NA BASHIR YAKUB-
Wako watu wengi wameathirika
kutokana na matendo
yanayotokana na uzembe,kutojali au makusudi
ya madaktari. Wapo waliopata vilema
vya muda kutokana na
uzembe huo, wapo
waliopata vilema vya
maisha na wapo
waliouliwa na madaktari hawa hawa. Ajabu ni
kuwa ukifanya tathmini
ya haraka utaona kuwa
watu wote waliopata madhila
kutoka kwa madaktari
huhusisha madaktari wa serikali
na katika hospitali
za serikali. Si rahisi
kukuta jambo la ajabu
la kitabibu limehusisha
hospitali binafsi. Swali
langu ni kuwa,
ewe
Mtanzania daktari
amekusababishia tatizo iwe
ugonjwa wa kudumu, ulemavu
wa muda au
wa kudumu, au hata kifo
cha ndugu au jamaa, umechukua
hatua gani baada
ya tukio hilo ?. Umekaa kimya ukiwa umeridhika
au umekaa kimya
kwakuwa hujui la
kufanya ?.
1.INARUHUSIWA KUMSHITAKI
DAKTARI KWA KUSABABISHA MADHARA
KWA
MGONJWA WAKATI WA
TIBA.
Wapo wanaodhani kuwa
madaktari hawashitakiwi kwa kutomhudumia
vyema mgonjwa. Hili si
kweli daktari ni
mtumishi sawa na
watumishi wengine na kosa
lolote la uzembe,
kutojali au makusudi
analofanya na kusababisha
madhara kwa mgonjwa
sheria inaruhusu kumchukulia
hatua daktari huyo. Sawa
na mtumishi mwingine
akitenda kosa kazini anaadhibiwa
ndivyo ilivyo kwa
madaktari pia. Kwa mujibu
wa sheria daktari
amepewa wajibu wa
hali ya juu
kuhakikisha anatumia taaluma
yake, weledi na
uadilifu katika kutoa
huduma ya tiba
na kuepuka kabisa
hatua au namna yoyote
inayoweza kuleta madhara
kwa mgonjwa.
Takwa hili
kwa daktari ni takwa la kisheria na
wala si hiyari. Kwa
hiyo watu waelewe
kuwa suala la
daktari kutoa matibabu
kwa umakini ni
lazima. Kitu kikiwa
lazima (mandatory) katika sheria
maana yake ni kuwa
kutofanyika kwake hutoa
haki ya mtendewa
kushitaki. Hivyo ndivyo
ilivyo kwa madaktari.
Kwa namna yoyote
anapokosa umakini katika
kutoa tiba basi
ni ruhusa kwa
mtendewa kushitaki.
2. MADHARA YALIYOSABABISHWA NA
MADAKTARI TANZANIA.
Miaka ya nyuma
wapo watu hospitali ya muhimbili
walifanyiwa upasuaji
huku kila mmoja
wao akifanyiwa sehemu
ambayo haihusiki. Ni kisa
maarufu kila mtu anakumbuka ambapo
mmoja alifanyiwa upasuaji
wa goti wakati
akiwa na tatizo
la kichwa na
mwingine akafanyiwa kichwa
akiwa anaumwa goti.
Mwaka
jana msanii mmoja
wa sanaa maigizo bongo
movie alifariki katika mazingira ya kutatanisha baada ya
kupigwa picha miale (xray)
na kusomewa kuwa
ana matatizo ya
utumbo na kuanza
kupatiwa matibabu ya
utumbo pale Mwananyamala.
Hali ilizidi kuwa
mbaya akarufaniwa muhimbili
ambapo madaktari bingwa
wakathibitisha kuwa aliyesoma
picha miale (xray) alikosea
tatizo la mgonjwa
halikuwa utumbo na
kuwa amepoteza muda
mwingi katika matibabu
yasiyohusika na hivyo
amechelewa jambo ambalo
lilipelekea kifo chake.
Matukio
ya mwananyamala nayo
ni mengi huo
ni mfano tu.
Kisa kingine cha hivi
karibuni ni kile kilichotokea
mkoa wa Tabora
urambo ambapo daktari
alimfanyia upasuaji wa
tumbo mwanamke na
kusahau kitambaa ndani
ya tumbo la
mama kitu kilichopelekea kuanza kuoza
utumbo hadi kufikia
kizazi nacho kuoza na
kuharibka kabisa. Mungu
mkubwa mama huyo alinusurika kifo.
Visa vya namna
hii vya kusahau
visu, mikasi, vitambaaa kwa
akina mama wakai
wa kujifungua navyo
havina idadi nchini
mwetu. Inasikitisha sana.
3. NAMNA YA
KUMSHITAKI DAKTARI ALIYESABABISHA MADHARA.
Natoa ushauri na
hamasa kuwa imefikia
wakati sasa tuwashitaki
hawa madaktari na
serikali yao ili
kwa kulipa fidia
kubwa wawe makini
na wapate funzo
na hii itakuwa
ni salama kwa raia. Nimesema hapo
juu kuwa daktari
akisababisha dhara kwa
uzembe, kutojali au makusudi
kwa mgonjwa anashitakiwa. Namna nzuri
ya kushitaki ni
kuomba kulipwa fidia
ya hela kutokana
na madhara uliyopata
au aliyopata ndugu
yako.
Kwakuwa suala ni kutaka
kulipwa hela basi ikiwa
unataka ulipwe kuanzia
shilingi moja mpaka
milioni 100 basi
fungua shauri hilo
mahakama ya wilaya
au ya hakimu
mkazi wengi huiita
mahakama ya mkoa. Na ikiwa
unataka ulipwe zaidi
ya milioni mia
moja mpaka bilioni
au tirioni na
kuendelea basi shauri
hilo lifunguliwe mahakama
kuu. Hii ni kwa
mujibu wa sheria.
Hakikisha mahakama utakayofungua shauri
kama ni ya
wilaya iwe ni ile ambapo tukio
hilo lilitokea.
Kama ilitokea
wilaya fulani basi mahakama ya
wilaya hiyo ndiyo ina
mamlaka ya kusikiliza
shauri hilo. Na
kwa upande wa mahakama kuu
fungua mahakama kuu
iliyo katika kanda ambapo
lilitokea tukio. Na hiyo
ni kwa mujibu
wa sheria pia. Katika
kushitaki mshitakiwa namba
moja atakuwa daktari
aliyesababisha madhara, pili
utaunganisha hospitali husika ikiwa
kama mshitakiwa namba
mbili na tatu
utaunganisha halmashauri ya
wilaya husika ikiwa
kama mshtakiwa wa
tatu.
Kisheria shauri
la namna hii
huwezi kumfungulia daktari
peke yake bila
kuwaunganisha hawa waajiri wake.
Hii ni kwasababu
yale mamilioni ya
hela unayodai inabidi yalipwe na
hospitali husika au
halmashauri kwasababu wao ndio
wanaomjua huyo daktari. Katika
kesi iliyotolewa hukumu wiki
hii na jaji
wa kanda ya Tabora Jaji Amir
Mruma halmashauri
ya wilaya ya
Urambo imeamrishwa kumlipa
Mwamini Adam kiasi
cha milioni 25
kutokana na uzembe
wa daktari uliomsababishia madhara. Hii
ndio sheria na
ndivyo ilivyo tuchukue
hatua sasa.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment