NA BASHIR YAKUB-
Wako
watu ambao wamekuwa
wakipata matatizo mbalimbali ya
ardhi lakini wasijue
la kufanya. Kati
ya hao wapo
ambao migogoro imeanzia
mikononi mwao na
wengine wamerithi migogoro
hiyo kutoka kwa wazazi
au ndugu zao. Yote
kwa yote iwe
mgogoro umeanzia mikononi
mwako au umeurithi
bado mgogoro ni mgogoro
na lazima utafute jambo
la kufanya
ili kuumaliza. Nitakachoeleza hapa ni
namna gani waweza
kumaliza mgogoro wa
ardhi kwa kutumia vyombo
tulivyonavyo pamoja na
sheria zetu.
1.AINA ZA
MIGOGORO YA ARDHI.
Migogoro ya ardhi imegawanyika
katika namna tofauti. Pamoja na kugawanyika
katika namna tofauti lakini
bado asilimia kubwa
ya migogoro huhusisha
umiliki. Migogoro ya umiliki baina
ya watu wawili au
zaidi huku kila mmoja akidai
kuwa mmiliki halali
aidha kwa kununua eneo husika, au kudai kurithishwa, au kudai
kupewa zawadi, au kudai
kugawiwa na mamlaka
za serikali n.k. ndiyo inayoongoza . Migogoro mingine
ni kama kumiliki eneo
maeneo yasiyoruhusiwa kisheria
kama hifadhi za
barabara, maeneo maalum
yaliyotengwa kwa miradi kama
shule, hospitali n.k . Migogoro
mingine ni kuuziwa eneo
ambalo tayari mwenye
nalo ameliweka dhamana
sehemu fulani. Kwa ufupi migogoro ni
mingi hiyo ni
baadhi tu.
2. NATAKA KUMALIZA
MGOGORO WA ARDHI NIFANYEJE
Kama
unasumbuliwa na mgogoro
wa ardhi na unahitaji kuumaliza tunashauri
mambo yafuatayo ya
kitaalam.
( A )
KUFANYA SULUHU.
Hiii
ni njia ambayo
ipo kisheria na
inaweza kutumika muda wowote
kabla ya kufungua kesi
au hata baada
ya kufungua kesi. Ni njia ambayo hutumiwa na
wahusika katika mgogoro
ambapo suluhu ya mazungumzo
hufanyika na wahusika
hutumia busara zao kuelewana. Unapoamua kutumia
njia hii jitahidi
sana kupunguza msimamo mkali
ulionao kuhusu ardhi inayogombewa. Baadhi ya
mambo kama hayana
umuhimu sana amua
tu kuachana nayo
ili kuweza kumaliza mgogoro. Wakati suluhu inaendelea jitahidi
sana kushuka au
kujishusha ili kuwezesha kufika muafaka. Lengo ni
kuepuka gharama kubwa
zaidi mbeleni , kuepuka
kupoteza muda, pia kuepuka kuharibu mahusiano na wale ulionao
kwenye mgogoro. Ikiwa makubaliano
yatafikiwa kupitia hili
basi yatawekwa katika
maandishi maalum ya
kisheria na yatakuwa na
nguvu za kisheria
na hayatakiukwa tena. Na
kama mgogoro ulikuwa umeshafika
mahakamani basi yale makubaliano
yatapelekwa mbele ya hakimu
au jaji yatasajiliwa
na yatakuwa kama hukumu ya mahakama. Hii
itakuwa njia ya
kwanza ya kumaliza
mgogoro wa ardhi.
( B ) PELEKA
MALALAMIKO YAKO BARAZA LA
ARDHI LA KATA.
Migogoro midogodogo
ya ardhi kama kugombea njia, jirani kutanua
eneo mpaka kuingia
eneo lako kwa kiasi
kidogo, kutiririsha maji kwenye
eneo la jirani, kushindwa kuacha
uchochoro au kugombea
uchochoro, na mgogoro mwingine
wowote ambao thamani
ya eneo linalogombewa haizidi milioni
tatu hupelekwa baraza
la ardhi la
kata. Thamani ya eneo
linalogombewa kama itazidi milioni tatu
basi usipeleke mgogoro
huo baraza la
kata kwakuwa sheria
inakataza na hivyo
utakuwa umepoteza muda. Kila
kata uliyopo baraza
la kata la
ardhi lipo na hivyo
mgogoro wako upeleke
hapo utapatiwa suluhu.
( C ) PELEKA
MALALAMIKO YAKO BARAZA
LA ARDHI NA
NYUMBA LA WILAYA.
Ikiwa
hukuridhika na maamuzi
ya baraza la
ardhi la kata
basi waweza kuendelea
mbele kwa kupeleka
mgogoro baraza la
ardhi la wilaya. Kila
wilaya inalo baraza
lake ukiuliza maeneo
ya makao makuu
ya wilaya yoyote
utaoneshwa. Baraza hili husikiliza
migogoro mikubwa kidogo
kuliko ile ya
baraza la kata. Muhimu
hakikisha ardhi unayolalamikia thamani
yake haizidi milioni hamsini
kabla ya kupeleka
malalamiko. Sheria imesema wazi
kuwa ardhi inayolalamikiwa inatakiwa
isizidi thamani ya
milioni hamsini ili baraza
la ardhi la
wilaya liwe na uwezo
wa kutatua mgogoro
huo.
Hivyo usipate usumbufu
kwenda baraza la
wilaya iwapo thamani
ya ardhi unayolalamikia inazidi milioni
hamsini. Kufungua malalamiko katika
baraza hili utafika
lilipo baraza utaomba
kupewa fomu namba
moja utapewa na utaijaza
kwa msaada wa
afisa wa mahakama
au wewe binafsi
kama unaweza. Pia waweza
kumtumia mwanasheria katika
kuandaaa malalamiko katika
hili baraza. Pia
inaruhusiwa kumtumia mwakilishi katika kuandaa
malalamiko na kusimamiwa
mpaka mgogoro kuisha.
( D ) PELEKA
MALALAMIKO MAHAKAMA KUU
YA ARDHI.
Ikiwa
hukuridhika na maamuzi ya
baraza la wilaya
sheria inakuruhusu kupeleka
malalamiko mahakama kuu
kitengo cha ardhi. Ikiwa
utaamua kupeleka malalamiko
yako mahakama kuu
ya ardhi hakikisha thamani ya
ardhi unayolalamikia inazidi
thamani ya milioni hamsini. Ikiwa
chini ya milioni
hamsini usipeleke malalamiko
kwakuwa utapoteza muda
mwingi na baadae
kabisa utawekewa pingamizi
kuwa mahakama haina
mamlaka ya kusikiliza mgogoro huo
na malalamiko yako yatatupiliwa
mbali.
Nimalizie kwa
kusema kuwa ni muhimu sana
kujua wapi ukalalamike
hasa ukichukulia ukweli
kuwa mgogoro wa
ardhi waweza kukuta
muda wowote. Ni muhimu
kujua wapi ukapate
haki. Kujua jambo kama
hili kutakuepusha kupoteza muda kushughulikia mgogoro
katika njia ambazo mwisho
haziwezi kusaidia au hata
zikisaidia suluhu yake
si ya kudumu
na pia haina
ulinzi wa sheria. Maeneo ya
kulalamika niliyoeleza hapa ni
maeneo ya kisheria na
suluhu yake ina
ulinzi kisheria na
hakuna wa kukiuka.
MWANDISHI WA MAKALA HAYA
NI MWANASHERIA NA
MSHAURI WA SHERIA
KUPITIA GAZETI LA
SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE
, GAZETI JAMHURI KILA
JUMANNE NA GAZETI
NIPASHE KILA JUMATANO.
0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
0 comments:
Post a Comment