NA BASHIR YAKUB -
Maudhui katika makala
haya yanatoka katika Sheria
ya Ndoa, sura ya 29,
iliyofanyiwa marekebisho 2010,
pamoja na Sheria ya Usimamizi
na Uendeshaji wa
Mirathi,Sura ya 325, R;E 2002. Ziko
aina mbili za
mali anazostahili mjane.
Kwanza ni mali
inayotokana na machumo
ya pamoja yeye
na marehemu mme
wake . Pili ni
urithi anaostashili kupata
kama mrithi wa marehemu.
Kwa mfano, mume amefariki. Lakini kabla
hajafa huko nyuma
walijenga nyumba yeye
pamoja na mke
wake. Au walinunua kiwanja
yeye na mke au gari
nk. Mme
sasa amefariki na kuacha hizo mali. Katika mali ya
namna hii kuna sura
mbili.
Sura ya kwanza ni
kuwa katika mali
hii kuna “share” ya
mme na kuna “share “
ya mke. Na “share” ya
kila mmoja inatokana
na ukweli kuwa
kila mmoja kati yao
alichangia kupatikana kwa hiyo
mali. Kwahiyo kila mmoja
ana “share” yake kutokana
na kile kiwango
alichochangia. Na mchango tulishasema kuwa sio
leta ni lete. Hata
kazi za nyumbani kama kupika, kufua, kulea watoto
nk. nazo ni mchango katka
kupatikana kwa mali.
Sura ya pili, ni
kuwa kama mume
amekufa basi mwanamke kama
mke halali anastahili
urithi kutoka mali
za mumewe. Urithi huu
utatoka katika zile
mali anazomiliki mumewe yeye
kama yeye. Urithi utatoka katika “share” ya mume
na si katika “share” nyingine.
Kwahiyo katika mali
ileile mjane atakuwa
na haki za
aina mbili. Haki ya
kupata
sehemu yake aliyochangia
katika kupatikana kwa
mali, na haki
ya kurithi mali ya
mme wake.
1.INAVYOFANYIKA.
Kinachotakiwa
kufanyika ni kuwa, kwanza kabisa
itatolewa sehemu ya
mali ambayo inahesabika kuwa
ni mchango wa
mke katika kupatikana
kwa ile mali na
itawekwa pembeni. Kwa
mfano , kama ni nyumba ya
vyumba sita na pengine mchango wa
mke na mme
ni nusu kwa
nusu, basi vyumba
vitatu vitawekwa pembeni
kama sehemu ya mchango wa
mke katika kupatikana
kwa hiyo nyumba.
Kwahiyo vitabaki vyumba
vitatu ambavyo ni
vya marehemu mme. Sasa
hivyo vyumba vitatu
vilivyobaki ndivyo vinavyotakiwa kuwekwa
mezani kama mali
inayotakiwa kurithiwa na warithi wote
wakiwemo watoto na
yeyote anayestahili kurithi
kisheria.
Kwakuwa mjane naye
ni mrithi kati ya
warithi wa kisheria
bado kumbe naye
anastahili mgao katika
vile vyumba vitatu vya
marehemu vilivyobaki. Hivyo
basi katika kugawa
vile vyumba vitatu vya
marehemu kwa warithi basi
na mjane naye atapewa
mgao wake lakini safari hii kama
mrithi halali.
Hoja kuwa alishapewa
vyumba vitatu mwanzoni
haitakuja hapa kwakuwa
ule haukuwa urithi
bali jasho au deni
lake kwenye ile mali. Urithi
sio jasho bali
mapenzi ya mtoa wosia
na matakwa ya lazima
ya kisheria kwa watu ambao lazima
warithi akiwemo mjane.
2. UTARATIBU
BAADA YA MIRATHI.
Katika mazingira
ya jambo kama hili
kinachoanza ni kumpata
msimamizi wa mirathi.
Na msimamizi wa
mirathi anaweza kuwa
ameteuliwa na marehemu
kwenye wosia au kama hakuna
wosia atateuliwa na
ndugu/wanafamilia na kuthibitishwa
na Mahakama. Lakini hata kama atakuwa ameteuliwa
na marehemu kwenye
wosia ni lazima
athibitishwe na mahakama.
Baada ya kupatikana
msimamizi wa mirathi kwa
utaratibu basi ni
hapo ambapo mjane anaweza
kudai haki ya kwanza ya
machumo ya pamoja(share) katika mali zizilizoachwa
kabla ya mgao
wa mirathi kuanza
kwa warithi. Haki hii
ataidai kwa msimamizi
wa mirathi.
Kama mjane ndiye
msimamizi wa mirathi
basi haki hii ya
machumo ataidai kwa warithi. Kama hakuna mgogoro
atapewa sehemu yake
ya machumo na
baadae sehemu yake ya urithi.
Na kama kutakuwa
na mgogoro au
ubishi basi mjane
atafungua malalamiko mahakamani
kuiomba mahakama itoe
tamko(declaration) kuhusu kupatikana
kwa sehemu yake
ya machumo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment