NA BASHIR YAKUB-
Kuongezeko kwa makampuni
na taasisi mbalimbali
kumeleteleza wingi wa
ajira maeneo mbambali
ya nchi. Mbali
na kuongezeka kwa ajira
hizi kumekuwepo na tatizo
kubwa la waajiriwa
kutojua haki zao
mbalimbali wawapo maeneo
ya kazi. Niseme
jambo moja tu kuwa
hakuna suala la msingi
kama muajiriwa kujua
haki zake. Hii ni
kwasababu kupitia kujua
haki zake ndipo
anapoweza kupata ujira stahiki, posho stahiki, masurufu stahiki, mafao stahiki,
malipo stahiki ya kuachishwa
kazi ikiwa ni
pamoja na ujumla
wa kufanya kazi kwa misingi
ya kazi.
Ni muhimu kila
mfanyakazi kupitia pitia haki
zake mara kwa
mara ili kujua nini
anapata na nini hapati. Uwe kazini au
umeachishwa bado ipo nafasi ya
kudai haki hizi
ili upate kilicho chako. Ukitegemea mwajiri
ndio akwambie haki
zako utakuwa unajidanganya
kwasababu yawezekana kabisa
faida kubwa ya mwajiri
ipo katika wewe
kutokujua haki zako. Ni
hasara kubwa kufanya
kazi bila kujua haki
zako . Kutokana na hilo leo nitaeleza baadhi
ya haki za
mfanyakazi.
1. HAKI
YA KUJUA SEHEMU
YA KUFANYIA KAZI.
Isiwe uliambiwa eneo
la kazi ni
Dar es salaam halafu ujikute
kila
siku una safari
za mikoani halafu
uambiwe eti hiyo
ndiyo kazi yenyewe,
hapana. Lazima eneo la
kufanyia kazi lijulikane
kwa mfanyakazi. Ijulikane
kuwa umeajiriwa na
eneo lako la
kazi ni Dar es salam , au
Mwanza au Kagera. Hii ina
maana kubwa kwakuwa
mfanyakazi asipojua eneo
lake la kazi
hataweza kudai malipo
yatokanayo na kufanya
kazi nje ya
ofisi . Lakini iwapo
unajua eneo lako
la kazi basi utakapokuwa nje
ya eneo la
kazi yakupasa kudai
malipo ya ziada. Kwa
hiyo hakikisha mwajiri
wako unakuainishia kwa
uwazi kabisa eneo
lako la kazi
na ulijue. Nje ya hilo
eneo ni malipo
mengine ambayo ni nje
ya mshahara wa
kawaida.
2. HAKI
YA KUJUA MAHALI/SEHEMU
MWAJIRI ALIPOKUTOA.
Waweza kuwa unakaa Mwanza
lakini mwajiri amekuitia
kazi Dar es
salaam . Au makazi yako
ni Arusha lakini
kazi iko Mbeya. Mazingira kama haya
yanazaa haki
ya msingi unapokuwa
unaajiriwa. Umuhimu wake
ni kuwa wakati
wa kustaafu au kumaliza mkataba
au ikitokea umeachishwa
kazi basi ni
wajibu wa mwajiri
kuhakikisha anakusafirisha kutoka
eneo la kazi
mpaka alipokutoa. Anatakiwa kukusafirisha
kwa kutoa usafiri
au kutoa gharama
za usafiri ukasafiri mwenyewe.
Hautoweza kupata haki hii
iwapo hujui kitu
kama hiki.
3. HAKI
YA KUJUA AINA
YA KAZI UNAYOTAKIWA
KUFANYA.
Lazima kazi unayotakiwa
kufanya ijulikane vyema. Isiwe
unafanya kila kazi
inayokuja mbele yako. Mchanganuo wa kazi
uwe wazi. Kama
ni sekretari ijulikane
kazi ni zipi
na zipi. Kama ni meneja
ijulikane kazi ni
zipi na zipi
kwa mchanganuo wenye
kueleweka kabisa. Hii husaidia
kutofanya kazi ambazo
si zako au
kufanya kazi nje
ya makubaliano. Kwa kujua
haki hii kazi
yoyote utakayopewa iliyo
nje ya mchanganuo
wa kazi zako, utapatana upya
na malipo yake
yatatakiwa kuwa nje ya mshahara.
4.HAKI YA
KUJUA MCHANGANUO WA MSHAHARA.
Mshahara ni jambo
moja lakini mchanganuo
wa mshahara huo ni kitu
kingine. Mwajiri anaweza
kukwambia mshahara ni
laki saba . Swali ni je
laki hiyo saba inagawika vipi. Ili
uendane vizuri na
haki hii mara
nyingi usiiangalie ile
laki saba isipokuwa angalia mchanganuo
wa laki saba. Lazima
mwajiri aoneshe kati
ya hiyo laki
saba mshahara kamili( basic
salary) ni upi, kodi
itakuwa kiasi gani, posho
ya usafiri itakuwa
kiasi gani, posho ya
chakula itakuwa kiasi
gani, posho ya pango
la nyumba ya mfanyakazi itakuwa
kiasi gani, fedha za
mfuko wa
hifadhi ya jamii
kiasi gani, na
makato mengine yote
ambayo hutokana na
makubaliano kati ya
mwajiri na mwajiriwa
yajulikane vyema. Hii
husaidia hata kudai malimbikizo kwa usahihi
baada
ya kazi kuisha. Huwezi
kupata stahiki zako kwa
kiwango unachotakiwa kulipwa
hasa baada ya
kazi kuisha kama huyajui
haya.
5.HAKI YA
KUJUA AINA YA
MKATABA WA KAZI.
Wapo watu ambao
wako makazini na hela
wanapata na maisha
yanakwenda lakini hawajui
wanafanya kazi kwa
mkataba wa aina gani.
Ni hatari kutojua
aina yako ya
mkataba kwakuwa utalazimika kukosa baadhi
ya haki zinazotokana
na mkataba wako
yakiwemo malipo na
posho nyinginezo. Lazima
ujue kama mkataba
wako ni wa muda
au wa kudumu. Mkataba wa
muda unao masurufu
yake na wa
kudumu unao masurufu
yake. Usipolijua hilo utayakosa
hayo masurufu. Mkataba
wa muda wa ajira
ni ule ambao
ni wa kipindi fulani kwa
mfano mwaka mmoja
lakini waweza kuongeza au
miaka miwili n.k. Kwa hiyo
ni vyema upitie
mkataba wako wa ajira ili ujue
ni wa aina ipi.
6. HAKI YA
KUJUA KAMA KUNA
KIPINDI CHA MPITO.
Kipindi cha mpito
hujulikana kama probation period. Hiki
ni kipindi ambacho
unakuwa umeajiriwa lakini
ukiwa chini ya
uangalizi maalum wa
kupima ufanisi wako
katika kazi. Ni muhimu
kuwekwa wazi kipindi
hiki kitaanza lini
na kuisha lini na
ni haki zipi ulizonazo ndani
ya kipindi hicho. Nasema hivyo kwakuwa
wapo watu ambao
wamewekwa katika kipindi hiki
kwa miaka mingi tu huku
wakikosa stahiki kamili
za ajira na pia
wakikosa hata stahiki za hicho
kipindi. Hii si sawa
na hulenga kumminya
mfanyakazi na kumfaidisha
mwajiri. Hivyo ni
muhimu uambiwe kipindi
hiki kinaanza lini
na kinaisha lini na
una haki
gani ndani ya
kipindi hicho.
Nitaendelea na haki za mfanyakazi
jumatatu.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. PIA NI KATI YA WANASHERIA WAANZILISHI WA BLOG HII . 0784482959, 0714047241
bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
0 comments:
Post a Comment