NA BASHIR YAKUB-
Kujua masuala mbalimbali kuhusu upangaji na haki
zake ni muhimu
sana hasa kwa
wakati huu ambapo muingiliano
wa watu kutoka
sehemu moja hadi
nyingine umeongezeka sana huku
makazi yakiendelea kuwa machache. Mbali ya
upangaji kwa ajili
ya makazi pia sekta ya biashara nayo imekua sana
kiasi cha kukuza
mahitaji ya pango kwa
ajili ya biashara. Ni kutokana
na hili pia kwa
muda wa hivi karibuni
tumeanza kushuhudia ongezeko
la migogoro kati ya
wapangaji na wenye
nyumba hasa katika
haya mapango ya
biashara. Ni hali hii
inayonifanya nione umuhimu
wa kueleza baadhi
ya mambo ya
msingi kuhusu upangaji.
Awali ya yote
ni vema kufahamu
kuwa suala la upangaji na upangishaji linaongozwa
na sheria ya ardhi.
Hii ni kwasababu
upangaji unahusu nyumba
na wakati mwingine
ardhi isiyo na
nyumba. Kwahiyo niseme tu
kuwa yeyote anayetaka kujua
haki za kupanga na
kupangisha basi na
asome sheria ya
ardhi .
1.UKIPOKEA HELA
YA MTU ULIYEMSAIDIA
MAKAZI ANAGEUKA KUWA
MPANGAJI WAKO.
Unapomweka mtu katika
ardhi yako kwasababu
yoyote ile iwe
anakulindia eneo lako au ndugu
tu umeamua kumsaidia
ni vema kujiepusha
na kupokea hela
yake yoyote ikiwa
hutaki awe na
hadhi ya upangaji.
Unapopokea hela za
mtu kama huyo
basi mtu huyo
kisheria sio kwamba
umemsaidia makazi tena isipokuwa
anageuka na kuwa
mpangaji wako na hivyo anastahili
haki zote za
kiupangaji. Ili
mtu asiwe mpangaji
katika ardhi yako
basi usipokee chochote kutoka
kwake hasa hela ambayo
hutolewa kwa mtindo wa
mwisho wa mwezi au
kila
wiki au vinginevyo.
Utakapo pokea hela kwa
mtindo huo basi hadhi
ya mtu huyo
itabadilika na kuwa
ya kiupangaji. Lakini ikiwa
hautaki awe na
hadhi hiyo basi
si vema kupokea hela
kutoka kwake kwa
mtindo huo. Hii
inahusu hata yule anayempa
mtu makazi huku
akimpa sharti la
kumlindia eneo au kulihudumia eneo
na kuifanya huduma hiyo
au ulinzi huo
kuwa kama malipo
yake ya kumpa makazi.
Kisheria kwa kulinda eneo ikiwa kama
huduma ya kulipia
makazi basi mtu
huyo anakuwa ni mpangaji
na anakuwa na haki
zote za kiupangaji
na hawezi kuondolewa
katika lile eneo
bila kuzingatia haki
zake kama mpangaji.
2. SIKU
ZILIZOZIDISHWA BAADA YA KODI KUISHA INABIDI
KULIPIWA FIDIA.
Mpangaji anayezidisha siku
baada ya zile
siku za mkataba
kuisha basi zile alizozidisha
inabidi azilipie fidia
kisheria. Kama mkataba
wake ulikuwa unaisha
tarehe 10/10/ na
yeye akaondoka tarehe
10/12/ basi kisheria
ibabidi alipe fidia ya miezi
miwili aliyozidisha. Na
ulipaji wa fidia
ya namna hii
huwa ni mara mbili
katika muda aliozidisha. Yaani kama
kwa mwezi alikuwa
akilipa laki moja na
sasa amezidisha miezi
miwili basi kila
mwezi aliozidisha ataulipia mara mbili ambayo
ni laki mbili
kila mwezi na
hivyo atalipa laki nne
kwa kuzidisha miezi
miwili. Hivi ndivyo
fidia kwa aliyezidisha
muda wa pango
huhesabiwa.
3. UPANGAJI
WA UTASHI.
Kwa jina la
kitaalam upangaji wa
utashi huitwa “tenancy
at will”. Hii
ni aina ya
upangaji ambapo mpangaji
na mwenye nyumba hukubaliana kama
ilivyo kawaida lakini
kwa sharti kuwa
mwenye nyumba atasitisha upangaji
wa mpangaji wakati
wowote atakapoamua. Upangaji
wa kawaida tuliozoea
katika mkataba wa
pango mpangaji na
mwenye nyumba huwekeana
muda wa kumalizika
kwa mkataba wa pango na
mara nyingi huwa
ni baada ya miezi
sita au mwaka
mmoja na wengine huwa
ni zaidi ya
hapo. Muda wa
kuisha kwa upangaji
huwa ni kitu
muhimu sana katika
mikataba ya kawaida
ya upangaji.
Lakini hali ni tofauti
kabisa katika mikataba
ya upangaji wa
utashi ambapo muda huwa
hauwekwi bayana ikiwa
na maana yeyote
kati ya mpangaji
au mwenye ardhi
anaweza kumaliza upangaji muda
wowote. Nalieleza hili ili watu
wasije kuingia katika
mtego kwa kusainishwa
mikataba ya upangaji
bila kuweka bayana muda wa upangaji.
ifahamike kuwa unaposaini mkataba ambao hauweki
bayana muda wa
upangaji basi upangaji huo
unageuka na kuwa
upangaji wa utashi( tenancy at will) na
ikiwa wewe ni
mpangaji basi ,mwenye
nyumba ana haki ya kukuondoa
katika nyumba/duka muda
wowote.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA
MSHAURI WA SHERIA
KUPITIA GAZETI LA
SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE
, GAZETI JAMHURI KILA
JUMANNE NA GAZETI
NIPASHE KILA JUMATANO.
0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment