NA BASHIR YAKUB-
Suala la matunzo ya watoto/mtoto lim ekuwa
ni suala ambalo wasomaji
wengi wamekuwa wakiniuliza sana. Wengi wao
wanaouliza ni wale
ambao wamezaa nje
ya ndoa na
hivyo kuna utata
wa matunzo ya
watoto na wale
ambao wamekuwa wana ndoa lakini
sasa tayari wametengana
aidha kwa talaka
au bila talaka. Niseme tu
kwa ufupi kuwa suala
la matunzo ya watoto
linajumuisha mambo mengi nami
nitaeleza baadhi
tu.
1.HUWEZI KUMLAZIMISHA
MTOA MATUNZO KUTOA AMBACHO HANA.
Kumekuwepo na tabia
ya wazazi hasa
upande wa wazazi
wa kike kuwalazimisha wanaume
ambao wamezaa nao na
kutengana nao
kutoa matunzo ya
watoto kwa kiwango
cha juu kabisa
ambacho pengine kinazidi
hata kipato cha
mtoaji. Hili si sawa.
Ni kweli sheria inamlazimisha
mwanaume kutoa matunzo
ya mtoto lakini
haimlazimishi kutoa kuliko
anachopata. Sheria haiseme kwakuwa
mwanamke anaishi na
mtoto wa mtu
basi mwanaume ndio sasa afanywe
kitega uchumi. Inafikia
hatua mwanamke hafanyi
kazi yoyote isipokuwa
anategemea ile pesa
ya matunzo ya mtoto ndio
iwe kila kitu
katika maisha yake.
Hii ndio sababu
hata akipewa kiasi
kinachotosha haoni kama
kinatosha kwakuwa kinakuwa na njia nyingi
kama saluni, nguo za kuvaa, pesa
ya upatu, michango ya
harusi na kitchen party
na kila kitu kinachohusu maisha
yake binafsi. Ieleweke wazi kuwa
kwa mujibu
wa sheria pesa
ya matunzo ya mtoto haihusiki
na haya. Pesa
ya matunzo ya
mtoto ni pesa
ya matunzo ya mtoto kama neno
lenyewe lilivyo na linavyojieleza
si vinginevyo.
2.INARUHUSIWA KUKATAA
IKIWA UNALAZIMISHWA KUTOA
MATUNZO YANAYOZIDI UWEZO WAKO.
Ikiwa mwanaume analazimishwa
kutoa kuliko kipato
chake basi anaruhusiwa
kukataa hata kama
amri hiyo imetolewa
na mahakama. Wengine huandikishana
polisi lakini bado
haibadili maana kwakuwa
mtu anatakiwa kutoa
kulingana na uwezo wake
au kipato chake. Wapo
wazazi hasa wa kike
ambao huwalazimisha wanaume
kutoa matunzo ya kuwasomesha
watoto international schools
wakati kipato cha
mwanume ni shule
ya kata. Sheria inachokataza
ni kukataa kabisa
kutoa matunzo ya mtoto
lakini haimlazimishi mtu kutoa kilichomzidi. Au
wengine hulazimisha kuwekewa
mpaka wafanykazi wa
ndani( house girl) wakati kipato
cha mwanaume hakiruhusu
jambo hilo.
Huu nao ni
unayanyasaji kwa upande
wa wanaume na
haukubaliwi na sheria. La
msingi ni kuwa
iwapo utalazimishwa kutoa
kuliko uwezo wako
we kataa. Na
kama uamuzi huo
umetolewa na mahakama
basi kataa kwa kukata
rufaa kupinga kabisa
jambo hilo. Sheria inaposema
matunzo ya watoto
haisemi kuwa watu
watoe kuliko uwezo wao hapana.
Sheria ni haki
na haki huzingatia
ukweli na hali
halisi ya jambo.
3. UMRI WA
WATOTO KUISHI NA
MAMA AU BABA.
Mara nyingi sheria hasa mahakama imeelekeza watoto walio
chini ya umri
wa miaka kumi
yaani kuanzia miaka
tisa kushuka chini kuishi na
mama japo umri halisi ulio katika sheria ya ndoa ni miaka saba kushuka chini. Kuanzia
miaka kumi kwenda
mbele mtoto anaweza
kuchagua aishi na nani kati
ya baba au
mama. Kwahiyo iwapo
mtoto amefikisha umri
wa miaka kumi
au zaidi basi
baba anaweza kumchukua
mtoto wake iwapo
pia mtoto atapenda
kukaa na baba
yake. Wapo wazazi ambao wamekuwa
wakiwagangania watoto hata
baada ya watoto kuvuka
umri huo ili
waendelee kuwafanya vitega
uchumi kupitia kudai
matunzo. Hili si sawa
hasa iwapo mtoto
yuko tayari kukaa
na baba yake.
4. BABA ANAWEZA
KUOMBA KUKAA NA
WATOTO HATA KAMA
NI WADOGO SANA.
Hapo juu tumeona
kuwa ni lazima
mtoto kukaa na mama iwapo
ana umri chini
ya miaka kumi.
Msimamo huu unaweza
kubadilika iwapo baba
atatoa sababu za
msingi za kuomba
mama asikae na watoto. Hii haijalishi
watoto wana umri gani
iwapo tu
ana sababu za msingi
basi ataomba kukaa
na watoto/mtoto wake. Sababu kubwa
za kuomba watoto
ni iwapo mama ana ugonjwa
wa akili na
hivyo kuwa hatari
kwa ustawi wa mtoto/watoto. Pia iwapo
mama anakaa na watoto katika
mazingira hatarishi kama
danguro, baa, sehemu za madisco, au
mama anajihusisha na
vitendo vya ukahaba
ambavyo si vyema kabisa
kwa makuzi ya
mtoto. Hii inajumuisha matendo yote maovu ambayo
kukaa na watoto/mtoto
yanaweza kuleta athari
mbaya kwake na ni
hapo baba atakapoomba
kuchukua mtoto/watoto na
atakubaliwa bila kujali
umri wa watoto.
5. HAKI YA
KWENDA KUWAONA WATOTO.
Wapo watu ambao huzuiwa kuwaona
watoto. Wengine huruhusiwa lakini
kwa masharti maalum
na kwa kupewa
muda wa kuzungumza. Hii haikubaliki kisheria
mzazi anapaswa kuwaona
watoto kwa uhuru na bila
masharti yanayolenga kumwondolea
haki hiyo. Ikiwa mzazi
anazuiwa kuwaona watoto/mtoto
au anawekewa masharti
magumu basi anaweza kudai
haki hii kwa
kupeleka malalamiko ustawi
wa jamiii au mahakamani haraka
iwezekanavyo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. bashiryakub@ymail.com 0784482959, 0714047241 TANGAZO MUHIMU
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
0 comments:
Post a Comment