NA BASHIR YAKUB-
Hapo awali niliandika
namna sheria isivyowaruhusu viongozi wa serikali
za mitaa
kuandaaa na kusimamia
mauzo na manunuzi ya nyumba au viwanja. Nikasema kitu hicho
hakiruhusiwi katika sheria
na wanaofanya hivyo hakika
wako katika makosa makubwa. Nikasisitiza kuwa wewe ambaye
mkataba wako umeandikiwa serikali za mitaa ujue wazi
kuwa mkataba wako wa manunuzi hauna
hadhi
kisheria. Huu ni ukweli
ambao nitazidi kuusema ili kuwaepusha watu na usumbufu
na ili watu wasiendelee kuingia
katika utapeli huu. Ndio,
huu ni utapeli na ni jinai. Ni sababu hizihizi
zinazowaingiza watu wasio na hatia kwenye migogoro ya ardhi na kuwapotezea hela
zao.
1.HUWEZI KUFANYA
TRANSFER UKIWA NA MKATABA
WA SERIKALI ZA MITAA.
Kwa wale ambao waliwahi
kufanyia mikataba yao ya
manunuzi ya nyumba/viwanja serikali
za mitaa halafu wakaamua kwenda ardhi
kubadili jina watakuwa wamekutana na hiki
kitu
ninachoongelea hapa. Ikiwa ulifanya
manunuzi ya ardhi na ukasimamiwa na serikali za mitaa basi ujue
huwezi kubadilisha jina kutoka
kwa aliyekuuzia kuingia
jina lako. Na hapo
ni vyote yaani
hati au leseni ya makazi. Huwezi kabisa kubadilsha kimojawapo
kati ya hivyo ikiwa
mkataba wako ni wa serikali za
mitaa.
2.KWANINI UTAKATALIWA
KUBADILI JINA.
Sababu ni ilieile kuwa
mkataba wa serikali za mitaa
si mkataba rasmi wa kisheria. Ni
mkataba kama mikataba ya
mitaani ambayo mtu anaweza kuchomoa karatasi
kwenye daftari dogo la
mwanae la shule halafu mkaandikiana. Hauna
hadhi ya kisheria ndio maana
mamlaka za ardhi hazikubali uutumie
kubadilisha jina. Ifikie hatua
watu wayaelewe kwa dhati haya.
3. HUWEZI PIA
KUUTUMIA KUTAFUTIA HATI/LESENI
YA MAKAZI.
Hapo juu
nimezungumzia kufanya transfer kwa wanao
nunua sehemu ambazo tayari zina hati,
ofa au
leseni za makazi.
Lakini kuna maeneo ambayo hayana
hati, ofa wala leseni za makazi. Haya ni maeneo
ambayo mtu akinunua
huanza na moja
kutafuta vitu hivi. Basi ikiwa mtu
amefanya mkataba serikali
za mitaa halafu anataka kuanza
na moja kutafuta vitu hivi ajue
wazi kuwa mkataba huo kamwe hauwezi
kukusaidia kupata hati
wala leseni ya makazi. Ukienda
mamlaka za ardhi na mkataba
wako huo hakuna shaka
yoyote isipokuwa lazima ukataliwe tu. Kwa
asiyeamini basi na ajaribu.
4.NINI UFANYE
IKIWA TAYARI UNA MKATABA
WA SERIKALI ZA MITAA NA
UNATAKA KUBADILI JINA
AU KUPATA HATI.
Ili ukubaliwe
kufanya transfer au kupata
hati iwapo una mkataba
wa serikali za mitaa basi
huna budi kuandikiwa mkataba
mpya na mwanasheria ambao
pia ataudhibitisha kwa muhuri
maalum. Nje ya hatua hii huwezi
kupata hati wala
kufanya transfer . Hili ni jambo ambalo halikwepeki
na ndio maana huwa
tunapenda kuwasisitiza watu
kufanyia mikataba yao
kwa wanasheria kuepuka usumbufu
badae.
5. UTAFANYAJE MKATABA
MPYA WA KISHERIA IWAPO
ALIYEKUUZIA AMEKUFA AU HUJUI ALIPO.
Inawezekana
wakati wa kununua ulifanya
mkataba serikali za mitaa na sasa unataka kupata
hati au kubadili
jina lakini aliyekuuzia amekufa au hujui pakumpata ili ufanye naye mkataba mpya
wa kukuwezesha kupata vitu hivyo.
Au umepata taarifa za makala
haya na sasa
unataka kufanya mkataba
mpya wa kisheria lakini
hapohapo hujui aliyekuuzia alipo au una taarifa amekufa. Jibu la
sintofahamu hii ni kuwa upo
utaratibu maalum wa kisheria
wa kurahisisha jambo hili. Kwanza upo utaratibu
wa kimirathi lakini pili
upo utaratibu wa Next
of Kin na kiapo.
Utaratibu huu utakuwezesha kuandika
mkataba mpya unaokubalika
katika kufanya transfer au
kupata hati bila
kuwepo aliyekuuzia.
6. USHAURI WA KITAALAM.
Usipende kufanya mambo
kienyeji katika masuala
ya msingi sana
kama ardhi. Ikiwa unataka kununua
ardhi hata kama ni
ndogo kiasi gani
mtafute mwanasheria yeyote
akusimamie mkataba wako ili uepuke
usumbufu wa baadae. Hi ni
kwasababu hali ilivyo hata
ukisema simtafuti mwanasheria
itakuwa ni kazi bure
kwakuwa mwisho wa siku ni lazima utamtafuta tu
la sivyo ukubali kukaa
na ardhi ambayo haina
hati au ambayo
ina hati/leseni ya makazi lakini milele ikae kwenye jina
la aliyekuuzia.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. PIA NI KATI YA WANASHERIA WAANZILISHI WA BLOG HII. 0784482959, 0714047241
bashiryakub@ymail.com
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
---WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
---UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
---UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
----IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0783851726.
0 comments:
Post a Comment