NA BASHIR YAKUB-
Mara nyingi tunapoongelea
umiliki wa ardhi
watu wengi hukimbilia
kufikiri kumiliki ardhi
labda pugu, bunju, tegeta , kimara
na hata huko
mikoani. Wengi hudhani
kumiliki ardhi lazima
iwe nyumba hizi
nyumba za kawaida
tulizozoea au
kiwanja kama viwanja tulivyozoea au shamba
kama shamba. Sikatai
kuwa hizi sio
ardhi hapana
hizi ni ardhi ila
ni vema sana
kuelewa kuwa ulimwengu
umekua sana na
kila kitu kimepanuka
ikiwemo dhana nzima
ya masuala ya
ardhi. Leo tunapozungumzia suala
la ununuzi wa ardhi ni
vema tukapanua mawazo yetu
zaidi. Katika kupanua
mawazo tutaangalia kitu ambacho
ningependa watu wengi wakifahamu.
Kwa jina la
kitaalam kitu hiki huitwa
ardhi vipande.
1.NINI MAANA
YA ARDHI VIPANDE.
Ardhi vipande ni
ardhi ambayo hupatikana katika
eneo au jengo .
Kwa mfano jengo la
ghorofa kumi na
mbili laweza kumilikiwa
na watu zaidi
ya ishirini huku kila
mtu akiwa na eneo lake. Jengo
hilo laweza kuwa
limejengwa na mtu
mmoja, kampuni au
shirika lakini kampuni
au shirika hilo
likaamua kuuza vipande
vipande labda kwa
mtindo wa ghorofa
moja moja ( floor) au
mtindo wowote ambao
wao watauridhia. Ili nieleweke
vyema nisisitize kuwa siongelei kuuza
kwa maana ya kupangisha
hapana naongelea kuuza
kwa maana ya
kuuza. Hivyo basi
kila anayenunua eneo
na akalimilki
katika jengo hilo ataitwa
mmiliki wa ardhi
kipande na hicho
kisehemu anachomiliki ndicho
kinachoitwa ardhi kipande.
2. KUONGEZEKA KWA MAJENGO
MAREFU NCHINI.
Hivi karibuni kila
mtu ni shahidi
kuwa tumeshuhudia kasi
kubwa ya kuongezeka kwa majengo
marefu hasa maeneo ya
mijini. Mashirika ya umma, mifuko
ya hifadhi kama
NSSF, PPF, makampuni
binafsi, watu binafsi,
mashirika na taasisi
mbalimbali za serikali zimekuwa
zikishindana katika ujenzi
wa majengo marefu
. Kati ya
haya yapo majengo
ya biashara na
ya makazi japo
kwa kusema tu
ni kuwa yale
ya makazi bado
ni machache.
3. UUZAJI NA UNUNUZI WA
ARDHI KATIKA MAJENGO
MAREFU.
Wengi tunadhani kuwa matumizi
ya majengo yale tunayoyaona ni
upangaji tu. Ni kweli mengi
hutumika kwa upangaji
lakini kwasasa yapo
majengo mengi pia ambayo kazi
yake si tu
kupangisha bali pia
kuuzwa. Uuzaji wa
maeneo ndani ya
majengo haya humpa
mtu haki ya
umiliki sawa na
mtu anayemiliki nyumba
chanika au bunju. Suala
la unanunua kiasi
gani hutegemea zaidi
makubaliano kati ya
wamiliki wakuu na mnunuzi wa
kipande . Aidha ijulikane
kuwa suala la
uuzaji na ununuzi
wa vipande ndani
ya majengo makubwa ni geni kwa
kiasi fulani hapa
kwetu. Hii ndio
sababu pia sheria
inayolinda utaratibu mzima
wa umiliki wa
vipande ndani ya
majengo ni mpya
pia. Sheria hii
inaitwa Sheria ya Vipande No. 16
ya Mwaka 2008. Zaidi
niseme kuwa umiliki wa
vipande katika majengo hauna tofauti
na umiliki mwingine
kama tutakavyoona kupitia
haki za wamiliki
vipande hapa chini.
4. HAKI ZA WAMILIKI
VIPANDE.
Mmiliki wa kipande
anayo haki ya
kuuza kile kipande
alichonunua, kukiweka rehani( dhamana mkopo), kukipangisha, kukigawa na kukitoa zawadi,
haki ya kupata
hati ya umiliki
inayoonesha eneo la
kipande cha mnunuzi, haki ya
kutumia eneo la
kipande bila kubughudhiwa
wala kuingiliwa na
mtu yeyote. Aidha
maeneo haya huwa
na haki nyingine
ambazo huitwa haki
za pamoja ambazo
huwahusisha wanunuzi au
watumiaji wote wa
vipande ndani ya jengo
kwa
mfano haki ya
maegesho, haki ya
matumizi ya veranda,
ngazi, haki ya matumizi ya
miundo mbinu kama
maji, umeme, mashimo
ya taka na mashimo
ya vyoo na
vitu vyote vinavyofanana na
hivyo.
Kutokana na haya
yote ni ushauri
wangu tu kuwa imefika
wakati sasa Watanzania waanze
kufikiria kumiliki maeneo
hata katika majengo
marefu. Si lazima
ununue bunju au
pugu kwani yawezekana bei
ya ununuzi wa
kiwanja na gharama
za ujenzi zikalingana sawa na
gharama za ununuzi
wa kipande ndani
ya majengo haya
tunayoyaona.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment