chochote kumuua ili
upate kupona wewe.
Katika mazingira yote
hayo niliyoeleza huna
shitaka la kujibu
mbele ya sheria.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA
MSHAURI WA SHERIA
KUPITIA GAZETI LA
SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE
, GAZETI JAMHURI KILA
JUMANNE NA GAZETI
NIPASHE KILA JUMATANO.
0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment