NA BASHIR YAKUB----
Katika makala iliyopita nilisema kuwa
vijana wengi wajasiriamali
wanaofungua biashara
za makampuni wanao uwezo mkubwa wa kufika mbali isipokuwa
tatizo lao ni taarifa za
mambo mbalimbali kuhusu uendeshaji wa kampuni hizo. Mambo ya uendeshaji wa kampuni ni mepesi
sana na
yanawezwa na mtu yeyote isiopokuwa tatizo
ni taarifa
na elimu ya namna ya uendeshaji
kisheria ili kampuni
ionekane ni kampuni.
Nilieleza namna kampuni inavyolipa kodi na taratibu za kikodi
za kampuni. Leo tuangalie kipengele
kingine cha uendeshaji
wa kampuni ambacho ni namna ya kupata leseni ya
biashara.
1. KAMPUNI ULIYOSAJILI
HAIWEZI
KUANZA KAZI BILA LESENI YA
BIASHARA.
Wajasiriamali
wengi wanaofungua kampuni wanajua kuwa ukishapata usajili wa kampuni basi unakuwa umemaliza kila kitu na unaweza
kuanza biashara. Wazo hili
si la
kweli kwakuwa baada ya kampuni
kuwa
imepata usajili na unataka
kuanza biashara ni lazima uwe na leseni ya biashara (business licence).
Kwa maana hii
kumbe mchakato wa kuanza biashara
na kampuni hauishii kwenye kupata
usajili wa kampuni.
Cheti cha kuzaliwa
kwa kampuni yako ( certificate of
incorporation) ni tofauti na
leseni ya biashara.Na
ili biashara ya kampuni ianze
kisheria lazima uwe
navyo vyote viwili.
2.
2. LESENI YA BIASHARA HUTAFUTWA WAPI.
Leseni za biashara zote
hupatikana manispaa. Kama wakati wa
kusajili kampuni uliandika
kuwa ofisi ya
kampuni yako (Registered
Office) itakuwa wilaya fulani basi leseni inatakiwa kufuatwa
katika manispaa
ya wilaya hiyo. Kwa
mfano uliandika kuwa ofisi za kampuni zitakuwa Kinondoni, hii ina maana kuwa
ukitaka leseni ya biashara lazima
uifuate manispaa ya
kinondoni na si
kwingine.
3.
3. MWENYE SIFA ZIPI ANARUHUSIWA
KUPATA
LESENI YA BIASHARA.
Sifa ya
kwanza ni kuwa mtu yeyote
raia wa Tanzania anayo haki ya
kupatiwa leseni ya biashara.
Pili Mtu huyo awe ametimiza umri wa
miaka kumi na nane (18).
Tatu awe na akili
timamu. Nne awe na eneo la kufanyia
biashara linalokubalika
kisheria. Aidha utaratibu uko tofauti kidogo kwa mtu
ambaye
sio raia wa Tanzania.
Mtu ambaye sio raia wa
Tanzania hawezi kutafuta
leseni ya biashara ikiwa hajapata
kibali maalum kutoka
idara ya
uhamiaji. Kibali
hicho lazima kiwe kinaonesha
biashara aliyokuja kuifanya
nchini na kazi
hiyo hiyo iliyo kwenye
kibali hicho ndiyo
tu itakayotolewa leseni
na manispaa.
4. KUPATA
LESENI
BILA USUMBUFU
NENDA NA VIAMBATANISHO HIVI.
(i) Kama
ni mtu binafsi
nenda na jina
la Biashara ulilochagua
na kama ni kampuni
nenda na (Certificate of Incorporation or Registration).
(ii) Pia kama
ni kampuni nenda na Memorandum and Article of Association” .
(iii) Nenda na Kitambulisho
cha mpiga kura,
Cheti
cha kuzaliwa
au Hati ya kiapo kuonyesha kuwa ni Mtanzania na kama ni
mgeni Hati ya kuishi
nchini daraja la
“A” (Residence Class
“A”).
(iv) Usisahau
hati ya kiuwakili
(powers of attorney) kama wenye
hisa wote wa
Kampuni wapo nje ya nchi.
(v) Pia lazima uende
na ushahidi wa kimaandishi kuonesha kuwa una
mahali
pa kufanyia biashara
. Ushahidi wa kimaandishi waweza kuwa hati za
nyumba za
mahali utakapofanyia biashara , mkataba wa pango
la sehemu uliyopanga kufanyia
biashara, risiti za malipo
ya kodi za
majengo au ardhi za
mahali utakapofanyia biashara.
(vi) Kumbuka
kwenda na hati ya kujiandikisha
kama mlipa kodi TRA (TIN) .
Ukiwa na
vitu hivi hautapata
usumbufu kupata leseni
ya biashara na utakuwa
umeepuka nenda
rudi.
5. FOMU YA
MAOMBI YA LESENI
YA BIASHARA NI
HII.
Maombi ya
leseni ya biashara
yana fomu maalum iitwayo 9TFN
2110 kwa jina la
kitaalam. Hii ndiyo mwombaji anatakiwa
kujaza na kuambatanisha viambatanisho nilivyoeleza
hapo juu.
Fomu hizi unazikuta
kulekule manispaa. Bei
ya fomu hizi
ni Tshs 1 000/= ( Alfu
Moja tu ). Tukutane tena
katika uendeshaji wa
kampuni.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. PIA NI MKURUGENZI NA MWANZILISHI WA BLOG HII 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
asante mkuu