NA BASHIR YAKUB-
Wakopaji nao wana
haki zao. Yapo mambo ya msingi
ambayo wanapaswa kuyajua
ili yawalinde iwapo
mambo yamewaendea vibaya.
Ukweli ni kuwa
ni busara unapokopa
kulipa deni lakini iwapo sababu za
kibinadamu zimejitokeza ambazo
ziko nje ya uwezo
wa mkopaji na ambazo
kwa namna yoyote
hawezi kuzizuia basi
ni vema mkopaji
awe na njia ya
kujiokoa yeye pamoja
na mali yake.
Uwepo wa
sababu za kibinadamu
zinazoweza kumzuia mtu
kulipa deni ndizo
zilizopelekea kuwapo baadhi ya
mambo katika sheria ambayo humlinda
mkopaji pamoja na
mali yake ikiwa ameshindwa kulipa
mkopo au amechelewa
kwa mujibu wa
makubaliano. Si kweli kuamini
kuwa mtoa mkopo
ndiye mwenye ulinzi
wa sheria peke
yake, hapana hata mkopaji naye
anao ulinzi wa sheria ikiwa mambo
yatamwendea vibaya kama
tutakavyoona. Kwanza tuangalie
sababu za kibinadamu
ambazo zinaweza kumfanya
mkopaji ashindwe kulipa
deni kwa wakati.
1.SABABU ZINAZOWEZA
KUMFANYA MKOPAJI ASHINDWE
KULIPA DENI.
( A )
MATENDO YA MUNGU ( Acts
of God ).
Matendo ya mungu
hujumuisha magonjwa/ugonjwa ambao huweza
kumsababisha mtu ashindwe
kabisa kuendelea na
biashara kwa namna
yoyote ile. Mtu hawezi
kuwa amelazwa na
hajitambui au anajitambua lakini
ugonjwa wake ni mkubwa
( serious) halafu ukategemea
afanye biashara na
arejeshe deni kwa
wakati.
Ni jambo
ambalo haliingii akilini. Ugonjwa ni
matendo kati matendo
ambayo husababishwa na
mungu na yako juu ya uwezo
wa mwanadamu yeyote. Zaidi,
matendo ya mungu
hujumuisha vitu kama
mafuriko, matetemeko ya
ardhi, ukame, vimbunga,
na kila kitu
ambacho hakiwezi kusababishwa
na mwanadamu. Ni
vigumu mkopaji kurejesha
deni iwapo moja
ya matendo haya yameikumba
biashara yake.
( B ) AJALI ISIYOZUILIKA ( innevitable accident) .
Ajali ni ajali suala la msingi
ni kuwa ajali
isiwe imesabaabishwa kwa makusudi
na mkopaji ili
akwepe kurejesha deni.
Kwa mfano juzi
tumeshuhudia ajali ya basi
lililoangukiwa na lori
njia ya mbeya.
Mle ndani walikuwamo
watu wana biashara zao
ambazo zimetokana na
mkopo na nyingi
zimepotea kabisa. Katika mazingira
yanayotambulika kama hayo
hakuna namna ambavyo
unaweza kulazimisha kuuza
nyumba/kiwanja cha mtu
eti kwakuwa amechelewa
kulipa ilihali kilichomchelewesha kinajulikana.
Hiyo ni ajali
isiyozuilika na lazima
watoa mkopo waizingatie. Pia
tulishuhudia ajali za meli kule Zanzibar
ambazo lazima ndani
yake walikuwamo wafanybiashara wakiwa
na biashara za
fedha za mikopo. Itakuwa sio
sawa kuharakia kuuza
dhamana ya mfanyabiashara kama huyu
wakati sababu iliyomchelewesha kurejesha
ikiwa wazi.
Vita ndani ya
nchi pia huingia
katika ajali isiyozuilika
na ni sababu
ya msingi ya
kuzingatia iwapo mkopaji
ameshindwa kurejesha mkopo.
( C ) SABABU
ZA KIDOLA/KIUTAWALA. (Executive
Authority ).
Kwa mfano mkopaji
ameweka biashara yake
mahali fulani halafu
serikali ikaja na
sera ya kumuondoa
eneo lile kwa
lengo la kuweka
mradi fulani kwa ajili ya
taifa, au serikali
imebadili utaratibu wa
fedha ghafla kwa kuongeza viwango
vya riba tofauti
na vile alivyokopea
mkopaji au mabadiliko yoyote
ya kisera
ambayo moja kwa
moja yanaathiri kwa
kiwango kikubwa biashara
na mkopo wa
mkopaji. Sababu hii
itakuwa nje ya
uwezo wa mkopaji
na yafaa izingatiwe
kabla ya kuchukua
hatua yoyote ya
kuuza mali yake.
( D ) SABABU ZITOKANAZO
NA SHERIA/MAHAKAMA ( statutory/judicial acts).
Yawezekana mtu amechukua mkopo
lakini wakati akiendelea
na biashara amehukumiwa
kifungo au hajahukumiwa
lakini yupo rumande
na hana dhamana. Mtu
huyu ni vigumu
kurejesha mkopo. Au
mtu amefungua biashara
lakini kuna
matatizo ya kisheria yamejitokeza na mahakama imetoa
amri ya kumzuia
kuendelea na biashara
au amri ya
kulifungia eneo lake
la biashara. Pia mtu kama
huyu hututarajii arejeshe
mkopo kwa wakati
kwa sababu zilizo
nje ya uwezo
wake.
2.NAMNA YA
KUOKOA NYUMBA/KIWANJA KISIUZWE
KWA KUSHINDWA/KUCHELEWA KULIPA
MKOPO.
Ikiwa zipo sababu za
msingi za kushindwa/kuchelewa kulipa
mkopo kama nilizotaja
hapo juu basi
waweza kuzuia nyumba/kiwanja chako
kisiuzwe. Njia kubwa , nzuri
na ya uhakika
ni mahakama. Utaratibu wake
ni kuwa utafungua
kesi mbili yaani
ndogo na kubwa.
Katika kesi kubwa
utakuwa ukieleza kilichotokea
kwa ukamilifu mpaka
ukashindwa kulipa deni
na ndani ya
kesi ndogo utakuwa
ukiomba nyumba/kiwanja chako
kisiuzwe kwakuwa wewe si
msababishaji wa kilichotokea. Kesi
ndogo itafunguliwa chini
ya hati ya dharula( certificate
of urgency) ili
iweze kusikilizwa kwa
muda mfupi na
kutolewa maamuzi ili kuwahi
wauzaji kabla hawajauza. Maamuzi ya
kesi ndogo yaweza
kutolewa hata ndani
ya siku moja
kutegemea na udharula
wenyewe.
Zingatia kuwa ikiwa
thamani ya mkopo au
eneo linalotaka kuuzwa
inaanzia milioni arobaini na moja
kwenda
mbele kesi itafunguliwa
mahakama kuu na
ikiwa chini ya
hapo itafunguliwa baraza
la ardhi na
nyumba la wilaya. Pia
zingatia kesi ya
namna hii hufunguliwa
katika wilaya lilipo
hilo eneo linalotaka
kuuzwa. Kwa kufuata
utaratibu mzuri waweza kuokoa nyumba/kiwanja chako
kisiuzwe kwa kuwa
hiyo nayo ni
haki yako kama
mkopaji.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI
LEO KILA JUMANNE
, GAZETI JAMHURI KILA
JUMANNE NA GAZETI
NIPASHE KILA JUMATANO.
0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
0 comments:
Post a Comment