NA BASHIR YAKUB-
1.DHAMANA NININI.
Dhamana
ni hatua ambapo mtu
ambaye tayari ni
mtuhumiwa wa kosa fulani huachiwa
huru kwa muda
ili kusubiri hatua
za kufikishwa mahakamani
au kama tayari
amefikishwa mahakamani husubiri
kuendelea kwa kesi
yake. Kwahiyo ili lije
suala la dhamana
ni lazima uwe
umetuhumiwa polisi au tayari umefikishwa mahakamani. Ieleweke kuwa
kuna aina kuu mbili za
dhamana. Kwanza dhamana ya
polisi na pili
dhamana ya mahakamani.Hapa tunazungumzia
dhamana ya polisi.
2.UKIOMBWA HELA KWA AJILI
YA
DHAMANA KATAA.
Dhamana
hutolewa bure. Ieleweke wazi kuwa hakuna malipo yoyote yanayotakiwa kutolewa ili
mtuhumiwa au mshtakiwa akubaliwe dhamana. Mchezo huu wa kuomba
hela ili mtu
apate dhamana umetamalaki zaidi vituo
vya polisi. Wewe kama raia unalotakiwa kujua ni moja
tu kuwa hakuna
sheria inayomtaka raia
kutoa hela ili
apate dhamana. Serikalini hakuna
risiti ya malipo ya
dhamana. Kama wewe utaamua
kutoa hela hiyo ujue umetoa kwasababu
zako lakini sheria
iko hivyo.Ifikie hatua
raia wajisimamie kwa kukataa
kutoa hela kununua
dhamana.
Hakuna kitu
ambacho askari anaweza
kukufanya ikiwa utakataa kutoa hela
kwa ajili ya dhamana.
Hakipo kabisa
kinachohitajika ni ujasiri wako tu
kwa kumwambia askari
kwamba sikupi hela
kwakuwa dhamana hainunuliwi. Usikubali kutoa
hela kwa ajili ya
dhamana ndugu ni kosa na
hela hizo ni rushwa. Na hiyo
ni kwa dhamana
zote ya polisi
pia ya mahakamani. Katika taratibu za
kupata dhamana hamna
kulipa hela.
3.
POLISI WANALAZIMIKA KUKUPA DHAMANA .
Hapo
juu nimesema kuwa
ili upate dhamana
hutakiwi kutoa hela
isipokuwa kuna mambo
yanazingatiwa ili upate dhamana. Baadhi
ya mambo hayo
ni haya.
( a ) Kisheria ikiwa
makazi yako au anuani yako ya
makazi inajulikana vyema
au haijulikani lakini
umewafanya polisi kuijua na
wakajiridhisha kwamba kweli
fulani haya ndio
makazi yake basi ni sababu
ya kupatiwa dhamana. Hii ni
kwasababu lengo kuu la dhamana ni ili
utakapohitajika upatikane kwa urahisi.
( b )Pili, ikiwa kosa
alilotenda mtu ni la kudhaminika hakuna
haja ya kuendelea
kumshikilia. Sheria imeshaweka
wazi makosa yapi dhamana ya
mtu itolewe na
makosa yapi isitolewe. Baadhi ya
makosa ambayo mtu
hatakiwi kupata dhamana ni
kama kuua(murder), uhaini,wizi wa silaha n.k. Ajabu ni
kuwa kwenye vituo
vyetu vya polisi unakuta hata
mwenye kosa la
kutukana naye kanyimwa dhamana.
Hii ni
kinyume cha sheria na
muda umefika wa raia wenyewe
kuyakataa haya.
( c ) Pia kama mtuhumiwa hana
kumbukumbu (criminal records) zozote
za uhalifu nayo ni sababu au
kigezo cha kumfanya
apewe dhamana haraka. Hakuna sababu ya
kuendelea kumshikilia mtu
ambaye kwa kumbukumbu hakuwahi
kutenda kosa lolote la jinai
hapo kabla. Kisheria kutokuwa na
kumbukumbu za uhalifu hapo
awali ni dalili za
uaminifu na ukweli. Hii
nayo ni sababu ya
kisheria na yafaa izingatiwe sana
huko vituo vya polisi.
( d ) Pia ikiwa polisi itajiridhisha kwamba mtuhumiwa
atatimiza masharti ya dhamana atakayopewa kama kufika siku na saa atakayoamriwa basi hakuna
haja ya kumgangania
mtu. Hii nayo ni kati
ya sababu ya kisheria
ambayo huwa haipewi nafasi
kwenye vituo vya
polisi na hivyo kuendelea kulifanya
suala la dhamana kuwa
gumu.
4. NAMNA
YA KUJIANDAA NA DHAMANA.
Ni
vema sana unapopata taarifa za
ndugu yako kushikiliwa kituo cha
polisi kujiandaa na
dhamana. Usitoke nyumbani kwenda
kituoni bila kujiandaa
na dhamana. Na hii ni iwe una
uhakika amefanya kosa fulani au huna
uhakika. Zaidi kama unajua
kosa lake ni la kudhaminika basi
umuhimu wa kujiandaa
na dhamana huongezeka. La kuzingatia sana hakikisha
unapotoka nyumbani una
barua inayokutambulisha kwa suala
la dhamana kutoka serikali
za mitaa, ukienda serikali za
mitaa wanazijua hizi
barua. Pia kama ni
mwajiriwa usisahau kwenda na
kitambulisho chako cha kazi. Hii
husaidia kutopoteza muda kwa
kurudishwarudishwa huku ndugu yako akiendelea kusota. Kwa kujiandaa
utamwokoa ndugu yako na
dhahama ya kulala au kukaa selo. Usiende
polisi ukiwa hujajiandaa kwakuwa kufanya hivyo
ni kupoteza mda tu. .
5.
OMBA KUJIDHAMINI MWENYEWE INARUHUSIWA.
Kuna
watu wamekuwa wakikosa
dhamana kwa kukosa
wadhamini. Lakini polisi wamekuwa
hawawaelezi watu hawa
haki hii ya
kujidhamini wenyewe. Mtu akikosa mdhamini
na polisi nao
wanakaa kimya mtu anaendelea kusota. Hili
si sawa kwakuwa
moja ya majukumu waliyonayo polisi
ni kuwaelimsha watuhumiwa haki
zao za msingi. Aidha kama ulikuwa hujui
ndio ujue kuanzia
leo kuwa inaruhusiwa
kujidhamini mwenyewe na ukaondoka
kituo cha polisi
bila kuhitaji ndugu
yeyote kukudhamini. Unachotakiwa
kufanya kama uko
mikononi mwa polisi ni
kusema tu kwamba
nahitaji kujidhamini ili upewe
fomu maalum uijaze na
uondoke. Usisahau kuliomba hili
ni haki yako.
6. UMUHIMU
WA DHAMANA.
Kwanza ni kumfanya
mtu kuwa huru kama raia wengine wote na
pili ni kumfanya mtu kuwa nje ili
aweze kujiandaa kukabiliana na tuhuma zinazomkabili kabla ya hajafikishwa
mahakamani mfano kupata msaada wa kisheria.
MWANDISHI
WA MAKALA HAYA
NI MWANASHERIA NA
MSHAURI WA SHERIA
KUPITIA GAZETI LA
SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE
, GAZETI JAMHURI KILA
JUMANNE NA GAZETI
NIPASHE KILA JUMATANO.
0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
Very simple and clear , thanks