NA BASHIR YAKUB-
Sheria ya ardhi
ni pana na ina mambo
mengi. Kila nikipata
nafasi huwa najitahidi
kueleza japo machache ili
watu waweze kuelewa masuala
mbalimbali kuhusu ardhi.
Ardhi ni rasimali
nyeti mno na hivyo
ni tatizo kubwa kuishi
bila kujua mambo ya msingi
na ya kisheria kuhusu ardhi. Kutokujua ni
moja ya sababu inayopelekea umaskini
wakati utajiri upo
mikononi mwako na upande
mwingine husababisha migogoro ya
ardhi inayoongezeka kila
kukicha huku watu
wakizidi kupata hasara.
Nimewahi kuandika kuhusu
namna ya kisheria ya
kujua iwapo ardhi unayonunua ina
mgogoro au hapana,
nikaandika kuhusu vitu
gani viwe ndani
ya mkataba wako
wa manunuzi ya
ardhi ili usitapeliwe na mikataba
ya ardhi kwa
ujumla, nikaandika kuhusu namna
nyepesi ya kubadili/kupata hati/leseni
ya makazi unaponunua
ardhi na mengine
mengi kuhusu ardhi. Leo
naeleza kitu kingine
muhimu katika sheria ya
ardhi ambacho ni dhamana(mortgages)
ambazo unaweza
kutumia kupatia mkopo
iwapo unahitaji mkopo.
1.NINI MAANA
YA DHAMANA.
Kifungu cha pili
cha Sheria Ya Ardhi
kinasema kuwa dhamana ni
hali ya mtu, taasisi
au chombo chochote
kuwa na maslahi
katika ardhi inayomilikiwa
na mtu mwingine
au chombo kingine, maslahi ambayo yanatokana
na deni au mkopo.
Maana yake ni kuwa ardhi
ni yako lakini
kitendo cha mtu mwingine
au taasisi nyingine kuwa na
maslahi ndani yake
na maslahi ambayo yanatokana
na kuwapo kwa deni
au mkopo basi hiyo ndiyo
dhamana.
Ieleweke wazi kuwa
dhamana haihusishi umiliki na
wala haina uhusiano na
umiliki. Dhamana ni dhamana na
mmiliki anaendelea kuwa
mmiliki. Dhamana haiondoi
haki ya umiliki( right of occupancy).
2.VITU AMBAVYO
WAWEZA KUWEKA
DHAMANA NA KUPATA
MKOPO.
Watu wengi wamekariri
kwa kujua kuwa dhamana
katika masuala ya
ardhi ni lazima
iwe hati ya
nyumba, barua ya toleo( offer)
au leseni ya
makazi. Ni kweli
vitu hivi hutumika kama
dhamana lakini si hivi tu
ambavyo vyaweza kutumika
kama dhamana. Vipo
vitu vingine ambavyo vyaweza
kusimama kama dhamana
na mtu akapata
mkopo kama ambavyo tutaona
hapa.
( A ) MKATABA
WA PANGO.
Kisheria mkataba wa
pango ni nyaraka halali
ambayo mtu anaweza
kuitumia kuombea mkopo
katika taasisi ya
fedha. Mkataba wa
pango ni yale
makubaliano ya kawaida
kati mwenye nyumba
na mpangaji. Mkataba wa
pango ni nyaraka
muhimu sana japo
watu wengi huwa
hawaipi uzito zaidi
ya kuamini kuwa
inalinda uhusiano kati ya mwenye nyumba
na mpangaji. Ni vyema sasa kujua
kuwa mkataba wa
pango hauishii kulinda
mahusiano ya mwenye nyumba
na mpangaji tu isipokuwa
ni nyaraka ambayo ikitumika
vyema yaweza kuwa zana
ya kukuza uchumi wako.
Kwa mfano umelipa
milioni tatu kama
pango la miezi
kumi na mbili. Unaweza
kupeleka mkataba huo
kwenye taasisi ya
fedha ukapewa pesa ambayo
iko chini ya hiyo
milioni 3 kwa
mfano unaweza kupewa
milioni 2 au moja
na nusu ambazo
utatakiwa kuzirejesha ndani
ya miezi minne
labda. Ina maana ikiwa
muda huo utaisha
kabla ya kurejesha
basi muda wako wa pango
uliobaki utachukuliwa na
waliokukopesha ili wautumie
kurejesha deni lao
aidha kwa kumpangisha
mtu mwingine au
kulitumia eneo lile
katika namna ambayo wanaamini
itarudisha hela yao
wanayokudai.
Biashara hii ipo
na inaruhusiwa kisheria
na ni ushauri wangu kuwa watu wajaribu
kwenye taasisi za fedha
watajuzwa kuhusu Jambo hili.
( B )MKATABA WA MAUZIANO (
sale agreement).
Mkataba wa mauziano
nao ni halali
kutumika kukopea kisheria.
Mkataba huu huu
wa kawaida ndio
ninaoongelea hapa. Unaponunua kiwanja/nyumba ambayo
haina hati , leseni ya
makazi wala barua
ya toleo (ofa) isipokuwa
ilichonacho ni maandiko
tu ya kununulia
basi maandiko hayohayo
ndio yanaweza kutumika kukopea. Si
lazima uhangaike sana kupata
hati au leseni
ya makazi ili
uweze kutafuta mkopo. Wasilisha maandishi
yako hayohayo kwenye
taasisi ya fedha na utapewa
maelekezo ya kupata
mkopo.
( D ) KUWEKA
DHAMANA SEHEMU YA ENEO BADALA
YA ENEO ZIMA.
Watu wengi hukimbilia
kuweka nyumba nzima
au kiwanja chote
kama dhamana kwa ajili
ya mkopo hata
kama mkopo wenyewe ni mdogo. Sheria
iko wazi kuwa
yawezekana nyumba au kiwanja kikawa
na hati moja lakini
hiyo hailazimishi kuweka
eneo lote kama
dhamana. Watu lazima wayaelewe
haya . Nyumba yaweza kuwa
ya vyumba vitano
ukasema mi naweka
vitatu , viwili au kimoja. Kiwanja
kinaweza kuwa sqm
400 ukasema mimi
naweka sqm 200
au 100 ili
nipate kiasi fulani cha mkopo.
Hata kama nyumba/kiwanja kina
hati moja bado
haizuiwi kufanya hivyo isipokuwa kitakachofanyika ni
kuwa hayo maelezo
ya nini kinawekwa
na nini kinabaki yatabainishwa na
kufafanuliwa vizuri katika mkataba,
kwa mfano eneo zima
ni kiasi fulani hivyo linawekwa
eneo kadhaa dhamana na
linabaki eneo kadhaa
au vinawekwa dhamana
vyumba kadhaa kwa ajili
ya shilingi kadhaa
na vimebaki vyumba
kadhaa.
Hayo ni
mambo ambayo huingia
ndani ya makubaliano
kimaandishi. Mara nyingi usipendelee kuweka dhamana
eneo zima au usikubali
kuchukua fedha kidogo
halafu ukaweka eneo kubwa
ni hatari iwapo
biashara haitakwenda vizuri. Wengi
waliofanya hivi wameingia
hasara kubwa. Usikurupuke lazima
uwe na mbinu.
( E ) HATI MILIKI YA KIMILA (
customary right of occupancy).
Wapo watu mijini
lakini wana maeneo
huko vijijini au
mashamba ambayo yana
hati miliki za kimila.
Hati miliki za
kimila ni hati miliki
zinazopatkana kwa maeneo yaliyo
vijijini. Lakini pia
hata kama huna
hati hii lakini una
shamba au eneo kijijini basi
imefika wakati sasa
ukalitafutie eneo hilo
hati ya kimila
ambayo ni rahisi
sana kuipata ili uweze
kuitumia kupatia mkopo
ili ukuze uchumi
wako. Hati ya kimila inakubalika
kisheria na itakuwezesha
kupata mkopo. Ni
hayo kwa leo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
0 comments:
Post a Comment