NA BASHIR YAKUB-
Kipindi cha nyuma
wakati nikieleza masuala
ya sheria za ndoa
niliwahi kueleza utaratibu
wa mgawanyo wa
mali iwapo ndoa
inavunjika. Kimsingi nilieleza mgawanyo
wa mali katika
msingi wa uwepo wa
ndoa ya mke mmoja.
Sikuwahi kueleza mgawanyo
wa mali iwapo
ndoa ni ya
mke zaidi ya
mmoja. Wengi waliuliza
swali hili ambapo
baadhi niliwajibu na
baadhi sikuwajibu. Leo sasa nitaeleza
mgawanyo wa mali
katika ndoa ya mke zaidi
ya mmoja pale ambapo mmoja
wa wake inatalakiwa .
1.NDOA YA MKE ZAIDI
YA MMOJA.
Kwa jina la kitaalam
ndoa za namna hii huitwa ndoa
za mitala. Waolewaji waweza
kuwa wawili, watatu , wanne, watano
au zaidi neno
mitala hubaki kuwa
mitala. Sheria yetu ya ndoa
inatambua ndoa ya mke zaidi
ya mmoja na
hivyo kwa waliofanya
hivyo hawajatenda dhambi yoyote kisheria. Ndoa za namna
hii mara nyingi
zimekuwa zikifungwa
na waislamu au
watu ambao huishi
maisha ya kufuata
mila ambao wengi
wao wako vijijini.
Hata hivyo tumeshuhudia
mazingira ya ndoa
za namna hii kwa
watu ambao ni wa makundi
tofauti na niliyotaja kwa
siku za hivi karibuni. Yote kwa yote
hizo ndio ndoa
za mitala.
2.ISEMAVYO SHERIA YA NDOA KUHUSU MKE
ZAIDI YA MMOJA.
Kifungu cha 57 cha
sheria ya ndoa
kinaweka wazi kwa
kusema kuwa, katika sheria
yoyote ile mwanaume
anapokuwa na wanawake
wawili au zaidi
wanawake hao wanatakiwa
kuwa na haki
sawa mbele ya macho ya
sheria na si
vinginevyo. Kawaida tumezoea
kuna u bi mkubwa
na u bi mdogo. Basi ieleweke kuwa hayo
ni mambo ya kwetu
lakini sheria haina
u bi mkubwa
wala u bi
mdogo. Sheria inajua
mke ni mke awe alianza
kuolewa au ameolewa mwishoni. Wake
wote wana haki
sawa mbele ya
mme wao na mbele
ya sheria na huo ndio
msimamo wa sheria.
3.MGAWANYO WA MALI UKOJE
IWAPO MKE MMOJA
AMETALAKIWA.
Katika hili msimamo
wa sheria ni kuwa
japo wanawake ni
wengi na mtu
aliyewaoa ni mmoja bado kila
mwanamke ana mgao wake
ambao uko tofauti
na mwingine iwapo
ndoa ikivunjika. Hapo juu
tumeona sheria ikisema
wanawake walioolewa na
mme mmoja wana haki
sawa. Ni kweli wana
haki sawa lakini
ili haki sawa ipatikane ni
lazima baadhi ya
mambo ya msingi
yazingatiwe. Ili mke fulani amzidi
mwingine katika mgao
wa mali ndoa inapovunjika
kitu kikubwa kinachozingatiwa ni
mchango wake katika
upatikanaji wa mali
zilizopo.
Ikiwa mchango
wa mwanamke fulani
ni mkubwa basi
atachukua kikubwa na
ikiwa mchango wake
ni mdogo basi
atachukua kidogo. Kubwa zaidi ni kuwa
kila mwanamke atachukua
kile kinacholingana na
mchango wake katika
upatikanaji wa mali
husika. Katika mgawanyo wa
mali za ndoa
sheria haikuweka msimamo
wa kiasilimia kama ilivyo
katika mambo mengine
ya mirathi n.k. Katika
hili sheria humtaka kila
mhusika kuthibitisha amechangia
nini ili apate haki
yake kutokana na
mchango huo.
4. BI MDOGO
ANAWEZA KUPATA MALI
NYINGI KULIKO BI MKUBWA.
Kwa msimamo wa nilichoeleza
hapo juu basi
yawezekana bi mdogo
akapata mali nyingi
kuliko bi mkubwa
iwapo ndoa yake
itavunjika.
Yawezekana bi mdogo
ameolewa miaka kiwili
tu lakini lakini
fedha yote ya
kujengea nyumba za
familia imetoka kwake au
nusu yote imetoka
kwake au kiasi
cha pesa kilicholeteleza upatikanaji wa
viwanja na magari
n.k. kilitoka kwake. Na
ikawa bi mkubwa
pamoja na kukaa
kwenye ndoa zaidi
ya miaka thelathini
lakini mchango wake
ni mdogo au
ni wa kawaida
ambapo hakuwahi kuchangia
chochote zaidi ya
mchango wake wa
kazi za nyumbani.
Kimsingi mchango wa
kazi za nyumbani
ni mchango na
unatambulika isipokuwa kwa mazingira niliyoeleza
hapa mchango huo
hauwezi kustahili mgao
sawa na wa
bi mdogo
aliyetoa pesa yote
au nusu mpaka mali
hizo zikapatikana.
Nimalizie kwa kukumbusha
kuwa kitu kikubwa kinachozingatiwa
katika
kugawana mali iwapo ndoa ya
mke zaidi ya mmoja imevunjika
ni kuangalia mchango
wa kila mmoja au
mchango wa anayeondoka
katika juhudi za
upatikanaji wa zile
mali. Kila mtu
atachukua kulingana
na mchango wake
baada ya kuudhibitisha.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
0 comments:
Post a Comment