NA BASHIR YAKUB----
Vijana
wengi wajasiriamali wadogo wamefungua
makampuni. Hakika wote waliofanya hivi wamefanya jambo jema
linaloendana na wakati. Niliwahi kuandika wakati nikielekeza namna nyepesi kabisa ya
kufungua kampuni kuwa, ni vigumu kwa leo kufanya biashara na ukawa
na mafanikio nje ya kampuni. Nikasema hata kama unauza maziwa,
mama ntilie, unauza mayai, kibanda cha huduma ya fedha kupitia simu,unauza
mihogo, haizuiwi kufungua kampuni. Kuna kampuni hata za
mtaji wa milioni moja na pesa hiyo si lazima uwe nayo mkononi ila ni
katika maandishi tu. Nikasema
anayetaka mafanikio kwa sasa ahakikishe hiyo
biashara yake ndogo kabisa anaifungulia kampuni. Kwakuwa wapo wengi ambao
tayari wamefungua makampuni basi zipo changamoto nyingi wanazokumbana nazo na kubwa zaidi ni taarifa au ujuzi wa mambo mbalimbali ya namna
ya kuendesha kampuni ili kampuni iwe kampuni
kweli. Moja ya eneo lenye shida au ambalo wajasiriamali
wadogo hawana taarifa nzuri kuhusu ni taarifa za kodi zinavyolipwa na kampuni kisheria. Hawajui ni kiasi gani, kwa muda gani na vipi.
Leo hapa nitaeleza kwa uchache kuhusu kodi
za kampuni. Kampuni hulipa kodi ya mapato, swali ni
kodi ya mapato nini.
1.
1. KAMPUNI HULIPA KODI YA
MAPATO, JE KODI YA
MAPATO NINI ?
Kodi ya mapato Tanzania ni tozo kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inayotokana na vyanzo vitatu ambavyo ni ajira, biashara pamoja na
uwekezaji. Aina hii ya kodi inatozwa kwa mamlaka ya Sheria ya Kodi ya Mapato ya
mwaka 2004, kama ilivyorekebishwa.Kwa upande wetu wa kampuni kodi inayolipwa kwa tafsiri hiyo hapo juu ni
kwakuwa kampuni ni biashara na pia ni kwakuwa ndani kampuni waweza kuwamo
uwekezaji.Hii ndio sababu kampuni hulipa kodi ya mapato.
2.
JE
WAJUA KUWA SI KILA KAMPUNI
HUTAKIWA KULIPA
YA MAPATO.
Mjasiriamali anatakiwa kujua kuwa si kampuni zote hutakiwa kulipa
kodi ya mapato. Kampuni zinazotakiwa kulipa kodi ya mapato ni kampuni zenye Dhima ya ukomo. Kampuni zenye dhima ya ukomo ni zile
zote ambazo ni Limited. Kama kampuni
yako ni Limited (LTD) basi inatakiwa kulipa kodi ya mapato. Nyingine zinazotakiwa
kulipa kodi ni kampuni za kudumu za ndani
na matawi ya Kampuni za wageni/wasio wakazi. Hizi
hazihusiki na wajasiriamali sitazifafanua zaidi.
Aidha,kama kampuni
umeiunda na umeingia ubia na
kampuni nyingine basi hutakiwi kulipa
kodi ya mapato.
3.
USIOGOPE KODI HUTOZWA KATIKA FAIDA
TU NA SI KUTOKA KILA FEDHA UNAYOINGIZA.
Kodi ya mapato ya kampuni hutozwa kwenye faida tu
iliyotokana na shughuli za biashara za
kampuni au faida uliyoipata kutokana na uwekezaji. Umeunda kampuni umempata mtu ana
mtaji akawekeza mtaji, faida inayopatikana hapo ndiyo faida kutoka
katika uwekezaji. Ifahamike kuwa
si kweli kuwa kila unachoingiza lazima kilipe kodi.
4. JE MAMLAKA
YA
MAPATO WANAJUAJE FAIDA ULIYOPATA ILI WAKUTOZE KODI
SAHIHI.
Hapo juu tumeona kuwa
faida tu ndio hutozwa kodi ya mapato lakini tujiulize swali, biashara unafanya
wewe ,akaunti za kampuni unazo wewe, kila kitu kuhusu kampuni yako ni wewe, je
hawa watu wa mapato wanajuaje faida
unayopata ili wakutoze kodi sahihi .Kuna yafuatayo ;
( a ) Kuna kitu kinaitwa utangazaji wa Mapato na Kodi ambacho ni tamko
linalowasilishwa TRA kuonesha mapato na kodi inayopaswa kulipwa kwa kila mwaka
wa mapato. Kwa mujibu wa sheria ya kodi, kampuni inalazimika kuwasilisha
makisio hayo hata kama haina faida. Wewe
mwenyewe unajitathmini umepata nini na unatakiwa kulipa nini na unapeleka
mwenyewe makadirio hayo. Kinyume chake ni kosa na asiyefanya hivyo adhabu inamsubiri.
( b ) Hesabu za makadirio hayo unayopeleka TRA lazima ziwe zimefanywa na mhasibu
ambaye anatambuliwa na bodi ya uhasibu Tanzania na kukaguliwa na mkaguzi wa
hesabu anayetambulika pia. Hawa ndio wanaotegemewa na TRA kupeleka ukweli wa umepata
faida kiasi gani na unatakiwa ulipe kiasi gani. Ndio maana wanaitwa wahasibu
wanaotambulika.
5. KODI YA KAMPUNI NI 30% TU YA FAIDA.
Kiwango
kinachotumika cha kodi ya mapato ya kampuni ni kukatwa asilimia 30 ya faida, na
kwa kawaida hulipwa katika hatua mbili. Kodi ya kwanza hulipwa kulingana na
makadirio ya mlipa kodi mwenyewe mwanzo wa mwaka wa biashara kama nilivyoonesha
hapo juu, na kodi ya mwisho hulipwa baada ya utathmini rasmi wa mapato kamili
mwisho wa mwaka wa mapato.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. PIA NI MKURUGENZI NA MWANZILISHI WA BLOG HII 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment