NA BASHIR YAKUB-
Katika migogoro ya ardhi yapo
mambo mengi ambayo
hujitokeza. Yumkini hii yote
huwa ni katika
kusaka haki. Liko
jambo moja ambalo ni
muhimu watu kulijua
hasa wale ambao
tayari wamejikuta katika
migogoro ya ardhi. Mara
nyingi imekuwa ikitokea
pale ambapo mtu fulani ana
mgogoro wa ardhi
na mtu mwingine
kumwendea polisi na
kumshitaki kwa jinai
ya kuvamia ardhi
yake( criminal trespass). Ni
kweli jambo hili
lipo kisheria lakini
haliko moja kwa
moja kama ambavyo
watu wamekuwa wakilichukulia kama ambavyo
tutaona badae.
1.JINAI YA
UVAMIZI WA ARDHI.
Nimesema hapo juu
kuwa jinai ya
uvamizi wa ardhi
huitwa “criminal trespass”. Kosa
hili huhesabika limetendeka
pale ambapo mtu huingia katika
ardhi ya mtu mwingine
bila ruhusa au
mamlaka yoyote ya
kisheria kutoka kwa
mmiliki au penginepo
huku akiwa na
nia mbaya. Mtu
anapokuwa amefanya hivi
tayari huhesabika ametenda jinai
ya uvamizi wa
ardhi. Ardhi kwa maana hii
hapa hujumuisha nyumba, shamba, kiwanja na kila kitu ambacho
huitwa ardhi.
2. KESI
YA MADAI YA UVAMIZI
ARDHI.
Hapo juu nimeeleza
kosa hili la
uvamizi ardhi lakini katika
upande wa jinai. Yafaa
tujue kuwa kosa
hili pia ni
madai. Kwa hiyo
kama hapo juu
tumeona anayevamia ardhi
ya mtu anaweza
kufunguliwa kesi ya
jinai basi tuelewe
kuwa kwa kosa hilohilo
waweza fungua pia
kesi ya madai.
Tofauti ya kesi
ya madai na
jinai katika kosa
hili ni kuwa
katika kesi ya
jinai mtuhumiwa akipatikana
na hatia basi
atatakiwa kwenda jela au adhabu
nyingineyo wakati katika
kesi ya madai
mlalamikiwa akipatikana na
hatia basi atatakiwa
kulipa fidia kwa
mtendewa. Kwa hiyo
uamuzi wa kesi
gani mlalamikaji afungue
uko mikononi mwake. Aidha
yawezekana pia kufungua
kesi zote mbili
kwa pamoja yaani mahakama fulani
ukafungua kesi ya
madai na mahakama
nyingine ukafungua kesi
ya jinai kwa wakati mmoja.
3. USIPOTEZE MUDA KUMFUNGULIA JINAI
YA UVAMIZI UNAYEGOMBEA
NAYE ARDHI.
Hapo juu nimeeleza
kuwa kuvamia ardhi
ni jinai lakini
yafaa tujue kuwa
jinai hii huwezi
kumfungulia kila mmoja.
Kabla ya 1980 ilikuwa
mtu yeyote aliyevamia
ardhi yako basi
unaweza kumfungulia jinai
ya uvamizi ardhi.
Lakini baada ya
mwaka huo mwelekeo
wa sheria ulibadilika. Mabadiliko yaliekeza
kuwa ikiwa mtu fulani ana
mgogoro wa ardhi
na mtu mwingine
basi hakuna mtu
kati ya watu
hao anayeweza kumfungulia mwenzake
jinai ya uvamizi
wa ardhi. Kwa mfano
A analalamika kuwa
sehemu anayoishi B
ni sehemu yake. Kutokana na
hilo A anaamua
kwenda moja kwa
moja eneo hilo kwa
B na kukaa au
kukaguakagua na kuondoka.
Kwa mazingira kama
haya B hawezi
kumshitaki A kwa
kuvamia ardhi yake. Mfano
mwingine ni kati
ya K na
Y. Hawa kila mmoja
anaamini kiwanja fulani
ni cha kwake.
Siku moja K
anapeleka mafundi wake
na kuanza kujenga
kitendo ambacho hakimridhishi
Y na kuamua
kumfungulia kesi ya
jinai ya kuvamia
eneo lake. Kwa
kesi kama hii
Y hawezi kushinda
na kimsingi hukutakiwa
kabisa kufungua kesi hiyo.
4. ISEMAVYO MAHAKAMA KUHUSU JINAI
YA UVAMIZI.
Katuka kesi ya
KIBWANA dhidi ya
JAMHURI , TLR 321 mahakama chini ya
Jaji kiongozi Mnzava
ilisema kuwa katika
kesi inayohusu umiliki
wa ardhi mahakama haipaswi
kuendelea kusikiliza kesi
ya jinai. Iliendelea
kusema kuwa iwapo
kuna ubishi wa
nani anamiliki mahali
fulani basi shauri
hilo haliwezi tena
kuwa la jinai
isipokuwa wahusika washauriwe
wakafungue kesi ya
madai. Kutokana na hayo yote
niliyosema hapo juu
basi nishauri kuwa watu wasipoteze
muda kufunguliana kesi
za jinai katika
mazingira ya uvamizi
ardhi kwani kufanya
hivyo ni kupoteza
muda kwakuwa kamwe
hautafanikiwa katika shauri la
namna hiyo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA BOFYA HAPO JUU
MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment