NA BASHIR YAKUB-
Watu wengi wanaonunua
ardhi wamekuwa wakipata
usumbufu mkubwa katika kubadili
majina yaani kutoka mmiliki
wa mwanzo kwenda
kwa mmilki mpya aliyenunua. Upo usumbufu ambao husababishwa
kwa makusudi na maafisa
wanaohusika lakini pia
upo usumbufu ambao husababishwa na
watu wenyewe wanaotaka
kubadili majina. Awali
ya yote lazima
nikiri kuwa baadhi
ya maafisa wa
mamlaka za ardhi
husababisha uchelewaji kwa
makusudi kabisa na lengo
likiwa kujenga mazingira ya
kupozwa kidogo. Hili lipo na kila mtu
ambaye amekuwa akishughulikia masuala
ya hati na
kubadili majina miliki
kama mimi atakiri
kukutana na haya. Hao tuwaache mimi
leo nazungumzia maandalizi ambayo
ukiyafanya mapema utafanikiwa
kwa urahisi na haraka
kubadili jina
la kiwanja au
nyumba kutoka kwa mtu
akiyekuuzia kuingia jina lako.
1.UMUHIMU WA
KUBADILI JINA HARAKA BAADA
YA MANUNUZI.
Sheria iko wazi kuwa
ambaye jina lake
linaonekana kwenye hati
ndiye mmiliki.
Kwa kauli hii
mnunuzi anatakiwa kufanya
jitihada za haraka
na za makusudi kubadili
jina mara tu baada ya
kununua kiwanja au nyumba.
Sikatai kuwa kunakuwa
na mkataba wa mauziano
lakini lazima ieleweke
kuwa mbele ya macho ya
sheria jina lililo
kwenye hati lina
uzito kuliko mkataba
wa mauziano. Usiridhike kukaa
na mkataba wa
mauziano ikiwa hujabadili
jina. Hii ni kwa
ajili ya ulinzi
wako na wa
ardhi yako.
Utakapotokea mgogoro
wa umiliki ikiwa
hujabadili jina waweza kuwa
katika hatari kubwa
ya kupoteza hasa
kama mgogoro huo umeanzishwa
na aliyekuuzia. Huu ndio ukweli na lazima tuonyane
ili tuwe salama na
mali zetu. Lakini pia hata
ukitokea mgogoro mwingine
wowote wa umiliki
kuna mambo ndani
ya sheria yataufanya
kuwa mgumu kutokana na sababu
tu kuwa ulikuwa hujabadili jina.
Hapo sijaongelea faida
nyingine za kubadili jina
kama kukopa n.k. Nishauri
tu kwa ufupi
kuwa unapojiandaa kununua
nyumba au kiwanja jiandae
pia na kubadili jina
moja kwa moja.
Hakikisha haya mawili
yanakwenda pamoja.
2. ILI KUBADILI
HATI KWA URAHISI
NA HARAKA HEBU
ANDAA NYARAKA HIZI.
( a ) NYARAKA ZA
UHAMISHO
Nayaraka za uhamisho
zinajumuisha fomu namba 29
ijulikanayo kama fomu
ya kusudio la
uhamisho( notification of
disposition) ambayo hueleza nia
na lengo la
muuzaji kutaka kubadili
jina au kuondoa
jina lake katika
hati. Hii utaandaa nakala
tatu . Pili ni fomu namba
30 ambayo hujulikana
kama fomu ya
idhibati ya uhamisho ( application for
approval of disposition). Katika
fomu hii muuzaji
pia atakuwa anatoa
idhini kwa mamlaka za
ardhi kuidhinisha hiari
yake ya kuachia umiliki
kutoka kwake kwenda kwa mtu mwingine ambaye ndiye
mnunuzi.
Mwisho ni
fomu namba 35
ijulikanayo kama fomu rasmi ya
kuhamisha umiliki ( transfer of
a right
of occupancy) ambayo
ndiyo rasmi sasa
huhamisha umiliki kutoka
kwa muuzaji kwenda
kwa mnunuzi. Hii ndiyo
humpa mnunuzi umiliki
rasmi . Pia mkataba wa
mauziano ni nyaraka
ambayo itaambatanishwa hapa.
Kwa kiwanja au
eneo ambalo halijaendelezwa ( halijajengwa) huandaliwa
kitu kiitwacho commitment
bond kikiwa kama
ziada ya nilivyotaja
hapo. Fomu zote
hizo pamoja commitment
bond hupatikana katika
ofisi za wanasheria
na huandaliwa na wanasheria.
( b ) TAARIFA
YA UTHAMINI.
Taarifa ya uthamini
ni taarifa rasmi ambayo
hutoa tathmini ya
thamani ya eneo/jengo. Lazima
umtafute mthamini( valuer)
ili athamini thamani ya
eneo/jengo lako na
hiyo taarifa iwasilishwe mamlaka za ardhi ili iweze
kupitishwa na mthamini mkuu
wa serikali Wizara
ya nyumba na makazi. Ukienda mamlaka
za ardhi uliza
utawakuta wathamini ili
wakufanyie kazi ya
uthamini ninayoongelea hapa.
( c ) URAIA
Sheria iko wazi kuwa
wanaotakiwa kumiliki ardhi ni
raia wa nchi
hii tu. Hivyo unapotakiwa kupata
hati ya umiliki
lazima pia uthibitishe
Utanzania wako. Hapa utatakiwa kuandaa nakala(copy) ya cheti
cha kuzaliwa ambayo imethibitishwa( certified) na
wakili au nakala
ya pasipoti ambayo
imethibitishwa na wakili
au kama huna
hivyo vyote basi
yakupasa kuandaa kiapo( affidavit).
( d ) ADA
Ni muhimu pia unapofanya
taratibu za kupata hati
au kubadili jina
kujiandaa na malipo
ya ada za ardhi. Ada
ziko aina tatu
kwanza stamp duty fee, consent/approval fee, registration fee. Sitaweka
viwango vya ada
hizi kutokana na
kubadilikabadilika kwake .
Mwisho niseme kuwa
ikiwa utajiandaa vyema
na haya utapata
hati kwa urahisi
au kama unabadili jina
utabadili kwa urahisi
pia. Jiandae epuka usumbufu.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
Ntakuona wapi nna masuala mengi ya ardhi ntahitaji msaada toka kwako, naona uko vizuri na unajitolea kuelimisha watu juu ya masuala ya ardhi
0754/0786-594534