NA BASHIR YAKUB-
Suala la matunzo
haliishi tu kwa mtoto/ watoto. Wengi
wa wanaume wamekuwa wakipendelea
kuwajibika kwa kutoa
matunzo ya watoto
na kumuacha mwanamke.
Jambo hili si
sawa na halikubaliki
kisheria. Ni vema kufahamu
kuwa suala la matunzo
kwa mwanamke limegawanyika mara
nne. Kwanza kuna
matunzo kipindi ambacho
ni cha ndoa
ambapo hakuna mgogoro
wowote baina ya
wanandoa. Pili kuna matunzo
kwa mwanamke kipindi
ambacho wanandoa wanakuwa
wametengana lakini hawajatalikiana. Tatu
kuna matunzo kwa
mwanamke kipindi ambacho
kuna mgogoro wa
familia mahakamani, na nne
matunzo kwa mwanamke
kipindi ambacho talaka
imekwishatolewa.
1.MATUNZO YA
MWANAMKE WAKATI WA
NDOA.
Hiki ni kipindi
ambacho ndoa huwa
inaendelea vyema bila
kuwapo kwa mgogoro
wa aina yoyote
ambao unaweza kutishia
uwepo wa ndoa hiyo. Katika
kipindi hiki mwanaume ana
wajibu wa kisheria
kutoa matunzo kwa
mke wake. Hii ni
kwa ndoa zote
yaani zile za
kimila, kiserikali, kidini ikiwemo
ile ya kuishi
wote kwa zaidi
ya miaka miwili ( presumed marriage). Mwanaume yeyote
ambaye anaishi na
mwanamke katika ndoa
mojawapo kati ya
hizi basi huyo
anawajibika kutoa matunzo
kwa mwenza
wake.
2.MATUNZO KWA
MWANAMKE KIPINDI AMBACHO
AMETENGANA NA MME WAKE.
Kisheria kuna tofauti
kubwa kati ya
kutengana na kutalikiana.
Kutengana ni kutengana
na inaweza kuwa
waliotengana wanaishi nyumba
moja lakini vyumba tofauti au vitanda tofauti. Lakini
pia inawezekana waliotengana
wakawa wanaishi nyumba
tofauti na sehemu
mbali kabisa. Huku kote
ni kutengana wala
sio kutalakiana au kuachana. Kwa
hiyo wanaume walio katika
kipindi cha kutengana
na wake zao
wanawajibika kutoa matunzo
kwa wanawake hao.
Hii ni kwa
mujibu wa sheria
wala si vinginevyo. Haki
ya mwanamke kutunzwa
inabaki palepale japo
hukai nae chumba
kimoja, hauli chakula
chake, haukai nae nyumba moja, na
wala hamshirikiana chochote.
Hii ina maana
kuwa kutoshirikiana naye
katika haki yoyote
ya ndoa hakuondoi wajibu
wa kisheria wa
kutoa matunzo kwa
mwanamke huyo. Katika
kipindi hiki cha
kutengana ni makosa kukataa
kumtolea matunzo mwanamke.
3.MATUNZO KWA
MWANAMKE KIPINDI AMBACHO
KUNA MGOGORO WA KIFAMILIA
MAHAKAMANI.
Baadhi ya wanaume
hukataa kuendelea kutoa
matunzo kwa mke hasa
pale ambapo mwanamke
amekimbilia mahakamani kutafuta haki
zake za kifamilia.
Lazima ieleweke kuwa
katika kipindi ambacho
mwanamke amefungua kesi
bado anakuwa yupo
katika ndoa na
hivyo anastahili haki
ya matunzo kama
mwanamke. Kufungua kesi
hakuondoi haki ya
matunzo hata kama
hiyo kesi aliyefunguliwa ni
mwanaume. Mwanaume anatakiwa
kuendelea kutoa matunzo
ya mwanamke huyo
mpaka mahakama itakaposema
vinginevyo.
4.KUTOA MATUNZO
KWA MWANAMKE AMBAYE
AMEPEWA TALAKA.
Matunzo ya aina
hii sio haki ya moja
kwa moja( automatic right).
Ni haki
ambayo hutolewa na
mahakama baada ya
kuzingatia mambo ya
msingi baada ya talaka. Kimsingi
talaka inapotolewa haki
zote za ndoa
hufa ikiwemo ya
matunzo kwa mwanamke. Pamoja
na hayo mahakama
hata baada ya
talaka na haki ya
matunzo kufa inaweza
kuamuru haki hiyo ya
matunzo kwa mwanamke
kuendelea baada ya kuzingatia mambo
kadhaa ya msingi. Hata
hivyo haki hii
haiwezi kudumu kwa
muda mrefu hata
kama itakuwa imetolewa na mahakama. Mahakama hutoa
haki hii kwa
muda tu.
5 . MWANAMKE AFANYE NINI IWAPO
MWANAUME HAMTOLEI MATUNZO.
Moja, mwanamke aende ustawi wa
jamii ulio karibu
naye na pili
anaweza kufungua shauri mahakamani.
Pia fidia hutolewa
iwapo kuna muda
ambao mwanaume hakutoa
matunzo huko nyuma.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment