NA BASHIR YAKUB-
Kumekuwa na tabia
ya taasisi za
fedha kuuza nyumba
au viwanja vya watu
walivyoweka rehani na kushindwa
kulipa mkopo kwa
bei ya kutupa. Kwakuwa taasisi
za fedha huamini
kwamba wana deni na
mtu na ameshindwa kulipa
hela zao na pengine kwakuwa
tayari wamekamilisha taratibu
zote za kisheria
za kuuza basi
huamua kuuza mali
ya mtu kwa
bei ambayo ni
ndogo kiasi cha
kustaajabisha.
Ni kawaida
kukuta nyumba ya milioni
mia ikiuzwa hata
milioni kumi na tano
ili kulipia deni
la milioni kumi
na mbili au kumi na tano. Watu wanapaswa kuelewa kuwa hili
si sawa na
sheria imekataza jambo
hili. Thamani ya nyumba
au kiwanja iko
palepale hata kama
mtu ameshindwa kulipa
mkopo. Si kweli kuwa kwakuwa
sheria imeruhusu kuuza
mali ya mtu
anaposhindwa kulipa mkopo
basi imeruhusu kuuza
bei yoyote ile
ilimradi muuzaji amepata
kiasi anachodai. Hili
si kweli kama tutakavyoona
hapa chini.
1.WAJIBU WA
TAASISI YA FEDHA KATIKA KUUZA NYUMBA YA
DHAMANA. .
Kwa kujua hili
la kuuza mali
za watu bei
ya kutupa Sheria
ya ardhi kifungu
cha 133 ( 1 ) kikasema kuwa
muuzaji wa nyumba
iliyowekwa rehani ana
wajibu mkubwa na
wa hali ya
juu kuhakikisha anachukua
tahadhari na anakuwa
mwangalifu kwa kiwango
cha juu kuhakikisha
wakati anapouza ardhi ya mtu
anaiuza kwa bei nzuri
na bei ambayo
inakubalika kuwa bei
inayostahili kwa wakati husika. Huu
ni wajibu wa
kisheria alionao muuzaji
au mnadishaji wa
ardhi ya dhamana. Kifungu
hicho kinasema kuwa
suala la kuuza
mali ya dhamana
kwa bei inayokubalika
ni haki ambayo
aliyeshindwa kulipa deni
anamdai muuzaji/mnadishaji. Kwa
hiyo wewe unayedaiwa unamdai
huyo mnadishaji anayetaka
kuuza nyumba yako
haki ya kuuza hiyo
nyumba katika bei
inayokubalika ( reasonable price).
2. NYUMBA/KIWANJA KIUZWE
BEI GANI KWA
MUJIBU WA SHERIA ?
Sheria ya ardhi
haikutaja moja kwa
moja ni kiasi
gani nyumba ya mtu
au kiwanja kinatakiwa kuuzwa. Hii ni
kutokana na utofauti
wa thamani wa mali
hizo
na hivyo isingekuwa
rahisi kusema kuwa
bei ya mwisho
ya nyumba au
kiwanja ni kiasi fulani.
Ili
kuliweka sawa hili kifungu
hichohicho cha 133( 2 ) kikasema kuwa
nyumba/kiwanja cha mtu
hakitakiwi kuuzwa 25% ya bei
ya soko ya
nyumba au kiwanja
hicho kwa wakati
huo au chini
yake.
Hii ina maana
kuwa ikiwa eneo
lako litauzwa kwa
njia ya mnada
baada ya kushindwa
kulipa deni halafu
likauzwa asilimia 25 au chini
yake kulinganisha na
bei ya soko
ya eneo hilo
kwa wakati huo
basi wauzaji na
mdai deni aliyewatuma
wote kwa pamoja
watakuwa wametenda kosa
la kisheria. Kwa
umuhimu mkubwa narudia
kusisitiza kuwa nyumba/kiwanja hakitakiwi
kuuzwa asilimia 25 ya bei ya
soko ya
wakati huo au
chini ya asilimia
25 ya bei
ya soko ya
eneo ya wakati
huo, hii ni kwa
mujibu wa sheria.
3.NINI UFANYE
IWAPO NYUMBA/KIWANJA CHAKO KIMEUZWA 25% AU
CHINI YAKE.
Kifungu hichohicho cha
133( 2 ) kinatoa mwarobaini
wa kuponesha kidonda cha
ardhi yako kuuzwa
25% au
chini yake . Kinasema kuwa
ikiwa ardhi ya
mdaiwa deni imeuzwa kwa
bei ya 25%
ya bei ya
soko au chini
yake basi mdaiwa
huyo anaruhusiwa kuiomba
mahakama kubatilisha mauzo
hayo. Hii ni
kwasababu mdai amekiuka
wajibu wake wa
kisheria na hivyo
kuyafanya mauzo hayo kuwa
haramu.
Nahimiza kwa
kusema kuwa watu ambao
wamefanyiwa kitendo kama
hiki wachukue hatua
stahiki haraka za
kuiomba mahakama kubatilisha
mauzo ya mali
zao ikiwa ziliuzwa
kinyume na nilivyoeleza
hapa. Usiseme au
ukadhani umechelewa kwani
hili linawezekana hata
kama imepita miaka
kumi tangu nyumba/kiwanja chako
kiuzwe kwa kuwa sheria ya
ardhi imetoa mpaka
zaidi ya miaka
kumi kwa aliye
na lalamiko kulipeleka mahakamani. Hivyo
chukua hatua sasa
wala usiseme umechelewa
katika hili.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
Mr yakubu hongera Sana kwa ushauri wako you are reall professional na MUNGU akakuongoze