NA BASHIR YAKUB-
Nimekuwa
nikiulizwa maswali mengi
kila inapotoka makala. Nami
nimeweka ahadi ya
kukusanya maswali hayo na
kuyajibu na si
kuyajibu kwa kumjibu
mtu aliyeuliza peke yake
, hapana isipokuwa kwa
kuyaweka katika makala
ili umma wote
ufaidike. Haya ni
baadhi ya maswali
ambayo nimeulizwa na haya ndiyo
majibu yake.
1.JE MALI
ALIYOPEWA MTU KABLA
YA KIFO CHA
MAREHEMU NAYO HUHESABIWA KATIKA KUGAWANA MIRATHI.
Yapo mazingira ambapo
marehemu huwa amempa
mtu/mrithi mali kabla
ya kifo. Mara nyingi
hii hujitokeza kwa
baba au mama na
mtoto ambapo baba/mama
humpa mali mwanae hata
kabla ya kifo. Hampi
ile mali kama
amemrithisha hapana isipokuwa
anaweza kumpa sehemu
ya mali pengine
ili ajenge au sehemu
ya shamba ili
alime na
wengine huwa wametoa
vitu kama magari
au hata nyumba.
Swali
ni je iwapo
mtu amepewa vitu
kama hivi au
amepewa kimojawapo kati
ya hivi ni
sawa vitu hivi alivyopewa kuhesabiwa
wakati wa kugawana
mali za marehemu
aliyempa mali hizo. Jibu
ni ndiyo, sheria inasema
iwapo marehemu hakuacha
wosia basi wakati wa
kugawana mali zake
vile vitu ambavyo alivitoa
kwa baadhi ya
watu/ warithi yafaa vihesabiwa
wakati wa mgawanyo
wa mali.
Sio kwamba mtu atanyanganywa mali
hizo hapana isipokuwa aliyekwishapewa hawezi
kupata mgao sawa
na yule ambaye
hakuwahi kupewa chochote
na marehemu wakati wa
uhai. Ambaye hakuwahi
kupewa chochote yafaa
apate mgao zaidi kuliko yule aliyekuwa
amepewa na marehermu
kabla ya kifo. Isipokuwa hali
itakuwa tofauti iwapo
marehermu ameacha wosia. Ikiwa
marehemu ameacha wosia
basi kila mtu atapata
kutokana na wosia unavyosema
bila kujali nani alikuwa
amepewa kabla na
nani hakupewa kabla. Wosia
utafuatwa hivyohivyo ulivyo.
2. JE
INARUHUSIWA KUINGIZA MALI
YA WANANDOA KATIKA
MALI ZA MIRATHI
ILI NDUGU WAZIGAWANE IWAPO MKE/MME NDIYE AMEFARIKI.
Yapo mazingira ambapo
mke anaweza kumtangulia
mume katika mauti
au mme anaweza
kumtangulia mke . Lakini mpaka
kifo kinamkuta mmoja unakuta
tayari kuna mali ambazo
zilikuwa zimechumwa na
wanandoa kwa pamoja
na hivyo kuwa
mali za familia.
Hapo hapo unakuta kuna
warithi kama watoto au
ndugu wengine na
wanataka mali zote
ziingizwe katika orodha
ya mirathi na
zigawanywe. Swali ni je sheria
inasemaje kuhusu jambo
hilo. Sheria iko wazi
kuwa katika mazingira
kama hayo huwezi kuingiza
mali zote kwenye
mali za mirathi. Kinachotakiwa kufanyika
ni kutoa kiwango
cha mgao wa
mali ambao alikuwa
anastahili marehemu kama
mgao wake katika
mali kama mwanandoa .
Kiwango hicho kikishapatikana basi
hicho ndicho kitakuwa
mali ya mirathi
ambayo ndugu na
watoto wanaostahili kurithi
watatakiwa kugawana. Mali nyingine
ya mwanandoa aliyebaki
ni makosa kuguswa
au kuingizwa katika
mali inayostahili kugawanywa
kwa warithi.
Mali yoyote ambayo
ni ya wanandoa
ni haki ya
kila mwanandoa na hakuna
ndugu yeyote mwenye
uwezo wa kumyanganya mwanandoa
aliyebaki. Iwe ni baada
ya kifo cha
mwenzake au wakati
wa uhai wa
wanandoa wote wawili.
Hivyo basi ieleweke
kuwa huwezi kuingiza
mali yote ya ndoa katika orodha
ya mali zinazotakiwa
kugawanywa kwa warithi
kabla ya kupiga
hesabu na kuweka
pembeni mali halisi za
mwanandoa aliyebaki.
3. JE MKE
ASIYE WA NDOA
ANAWEZA KURITHI.
Swali hili nimeulizwa
sana. Na nimeendelea
kuulizwa hata baada
ya kuwa nimelijibu.
Niliwahi kulijibu makala zilizopita. Lakini bado naendelea kuulizwa
swali hili na
mimi sitaacha kulijibu
mpaka kusiwe na
muulizaji wa swali
hili . Basi ieleweke wazi
kuwa mwanamke asiye
wa ndoa hata
kama anaishi na
mwanaume kwa mtindo
ambao ukiuangalia utadhani ni
mke na mume
bado ikitokea mwanaume
huyo kufa mwanamke
wa namna hiyo
hawezi kudai chochote
katika mali za yule mwanaume. Mke
halali ni mke ambaye
mahusiano yake na
mwanaume yametokana na
ndoa halali. Nje ya
ndoa halali hakuna
urithi.
Hii iko hivyo
hata kwa mwanaume asiye na
ndoa iwapo mke
atafariki. Aidha ieleweke kuwa
wakati ambao sio wa
kifo kwa
mfano wakati wa kuachana
baina ya mke na
mume ambao wameishi
kama wanandoa lakini
wakiwa hawana ndoa mwanamke
asiye wa ndoa
ana haki ya
kupata mgao wa mali. Na hii ni
ikiwa wameishi wote
kwa zaidi ya miaka miwili
kama mke na mume
na ikiwa kuna
mali waliyochuma kwa pamoja . Kwa maana
hiyo kwa mazingira
ya kuachana ya
kawaida mwanamke asiye na
ndoa anaweza kudai
mali lakini baada
ya kifo hawezi kudai
mali.
4. NINI UFANYE
IWAPO HUKURIDHIKA NA NAMNA MIRATHI
ILIVYOGAWIWA.
Iwapo kuna mtu
hakuridhika na mgao
wa mali za
marehemu basi sheria
inasema kuwa anatakiwa
kupeleka malalamiko yake
katika mahakama iliyomteua
au kumuidhinisha msimamizi
wa mirathi. Kwa kawaida
msimamizi wa mirathi ndiye
hugawa mali za marehemu hivyo iwapo
mtu hakuridhika basi
ana haki ya
kwenda kulalamikia hicho
ambacho hakuridhika nacho
na atasikilizwa na ikiwa yuko
sahihi basi atapewa
haki yake mara
moja.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
0 comments:
Post a Comment