NA BASHIR YAKUB-
Kuna malalamiko katika baadhi
ya maeneo na
zaidi malalamiko haya yamekuwa
yakielekezwa kwa mamlaka
za serikali za
mitaa. Nimewahi kuandika kuhusu
ukiukaji wa taratibu
mbalimbali ambao hufanywa
na serikali za
mitaa katika maeneo
au ardhi za
watu. Pia niliandika
kuhusu upotoshi wa mamlaka za
serikali za mitaa
katika kuwaandalia watu
mikataba ya mauzo
ya ardhi wakati wakijua
kuwa hawaruhusiwi kufanya
hivyo jambo ambalo
huwasababishia wananchi usumbufu
mkubwa wanapoamua kutafuta hati
au kubadili majina
kwakuwa mikataba hiyo
ya serikali za
mitaa huwa haikubaliki
kisheria na hivyo watu
hurudishwa kuibadili.
Leo tena nazungumzia
ubabe walionao serikali
za mitaa wa
kutwaa maeneo ya
watu na kuyapangia
shughuli mbalimbali za
mtaa huku yakiwa
ni maeneo ya
watu binafsi. Kugeuza maeneo
ya watu njia
bila fidia ni
moja ya uonevu mkubwa
ambao wamekuwa wakiupata
wananchi kutoka serikali
za mitaa. Kwa ufupi
tutaangazia jambo hilo likoje
kisheria.
1.SERIKALI ZA
MITAA HAWARUHUSIWI KUTANGAZA
ENEO FULANI KUWA
NI NJIA.
Serikali za mitaa
hawana mamlaka kisheria
kuchukua eneo la mtu kulitangaza
kuwa njia. Kinyume
na ilivyozoeleka ambapo
viongozi wa serikali
za mitaa hutembea maeneo
mbalimbali ya mtaa
na kuchukua maeneo
ya wananchi kwa
madai kuwa yanapaswa
kuwa njia. Sheria
ya ardhi inasema
kwamba serikali kuu au serikali
ya mtaa au chombo
chochote hakiruhusiwi kutenga
maeneo kuwa njia
isipokuwa lazima watume
maombi kwa kamishna
wa ardhi ambaye
ndiye atakuwa na
mamlaka ya kutangaza
eneo fulani kuwa ni
njia.
Sheria inaendelea kusema
kuwa maombi hayo yatakuwa
yamewekwa katika fomu
maalum na kujazwa
katika namna inayokubalika. Kwa
hiyo kumbe hali haiko
kama
tulivyozoea ambapo serikali
za mitaa huamua
kuchukua eneo la
mtu na kulifanya
njia bila ruhusa ya
kamishna wa ardhi.
Ieleweke kuwa utaratibu ndio huo
wa
kutuma maombi kwa
kamishna wa ardhi
na si kuamka
asubuhi na kulifanya
eneo la mtu
kuwa ni njia.
2. KUTOA TAARIFA
KWA MTU AMBAYE
ARDHI YAKE INATAKIWA
KUGEUZWA NJIA.
Sheria ya ardhi inasema
kuwa iwapo ardhi ya mtu
yeyote
imependekezwa kugeuzwa njia
basi ni lazima
mtu huyo apewe
taarifa rasmi ya
maandishi. Isiwe tu kiongozi
wa mtaa anakuita
ofisini na kukwambia
kuwa lile eneo
ni njia hapana
inatakiwa taarifa maalum
ambayo yule aliyepewa
pia atapata nafasi
ya kuijibu ikiwa ataona
ni vyema kufanya
hivyo.
3. HAKI
YA KUKATAA ARDHI
YAKO KUGEUZWA NJIA.
Haki hii ndiyo
inayofanya kuwepo kwa haki
ya taarifa rasmi kwa mtu ambaye
eneo lake linatakiwa
kugeuzwa njia. Lengo
la taarifa ni
kumfanya mtu apate
nafasi ya kukubali
ardhi yake kubadilishwa
matumizi au kukataa. Hivyo
ikiwa atapewa taarifa
naye akawa hayuko
tayari ardhi yake kugeuzwa njia
basi anayo ruhusa
ya kukataa kwa kupeleka pingamizi
kwa kamishna wa
ardhi.
4. HAKI
YA KULIPWA FIDIA
IWAPO ENEO LAKO
LITAGEUZWA NJIA.
Sheria ya ardhi
inasema kuwa iwapo eneo
la mtu litachukuliwa
au kutengwa kama
njia basi mtu
huyo atatakiwa kufidiwa
thamani ya ardhi ilyofanywa
njia. Pia atatakiwa
kulipwa fidia kwa
hasara yoyote iliyosababishwa na
hatua hiyo ya
kugeuza eneo lake kuwa njia.
Hasara
ni nyingi yaweza
kuwa mazao, biashara fulani iliyokuwa
ikifanyika eneo hilo na kila
kitu ambacho ni hasara
kilichosababishwa na hatua
hiyo. Izingatiwe kuwa fidia ya
ardhi na hasara
ni vitu viwili
tofauti na vyote
hutakiwa kulipwa kwa pamoja.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment