NA BASHIR YAKUB -
Mwanamke ameachwa na
mume wake wa
zamani. Lakini hajamuacha
kisheria. Hakumpa talaka
isipokuwa waliachana tu
kila mtu akaendelea
na maisha yake tena
kwa muda sasa.
Wewe umekutana na
huyo mwanamke na
umeanzisha naye mahusiano.
Umeanza kuishi naye au
umeamua kabisa kumuoa.
Ulimuuliza kuhusu mahusiano
yake ya zamani akakueleza
bila kukuficha yaliyomsibu.
Na wewe ukaona kwa kuwa
tayari hayuko na
huyo mume wake
wa zamani kwa
muda mrefu au
muda kiasi basi
haina shida. Kitu cha msingi kwako
ulichozingatia ni kuwa
hawa watu hawako
wote tena kwa maana mahusiano
yao waliyasitisha.
Je sheria inasemaje
kuhusu hali hii. Je
kukaa na mwanamke
wa namna hiyo kwa maana ya
kuishi naye bila
ndoa, au kuishi
naye kwa ndoa
au kuwa naye
katika mahusiano bila kuishi
naye kumezungumziwaje na sheria. Je
uko salama. Je
hakuna lolote linaweza kukutokea
likakusababishia usumbufu, gharama,
na kurehani mustakabali
wa maisha yako.
Je nini ufanye
ikiwa umo katika
hali kama hiyo.
Haya na mengine
yataelezwa hapa chini. Sura
ya 29 ya sheria
ya ndoa , iliyorekebishwa mwaka
2010 itatupatia majawabu
ya maswali haya.
1.NI WAKATI
GANI NDOA HUHESABIKA
IMEVUNJIKA.
Ndoa ni zao
la sheria na
kufa kwake hufa kisheria.
Ndoa haivunjiki isipokuwa
taratibu za kisheria
zimefuatwa. Ndoa inaweza
kuvunjika kwa kifo
cha mmoja wana
ndoa, kwa kupotea
kwa mda mrefu
na kuihisiwa kufa
kwa mmoja wa
wanandoa( presumption of death), lakini pia
ndoa hufa/huvunjika kwa
talaka.
Kama mojawapo ya
hayo juu halijajitokeza ndoa hiyo
bado inaishi. Kwahiyo
mwanaume unatakiwa kujua
kuwa mwanamke uliyemuoa
au unayeishi nae
bila ndoa au
uliye naye tu katika
mahusiano ya kawaida
, ikiwa hapo awali
alikuwa katika ndoa
na mojawapo ya
yaliyotajwa hapa juu
hayajatokea basi mwanamke
huyo ndoa yake
bado inaendelea. Hapo
badae itaelezwa hatari kubwa zinazokukabali .
2. JE
KUTENGANA NI TALAKA.
Unaweza kudhani kuwa
uko salama kwasababu
una uhakika mwanamke
uliyenaye ametengana na
mme wake wa
mwanzo na hivyo
wewe uko salama. Kisheria kuna
tofauti ya kutengana
na kuachana/kutalikiana. Kutengana
sio talaka. Talaka
ni talaka mpaka
itolewe kwa mujibu
wa sheria.
Pia kutelekeza sio
kuachana/talaka. Watu wanaokuwa
wametengana au
wametelekezana bila talaka
fahamu kuwa watu
hao kisheria bado
ni wanandoa.
3. KIFUNGO
CHA MIAKA 3.
Kifungu cha 152 ( 1) cha
sheria ya ndoa
kinakifanya kitendo cha kufunga ndoa
na mwanamke ambaye
bado ndoa yake
haivunjwa kisheria kuwa
kosa.
Kifungu kidogo ( 1
) na ( 2 ) kinasema kuwa mme
aliyemuoa mke huyo
na mke mwenyewe
aliyeolewa wote kwa
pamoja wanahesabika kutenda
kosa hili. Na
kifungu kidogo cha (
3 ) kinasema kuwa
hao wote wawili
wakithibitika kutenda kosa
hilo basi adhabu
yao ni kifungo
kisichozidi miaka 3
jela.
Lakini pia kifungu
kidogo cha ( 4 ) kimemuingiza
kila mtu ambaye ameshiriki kwa namna moja
ama nyingine katika ndoa
hiyo kuwa ametenda
kosa na adhabu
yake kuwa kifungo
kisichozidi miaka mitatu
kama ilivyo kwa
wahusika wakuu.
Kwa ujumla hili linahesabika
ni kosa la
mwanamke kuolewa mara mbili na
wanaume wawili tofauti
kwa wakati mmoja(Polyandry).
Aidha kuishi naye
tu bila kumuoa mwanamke
ambaye ndoa yake
haijavunjwa kisheria au
kuingia naye katika
mahusiano ya kimapenzi
bila kuishi naye,
ni kosa la
zinaa( adultery) . Sheria yetu inatambua kosa la zinaa.
Kifungu cha 72
cha sheria ya
ndoa kinatoa adhabu ya kulipa fidia
kwa atakayezini na mke
wa mtu au mme
wa mtu.
Ni vema kujihadhari
ili kuepuka kuingia
katika msukosuko wa
sheria. Hakikisha mwanamke
anapata talaka kwa
mujibu wa sheria
halafu wewe sasa
uendelee naye kwa
amani. Usiseme huyu si ameachika tuu,
hapana, hakikisha amepata
talaka.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
safi tunapata kutambua tusichokijua