Na Bashir Yakub, WAKILI. -
Wako Watanzania ambao wako nje ya nchi ambao wamezaa watoto huko.
Yawezekana kwa taratibu za nchi walizomo hao watoto waliowazaa huko wanahesabika ni raia wa huko.
Au wengine huamua tu kwa hiari yao kuwabadilisha uraia watoto hao na hivyo kuwa na raia wa huko.
Yumkini,baba au mama yeye mwenyewe huendelea kubaki na uraia wa Tanzania na hali watoto sasa sio Watanzania.
Swali ni je ikiwa baba au mama huyu ana mali Tanzania hasa ardhi anaweza kuwarithisha watoto hawa ambao sio Watanzania ??.
Wote twajua kuwa kwa Sheria ya Tanzania mtu yeyote asiye Mtanzania haruhusiwi kumiliki ardhi(kiwanja, nyumba au shamba).
Hata hivyo, mahakama kuu chini ya Jaji TWAIB katika Shauri la Madai Na. 1/2011 alitoa maamuzi na kueleza kuwa mtu asiye Mtanzania anaweza kumiliki ardhi kwa njia ya urithi.
Kwa msingi huu Watanzania ambao wamezaa watoto ambao sio Watanzania kwasababu yoyote ile wanaweza kuwarithisha watoto hao viwanja, nyumba au mashamba yaliyoko Tanzania na hao watoto kuhesabika ni wamiliki.
Aidha, hawaturuhusiwa kumiliki kwa njia nyinginezo kama kununua ama kupewa zawadi kupitia waraka wa zawadi( Deed of Gift).
0 comments:
Post a Comment