NA BASHIR YAKUB-
Wosia ni jambo kati ya mambo ambayo
huwasumbua watu wengi. Sababu ya kuwasumbua
wengi ni lile
lile tu
kuwa ufahamu wa mambo ya sheria haujawa wa kutosha katika jamii. Tatizo la wosia limepelekea
magomvi makubwa ya kifamlia hasa wakati wa misiba
au baada ya misiba. Pia wakati mwingine ni tatizo hilihili ambalo limewafanya baadhi ya watu tena ndugu kugombea maiti. Kama watu wanaelewa vyema habari ya wosia na haki
za kila mtu katika wosia sioni haja ya ndugu kugombea maiti au baadhi ya mambo ambayo marehemu pengine ameyatolea ufafanuzi kabla ya kifo
chake. Kuna wosia wa aina mbili,. Kwanza wa maandishi na pili wa
maneno. Leo sisi tunaangalia wa maneno
lakini kwanza wosia ninini.
1.
1. WOSIA
NINNINI.
Tangazo la Serikali Nambari 436
la mwaka 1963 ambalo linajumuisha
sheria za kimila linatafsiri wosia kama, “kauli inayotolewa na mtu
wakati wa uhai
wake kwa hiari
yake kuonesha nia yake jinsi
gani angependa mali yake
igawanywe baada ya kufa
kwake.
Hilo ni tamko la serikali ni moja ya tafsiri ya maana ya wosia.
Pengine twaweza kusema tafsiri hii haijitoshelezi
sana . Tuna
sema hivyo kwakuwa tafsiri hiyo
haiingizi baadhi ya mambo ya
msingi japo ni tafsiri halali. Tafsiri
nzuri zaidi inayoingiza mambo
mengi ni hii,
Wosia ni tamko au
maandishi anayotoa mtu wakati
wa uhai wake akielezea mazishi
yake yatakavyofanyika
akionyesha mahali atakapozikwa
au jinsi mali zake zitaka
vyogawiwa kwa warithi wake baada
ya kifo chake.
Kwa tafsiri hii ni kwamba wosia waweza kuwa maandishi
au tamko. Lakini pia
wosia hauoneshi tu mgawanyo
wa mali za marehemu isipokuwa
unaonesha pia namna
ya kufanya mazishi na mahali
atakapozikwa mtu baada
ya kifo chake.
2. WOSIA WA MANENO NININI.
Kwanza
wosia huu wakati mwingine
huitwa wosia mdomo,
wosia maneno, au wosia
wa tamko/matamshi. Maana
ya
wosia huu ni kuwa ni
tamko analotoa mtu wakati wa uhai
wake
akielezea mazishi yake yatakavyofanyika likionyesha
mahali atakapozikwa au jinsi mali zake
zitakavyogawiwa kwa
warithi wake baada ya kifo chake. Kwahiyo hili ni tamko tu
basi.
Hapa hamna andishi lolote linalohusishwa ni mtu anaongea
kama kuongea
kulivyo.
3.WOSIA WA MDOMO LAZIMA USHUHUDIWE
MASHAHIDI WASIPUNGUA WANNE.
Wosia huu unapaswa
kushuhudiwa na mashahidi
wasiopungua wa nne. Ina maana ni kuanzia watu wanne kwenda mbele. Mashahidi
watatu, wawili, mmoja hawaruhusiwi . Aidha mashahidi hao
sio kwamba mtoa
wosia anawachagua kwa
namna anavyotaka kwakuwa
usia ni wake. Sheria
imemwekea mipaka maalum mtoa wosia anayopaswa kuzingatia wakati wa
kuteua mashahidi wake
wa wosia. Hatua hii ilizingatia matakwa
ya msingi ya jamii zetu. Sheria inataka
mashahidi wawili kati ya
mashahidi hao wawe
ni wa ukoo wa huyo
mwosia. Hapa
kuna mambo mawili
kuna familia kuna na ukoo.
Sheria inasema ukoo . Ukoo
ni mkubwa kuliko familia,
ni zaidi ya
fanilia . Hivyo basi sheria
inaposema mashahidi wawili watoke ndani ya ukoo
mtu asilazimishe kwamba lazima
watoke ndani ya familia.. Haya
yapo ndio maana
naweka msisitizo. Aidha wawili waliobaki
wanaweza kutoka nje ya
ukoo wa mwosia. Anaweza kuwa
jirani, rafiki wa familia
au mwingine yeyote
mtoa wosia atakayemuona anafaa kushuhudia
wosia wake.
4. KUBADILISHWA KWA
WOSIA WA MDOMO.
Wakati wowote
mtoa wosia akiamua
anaweza kufuta wosia wa awali
kwa ajili ya mabadiliko
au vinginevyo. Kama
ni kufuta kwa ajili ya
mabadiliko anaweza kuandaa
mwingine kwa mdomo
kama alivyofanya awali
huku akibadilisha mashahidi
au akitumia walewale au akabadilisha kutoka
wosia wa mdomo
kwenda wa maandishi
kwa maudhui
ile ile au kwa mabadiliko katika
maudhui.
5. WARITHI
HAWAWEZI KUWA MASHAHIDI.
Ni haramu
kisheria mmoja wa watu
ambao ni warirhi kuwa shahidi
katika wosia. Si tu
haramu bali pia ni
kihoja. Mchezaji hawezi tena
kuwa refa
6. MAMBO MENGINE
MUHIMU KATIKA WOSIA
WA MANENO.
Kwanza mtoa wosia awe amefikisha umri wa miaka kumi na
nane. Awe na akili timamu wakati
anatoa wosia huo, wosia ueleze bayana nani
atausimamia, ueleze bayana nani ni
warithi, pia zingatia sana wosia
ni siri mpaka
baada
ya kifo cha muusiaji.
7. WOSIA WA MANENO
NI KWA AJILI
YA KWA WASIOJUA
KUSOMA NA
KUANDIKA.
Izingatiwe kuwa wosia wa maneno ni
kwa ajili ya watu wasio jua kusoma na
kuandika. Anayejua kusoma
na kuandika
basi na afanye
wosia wake
kwa maandishi. Aidha wosia wa
maandishi utaelezwa vyema makala
zijazo.
MWANDISHI
WA MAKALA HAYA
NI MWANASHERIA NA
MSHAURI WA SHERIA
KUPITIA GAZETI LA
SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE
, GAZETI JAMHURI KILA
JUMANNE NA GAZETI
NIPASHE KILA JUMATANO.PIA NI KATI YA WANASHERIA WAANZILISHI WA BLOG HII 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment