Thursday 28 July 2022

MALI ZA MTU ALIYEPOTEA ZINAWEZA KUGAWIWA KWA NJIA YA MIRATHI.





Bashir  Yakub, WAKILI. - 

Ikiwa ndugu yako, mme, mke, mtoto, kaka, dada nk.amepotea kwa kipindi cha Miaka 7  na hakuna taarifa zozote kujua aliko, basi inaruhusiwa mali zake kugawiwa kwa njia ya mirathi.

Huu ni muongozo wa Mahakama kuu ya Tanzania katika Maombi No. 71/2021 .

Hata hivyo hatua hii  inakuja baada ya  kumuazimia aliyepotea kuwa amekufa. 

Maana yake sheria katika mirathi imeruhusu mtu aliyepotea kwa miaka 7 na kuendelea kumuazimia/kumtangaza kuwa amekufa.

Akishatangazwa kuwa amekufa basi haki ya kuingiza mali zake katika mirathi kwa wale wanaostahili inaibuka.

Ushahidi kuwa amepotea na haijulikani alipo ni pamoja na matangazo yenye picha yake kwenye magazeti na vyombo mbalimbali vya habari.  Ushanidi wa ndugu , jamaa,marafiki, wafanyakazi wenzake kama wapo nk.

Basi mali zake zikishaingizwa katika mirathi zitagawiwa kwa warithi halali  kama sheria husika inavyoelekeza.

Kwahiyo wenye tatizo la namna hii wanaweza kujielekeza katika utaratibu huo wa kisheria.

0 comments:

Post a Comment